Ili kuongeza wigo wa Kodi, kila duka na, au biashara za mitaani, wanapopewa leseni, lazima wawe na lipa namba

Ili kuongeza wigo wa Kodi, kila duka na, au biashara za mitaani, wanapopewa leseni, lazima wawe na lipa namba

Wewe uliyeleta hoja ndio utetee hoja yako.., otherwise haina mashiko. Au laa BOT waache kuchapisha pesa.
Tuko katika era ya digital money, paper money itakuwepo, ila digital currency ndio Dunia ijayo
 
Naona ili kuepuka ukwepaji kodi kila mfanyabiashara aingizwe VAT, na iwe % ndogo wala sio 18 ya sasa, kwa sasa mtu anayelazimika kudai rist ni yule aliyeko vat ambaye hana vat hana habari na mambo ya rist, au yeyote yule anayetaka kufanya biashara na serikali lazima awe na vat, kuliko ilivyo sasa mwenye vat na asiye na vat wote mnakubalika serikakini.
Naunga Mkono hoja
 
Itaongeza WiGo wa kukusanya kodi na kuepusha vurugu za kukimbizana na TRA kisha kuondoa nafasi ya rushwa. Kimsingi hii itakuwa inatupeleka kuwa Taifa linalotumia paperless and coinless Money. Hence, kupunguza athari za climate change!!!
Kuna mtu ame-like hiki ulichoandika [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Unapodai maendeleo, jiulize kama unalipa Kodi, nashauri Kila biashara ambayo haitumii EFD receipt, Sasa zilazimishwe kuwa na LIPA NAMBA.

Mfanyabiashara, kama anafanya biashara Kila siku, hajatoa taarifa kwa mamlaka kwamba ameifunga, angalau kwa wiki au mwezi aonekane kuitumia, na namba hiyo iwe inakata Kodi moja kwa moja kimtandao na kuiwasilisha TRA.

Hii inaweza kupunguza kukimbizana mitaani,kupanua wigo wa Kodi, na Kila mtu anapodai maendeleo, kwanza aonekane amewajibika kulipa Kodi.

Haina haja ya kununua device mpya, ni simu hiyohiyo ya mmiliki wa biashara na laini ya/za simu alizowasilisha kwa mamlaka na LIPA NAMBA yake, na kama inaonekana LIPA NAMBA haitumiki, basi mamlaka, kimfumo, Ione, na waweze kumfikia hata kimitego
Bila shaka wewe ni muajiriwa
 
Tatizo mkisha ajiliwa mnaona mmemaliza maisha, jiajiri ndo utajua kwa nn machinga hawataki kuhama mjini.
 
Ni idea nzuri lakini inahitaji biashara zisiwe za mfumo wa taslim jambo ambalo haliwezekani kwa sasa bado hatujafika huko. Labda miaka mingi mbeleni.

Dawa kwa sasa ni udhibiti wa bidhaa zilizo tayari kuingia sokoni(Import na zilizopo viwandani) kabla hazijaingia sokoni.

Badala ya kuangaika na mauzo serikali iwe na mfumo unaotrack manunuzi tu. Wao wasideal na mambo ya hujatoa risiti, Wahakikishe wana taarifa za manunuzi ya bidhaa mpya zilizoagizwa nje au kuzalishwa nchini. Hakuna mfanyabiashara anayenunua bidhaa ambayo haiuzi.

SAJILI BIDHAA MPYA ZOTE, ZIKITOKA JUA ZIMEENDA KWA MFANYABIASHARA YUPI NA KWA KIASI GANI BAAASI.

KAMA HUJAUZA KWANINI UNANUNUA?
 
Umekurupuka!

Kwahyo sisi watanzania hawahawa tutalazimika kuwa na pesa kwenye sim ndyo tununue huduma? Mtanzania gani anapenda usumbufu huo?

Kama inashindikana kwenye EFD machines basi watanzania tutaendelea kulalamikia TRA wananyanyasa wafanyabiashara kila siku bila kujua wafanyabiashara wenyewe ndyo chanzo cha yote wanayofanyiwa na maafisa wa TRA
 
Sio kwamba watu hawataki ila pesa kila siku watu wanaiba hiyo nguvu ya kulipa kodi inatoka wapi.
 
Aende kwa wakala aweke hela kwenye line yake. Kisha Arudi alipe kwa Lipa namba.
Sasa kwanini BOT ichapishe pesa isiyoweza kutumika? Ukizingatia kuchapisha pesa ni gharama kubwa sana? Na akalipa kwa cash kisha akapewa risiti yake.., utamfanya nini? Yaani uta-enforce vipi hilo agizo la lipa namba?
 
Back
Top Bottom