TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
Mzee mmoja akakutana na kijana aliyemuuliza:
"Unanikumbuka?"
Na yule mzee akamjibu hapana. Basi yule kijana akamwambia nilikuwa mwanafunzi wako, na mwalimu akamuuliza:
"Unafanya nini sasa, unajishughulisha na mambo gani katika haya maisha?"
Yule kijana akamjibu:
"Nilikuja kuwa mwalimu."
"Ah, wewe ni mwalimu mzuri kiasi gani, umenifikia?" Akauliza yule mzee.
"Ndio, nimekufikia. Ukweli ni kwamba, nilikuja kuwa mwalimu kwasababu ulinivutia sana hadi nikatamani kuwa kama wewe."
Yule mzee, akataka kujua zaidi, akamuuliza ni muda gani wakati alipokuwa anasoma aliamua kuwa mwalimu. Na yule kijana akamwadithia hii hadithi:
"Siku moja, rafiki yangu, mwanafunzi pia, alikuja shuleni akiwa na saa nzuri mpya, na nikaamua kuwa niliihitaji.
Niliiba ile saa, niliichomoa kutoka mfukoni mwake.
Na muda mfupi baadae, rafiki yangu akagundua kuwa saa yake hakuwa nayo tena na mara moja akalalamika kwa mwalimu wetu, ambaye ulikuwa wewe.
Basi ukaliambia darasa kuwa, 'saa ya huyu mwenzenu imeibwa wakati wa masomo leo. Yeyote aliyeiiba, tafadhali airejeshe.' Na sikuirejesha kwasababu sikutaka kuirejesha.
Ulifunga mlango na ukatuambia tusimame kwa kutengeneza duara. Ilikuwa uanze 'kutusachi' mfukoni mmoja baada ya mwingine hadi saa ipatikane.
Hatahivyo, ulituambia wote tufumbe macho, kwasababu ungeitafuta saa yake kama wote tungalifunga macho. Na tulifanya kama ulivyoelekeza.
Ukaanza kwenda mfuko baada ya mfuko, mtu baada ya mtu, na ulipofika katika mfuko wangu, uliikuta ile saa na ukaichukuwa. Na uliendelea kusachi mifuko ya kila mmoja wetu, na ulipomaliza ulisema 'fumbueni macho yenu'. Tumeipata ile saa.'
Hukunisemesha na wala hukutaja tena lile tukio. Pia hukusema ni nani aliyeiba ile saa. Siku ile ulinitunzia sana heshima yangu daima. Ilikuwa siku ya aibu kubwa sana maishani mwangu. Lakini siku hii pia ndiyo siku niliyoamua kutokuwa mwizi, au kuwa mtu mbaya na kadhalika. Hukusema chochote, wala hukunigombeza au kuniita pembeni kuniadhibu.
Niliupokea ujumbe wako kwa ufasaha kabisa.
Ninakushukuru sana, nilielewa ni nini mwelimishaji wa kweli anapaswa kufanya. Unakumbuka hili tukio, profesa?
Yule profesa mzee akajibu, 'Ndio, nakumbuka tukio la saa kuibwa, ambayo niliitafuta mfukoni mwa kila mwanafunzi. Sikukukumbuka wewe, kwasababu mimi pia nilifumba macho yangu wakati nilipokuwa nawasachi.
Jambo muhimu kutambua unapofundisha:
Kama ili kumsahihisha ama kumrekebisha mtu unalazimika kumdhalilisha; basi hujui kufundisha."
Asante kwa kusoma 🙏🙏🙏