Sipo na Yanga kwenye hili sakata ila watu mnasahau hizi timu mbili zina nguvu kuliko chama chochote cha siasa.
Yanga au Simba ikiamua waziwazi kumkataa kiongozi wa kisiasa na ikakaza kweli kweli, huyo kiongozi lazima aanguke.
Hivi vilabu viwili vinaonekana dhaifu mbele ya wanasiasa kwa sababu viongozi wake wamepachikwa na wanasiasa kwa hiyo lazima wafuate masharti, vigezo na mashinikizo ya kisiasa. Mambo ya kulipa fadhila kwa wanasiasa yamewapotezea weledi na ujasiri wa kusimamia kwa dhati yale yaliyo na manufaa kwa vilabu vyao.