Mwl Athumani Ramadhani
JF-Expert Member
- Sep 10, 2022
- 1,280
- 2,522
Kilio cha umeme kimetamalaki kila kona nchini kwa sasa na Hii inasababishwa na serikali kutumia chanzo kikuu kimoja cha umeme KWA zaidi ya asilimia 90 ya mikoa yote.
Chanzo chetu kikuu cha umeme ni maji na Sasa ukame ndio kisingizio kikuu,serikali inapaswa kuwekeza Katika vyanzo vingine vya uhakika kama vifuatavyo;-
JUA(SOLAR ZONE -KANDA YA KATI NA MAGHARIBI)
-Asilimia zaidi ya 60 ya mikoa yote nchini kuna jua la kutosha,hasa mikoa kama Dodoma ,singida, Tabora,kigoma,shinyanga na maeneo mengi ukanda wa kati yana jua la kutosha,mikoa hii ingetumia nishati ya jua na sio maji kutokana na ukame wa maeneo haya!
Serikali ingewekeza mifumo ya solar panels za kisasa na betri KUBWA na eneo hili lingeitwa SOLAR ELECTRIC ZONE,Umeme wa jua unatosha Sana hata kuendesha mashine za kusaga unga na mitambo mbalimbali!
CASE STUDY
-Mwaka 2015 aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Igalula ndugu Rashidi Mfutakamba aliingiza teknolojia hii kwenye baadhi ya vijiji na mradi ulifua Umeme wa kutosha Sana hadi ulitumika kuendesha mashine za unga kukoboa na kusaga,Hadi leo miradi hiyo imekufa KWA kukosa usimamizi kutoka serikali kuu,hii ni Baada ya kukabidhiwa kwa kamati za vijiji ambazo wahusika hawana elimu ya kutosha ya umeme na kushindwa kufuatilia malipo na kufanya ukarabati unaotakiwa,miradi hii Hadi Sasa imekufa na kubaki magofu ya solar na betri chakavu!
WATER ZONE (KANDA YA ZIWA NA MAENEO YENYE MVUA YA MISIMU MIWILI KWA MWAKA)
Kwenye mikoa yenye maji ya kutosha kama Kanda ya ZIWA mikoa ya kagera,MWANZA,mara na ile mikoa yenye mvua za MISIMU miwili kama kilimanjaro,njombe,mbeya na mingine ya aina hiyo,umeme wa maji utumike ili kukidhi mahitaji ya mikoa husika kuepusha mzigo mzito wa mahitaji ya umeme wa aina Moja KWA mikoa mingine ambayo haina maji ya kutosha.
BIOGAS ZONE (MIKOA ISIYO NA MVUA ZA KUTOSHA PIA INA BARIDI KALI HAMNA JUA)
Mikoa kama manyara na Arusha na baadhi ya mikoa yenye Hali kama hiyo,utafiti ufanyike wa kutosha kuibaini mikoa hii!
Hapa itumike teknolojia ya kusindika uchafu (kinyesi) kwenye matank MAKUBWA ya mikoa husika,ILI kupata gesi ya mboji (BIOGAS) na kutumika kuzalisha Umeme wa kutosha!
Najua kuna changamoto za kisheria kwenye hilo,lakini tunaweza kubadili SHERIA zinazotubana na tukawa huru na kufanya kile kinachopaswa ILI kuvuna umeme wa kutosha KWA teknolojia hii.
CASE STUDY
Wakati nikiwa chuo pale Udsm Doctor Minati wa inoganic chemistry aliwahi tufundisha umeme huu wenye changamoto kisheria huku kwetu na akasema kuwa chanzo hiki cha umeme kinatumika Sana kwao India,ipo haja ya wataalamu wetu wa umeme waende india wakajifunze Namna ya kutumia Umeme huu unavofanya kazi!
Iwapo tukiwa tayari kutumia vyanzo vya Umeme tofauti tofauti kutokana na aina ya mikoa na vyanzo vyake tutatatua mzigo wa kutumia chanzo Cha aina Moja ambacho hakitoshelezi mahitaji na kusababisha mgao wa umeme kama sasa inavyotokea nchini.
N.B
Ufungwaji wa mita za umeme na malipo ya luku za Umeme utazingatiwa kama ilivyo Sasa ILI shirika la umeme lijiendeshe lenyewe na kufanya ukarabati!
Wenye mamlaka mnaweza mkaboresha zaidi ya uandishi wangu!
Mungu ibariki Tanzania nchi yangu!