Ili kuondoa tozo Serikali ifanye yafuatayo

Ukichukua Kodi kutoka kwa wanyonge Yaani wakulima na Wafugaji alafu uende kununulia vieti 8 . yaani utakuwa unapunguza siku zako za kuishi huwezi piga miaka 2 utrest in peace.Machozi ya mnyonge ni mabaya saaana.
 
Kongole Mkuu

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"!
Asante mkuu kwa pongezi.

Ni matamanio ya kila mpenda haki kuona rasimu ya Warioba ikibarikiwa na kuwa katiba. Lkn amini, aminii nakuambia hili halitatokea mpk TUCHAPANE kwanza.
 
Yafuatayo ni mapendekezo yangu yatayobana matumizi na/ama kuibua/kuongeza makusanyo.

1. Wabunge walipwe sh 45,000/= kwa siku badala ya Tsh 300,000/= kama sitting allowance. Hivyo serikali itaokoa Tsh 255,000/= × 395 (idadi ya wabunge ) kwa siku sawa na TSh 100,725,000/=kwa siku.

2. Tabia ya watumishi wa umma kifanyia semina kwenye mahoteli ife. Wafanyie kwenye majengo ya serikali kama vile mabwalo ya shule, mdarasa, ofisi za umma na kumbi za mikutano za majengo yao.

3. Semina zinazomtaka mtumishi kusafiri zikome badala yake zifanyike kwa teknonolojia. Mfano ZOOM, Skipe, Space, n.k

4. Kodi ya mifugo
(a) Ng'ombe mmoja alipiweTsh 12,000 kwa mwaka (1000 kwa mwezi).

(b) Mbuzi, kondoo, punda na mbwa kila mmoja alipiwe Tsh 6,000/= kwa mwaka (Tsh 500 kwa mwezi)

(c) Ndege (kuku, bata, njiwa) kila mmoja alipiwe Tsh 2,400/= kwa mwaka. Sawa na TSh 200/= kwa mwezi

5. Mashamba. Kila mkulima alipie Tsh 5000 kwa kila ekari anayolima kwa mwaka. Hapa kwa. Msaada wa maafisa ugani ambao wamepewa pikipiki inawezekana.

6. Sanaa. Kila single ya muziki (bongo flava, gospel, kaswida,) ilipiwe Tsh 100,000/ na kila part ya movie ilipiwe Tsh 50,000/=. Cosota na Basata wasaidie hapa.

7. Football. Wachezaji walipie 8% (indigenous) na 12% (foreigners) ya mapato yao kama kodi.

KARIBUNI kwa mawazo zaidi ama maboresho
Nenda ofisini kwa Mwigulu umweleze haya
 
Nenda ofisini kwa Mwigulu umweleze haya
Chawa wake watanitoa nduki mkuu. Tatizo la viongozi wa Afrika wanadhani ukishakuwa na cheo basi unapata na akili kubwa. Wanasahau kuwa cheo hakibadilishi akili.
 
Hayo yote yanawezekana endapo sisi raia wakawaida tukiamka achana na hawa wanaojiita wanasiasa wanajali koo zao tu wakati sisi tunaumia kila uchwao. Inapaswa tuamke muda umefika sasa, sio kila siku tunalalamika tu. Kila jambo lina mwisho wake, hao kenge mwisho wao umefika. Tudai katiba mpya kwa nguvu zote ikibidi tuwapelekee moto wasitake kutuzoea kabisa.
 
Yafuatayo ni mapendekezo yangu yatayobana matumizi na/ama kuibua/kuongeza makusanyo.

1. Wabunge walipwe sh 45,000/= kwa siku badala ya Tsh 300,000/= kama sitting allowance. Hivyo serikali itaokoa Tsh 255,000/= × 395 (idadi ya wabunge ) kwa siku sawa na TSh 100,725,000/=kwa siku.

2. Tabia ya watumishi wa umma kifanyia semina kwenye mahoteli ife. Wafanyie kwenye majengo ya serikali kama vile mabwalo ya shule, mdarasa, ofisi za umma na kumbi za mikutano za majengo yao.

3. Semina zinazomtaka mtumishi kusafiri zikome badala yake zifanyike kwa teknonolojia. Mfano ZOOM, Skipe, Space, n.k

4. Kodi ya mifugo
(a) Ng'ombe mmoja alipiweTsh 12,000 kwa mwaka (1000 kwa mwezi).

(b) Mbuzi, kondoo, punda na mbwa kila mmoja alipiwe Tsh 6,000/= kwa mwaka (Tsh 500 kwa mwezi)

(c) Ndege (kuku, bata, njiwa) kila mmoja alipiwe Tsh 2,400/= kwa mwaka. Sawa na TSh 200/= kwa mwezi

5. Mashamba. Kila mkulima alipie Tsh 5000 kwa kila ekari anayolima kwa mwaka. Hapa kwa. Msaada wa maafisa ugani ambao wamepewa pikipiki inawezekana.

6. Sanaa. Kila single ya muziki (bongo flava, gospel, kaswida,) ilipiwe Tsh 100,000/ na kila part ya movie ilipiwe Tsh 50,000/=. Cosota na Basata wasaidie hapa.

7. Football. Wachezaji walipie 8% (indigenous) na 12% (foreigners) ya mapato yao kama kodi.

KARIBUNI kwa mawazo zaidi ama maboresho
Naunga hoja kwa 100%
 
Back
Top Bottom