Ili kuisaidia Yanga, Morrison anahitaji utulivu na heshima uwanjani

Ni hivi huyo mchezaji ashajiona ni mkubwa kuliko Yanga ndio maana anafanya upuuzi. Kitendo cha nyinyi mashabiki wa yanga kumshangilia kutembea juu ya mpira pasipo na faida yoyote mmevimbisha kichwa.
Huyo mchezaji ni mtulivu sana angekuwa ni wa kupaniki nadhani angekuwa keshapigana tangu kuanzia mechi yake ya pili kucheza hadi Jana. Sisi tunamtrgemea sana na ni Bonge la mchezaji,kazi kwenu!!
 
Yaani wewe ni muangalia mpira wa bongo uliyekubuhu tena una uswahili hasa kuliko hivyo vitendo vya kiswahili vya uwanjani
 
Huna unalolijua wewe. Umejaa u mbu×3 alosema Rage
1.Zidane akiwa kapteni na mchezaji tegemeo la ufaransa alimpiga Materazzi siku ya fainali ya kombe la dunia tena wakiwa hawana hata mpira. Je zizou hakuwa mchezaji mzuri?
2. Drogba alimzaba kibao vidic kwenye fainali ya UEFA CL 2008 tena pasi na mpira akalimwa umeme je Drogba hakuwa mchezaji mzuri!?
3. Rooney alimkita mwenzake kwenye robo fainali ya EURO 2006 kama sikosei akalimwa umeme,je Rooney hakuwa mchezaji mzuri? Mifano ni mingi. Ila nachotaka kukwambia ni kwamba Morrison ni mchezaji mzuri sana na kumpiga kwake kipepsi mwenzake haimuondolei ubora wake. Cha msingi tuungane Mimi na wewe kuwataka waamuzi wamlinde mana inafahamika wachezaji wakubwa hulindwa na referees
 
Ushauri wangu ni kuwa jamaa aendeleze kipaji chake cha komfuu maana si kwa kile kiwiko
 
Mwizi sio mtu wa kumuamini
 
Yaani wewe ni muangalia mpira wa bongo uliyekubuhu tena una uswahili hasa kuliko hivyo vitendo vya kiswahili vya uwanjani
Kwanza sioni sababu ya wewe kupanic na kumwaga mipovu yako, morrison mpuuzi tu
 
Muwe watululivu bado hamjaona vituko vya morisoni mbali na kutembea juu ya mpira pasipo na faida yoyote,amepiga viwiko ,mwisho atamuibia gari mchezaji mwenzake huyu kwa ufundi kabisa ndipo kwasu watashituka
 
Kwahiyo mifano yote hiyo uliyoitoa unataka kujustify kwamba kitendo alichokifanya Morrison kilikua sahihi?

Hata ukiwa mchezaji mzuri vipi vitendo vya kihuni kama hivyo kwenye mpira havikubaliki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…