Ili kuongeza wigo wa Kodi, kila duka na, au biashara za mitaani, wanapopewa leseni, lazima wawe na lipa namba

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Unapodai maendeleo, jiulize kama unalipa Kodi, nashauri Kila biashara ambayo haitumii EFD receipt, Sasa zilazimishwe kuwa na LIPA NAMBA.

Mfanyabiashara, kama anafanya biashara Kila siku, hajatoa taarifa kwa mamlaka kwamba ameifunga, angalau kwa wiki au mwezi aonekane kuitumia, na namba hiyo iwe inakata Kodi moja kwa moja kimtandao na kuiwasilisha TRA.

Hii inaweza kupunguza kukimbizana mitaani,kupanua wigo wa Kodi, na Kila mtu anapodai maendeleo, kwanza aonekane amewajibika kulipa Kodi.

Haina haja ya kununua device mpya, ni simu hiyohiyo ya mmiliki wa biashara na laini ya/za simu alizowasilisha kwa mamlaka na LIPA NAMBA yake, na kama inaonekana LIPA NAMBA haitumiki, basi mamlaka, kimfumo, Ione, na waweze kumfikia hata kimitego
 
... itaboresha vipi tofauti na efd?
Itaongeza WiGo wa kukusanya kodi na kuepusha vurugu za kukimbizana na TRA kisha kuondoa nafasi ya rushwa. Kimsingi hii itakuwa inatupeleka kuwa Taifa linalotumia paperless and coinless Money. Hence, kupunguza athari za climate change!!!
 
Huucni utaahira, kwahiyo mtu ana pesa yake Cash ila ashindwe kulipia bidhaa kisa hana pesa kwenye simu?
 
Naona ili kuepuka ukwepaji kodi kila mfanyabiashara aingizwe VAT, na iwe % ndogo wala sio 18 ya sasa, kwa sasa mtu anayelazimika kudai rist ni yule aliyeko vat ambaye hana vat hana habari na mambo ya rist, au yeyote yule anayetaka kufanya biashara na serikali lazima awe na vat, kuliko ilivyo sasa mwenye vat na asiye na vat wote mnakubalika serikakini.
 
Wakishazikusanya waende wafanya vitu kama chawa wa mama na kununua ma vietee au sio.
 
Huucni utaahira, kwahiyo mtu ana pesa yake Cash ila ashindwe kulipia bidhaa kisa hana pesa kwenye simu?
Mwenye duka/biashara, ambayo haina masharti ya EFD anawekewa minimum number ya transaction kwa muda fulani, Vyote viende kwa pamoja, mwanzo mgumu hasa kwa wezi na wakwepa Kodi kama wewe
 
Kwahoyo unataka kumuadhibu mtu kisa wateja wake hawana pesa kwenye simu bali wanakuja na cash? Umerogwa wewe
 
Naona ili kuepuka ukwepaji kodi kila mfanyabiashara aingizwe VAT, na iwe % ndogo wala sio 18 ya sasa, kwa sasa mtu anayelazimika kudai rist ni yule aliyeko vat ambaye hana vat hana habari na mambo ya rist, au yeyote yule anayetaka kufanya biashara na serikali lazima awe na vat, kuliko ilivyo sasa mwenye vat na asiye na vat wote mnakubalika serikakini.
 
Jibu kwa hoja, kuelewa bila hoja? Kwahiyo utamuadhibu mtu kisa wateja wake hawana pesa kwenye simu?
Mfanyabiashara ni wakala wa TRA wa kukusanya mapato, haadhibiwi, anatimiza wajibu
 
Back
Top Bottom