Ili ligi yetu iwe bora na ya kuvutia TFF na Bodi ya ligi inapaswa kushughulika na haya yafuatayo

Ili ligi yetu iwe bora na ya kuvutia TFF na Bodi ya ligi inapaswa kushughulika na haya yafuatayo

Yaani unataka ratiba ya kucheza saa 8, baadhi ya timu ifutwe, au Simba na yanga nao, wakicheza saa nane hamna shida, ratiba iendelee tu.
Ndio iwe hivyo kusiwepo na ubaguzi, ukiangalia ratiba miaka yote haijawahi kutokea hata mara moja Simba au Yanga akacheza saa nane mchana. Kibaya zaidi hali ya hewa hapa nchini maeneo mengi saa nane ni jua kali, inakuaje timu nyingine zicheze hawa wengine wasicheze kama kweli tumedhamiria kutengeneza fair competition?
 
Mkuu, hizo n malipo ya haki ya kuonyesha mechi zao, Azam ndio anayeonyesha ligi hvy kwakuwa anapata faida watu kununua vifurushi kwa ajili ya kuona mechi za team flani ndio mana akaambiwa anatakiwa kuwalipa, na Azam ndio anatoa pesa nyingi kwenye ligi kumzidi hata huyo mdhamini mkuu wa ligi NBC.

Yn kwa ufupi ni kwamba, Azam anapata faida kupitia kuonyesha hizo mechi ndio mana anawalipa, n sawa na ww unapofanya kazi unamuingizia faida Boss wako na yeye anakulipa sehemu ya faida uliyomuingizia ww.
Hawakuandika kuwa ni malipo ya kununua haki, bali ni udhamaini unaoendana na wao kupata haki hizo. Ni kama ambavyo SportPesa anaidhamini yanga na kupitia udhamini huo anaoata haki ya jina lake kuandikwa kifuani mwa jezi ya Yanga.
 
Hawakuandika kuwa ni malipo ya kununua haki, bali ni udhamaini unaoendana na wao kupata haki hizo
😂 Ww mwnyw Umeelewa ulichokiandika hapa 😂
Ni kama ambavyo SportPesa anaidhamini yanga na kupitia udhamini huo anaoata haki ya jina lake kuandikwa kifuani mwa jezi ya Yanga.
Haya ni wap nembo ya Azam umeiona kwenye jezi za timu?
 
Mkuu, hizo n malipo ya haki ya kuonyesha mechi zao, Azam ndio anayeonyesha ligi hvy kwakuwa anapata faida watu kununua vifurushi kwa ajili ya kuona mechi za team flani ndio mana akaambiwa anatakiwa kuwalipa, na Azam ndio anatoa pesa nyingi kwenye ligi kumzidi hata huyo mdhamini mkuu wa ligi NBC.

Yn kwa ufupi ni kwamba, Azam anapata faida kupitia kuonyesha hizo mechi ndio mana anawalipa, n sawa na ww unapofanya kazi unamuingizia faida Boss wako na yeye anakulipa sehemu ya faida uliyomuingizia ww.
Kwa hio mdhamini hatakiwi kupata faida? kweli Rage aliona mbali
 
😂 Ww mwnyw Umeelewa ulichokiandika hapa 😂

Haya ni wap nembo ya Azam umeiona kwenye jezi za timu?
Kuna title sponsor na co-sponsor NBC ni title sponsor ndio maana ana kaa kwenye jezi kwa akili hizi Mangungu yupo sahihi
 
Naaam!! kila ligi msimu inapoanza na kuisha lazima kuwe na malalamiko ya kuonewa haswa kwa hizi timu za kariakoo (Simba na Yanga) ni muda sasa wa Tff na Bodi ya ligi kushughulika na hizi lawama au lawama na makelele yanayojitokeza kila msimu unapoisha

Tff na Bodi ya ligi ishughulike na haya yafuatayo ilikutokomeza ama kupunguza lawama kutoka kwa wapenzi wa mpira katika ligi yetu ya NBCPL

(1) uchunguzi wa hali ya juu kwa timu zinazotoa rushwa kwa marefa, hiki kimekua ni kilio cha kila msimu unapoisha, mpira ni mchezo wa wazi wala hauchezwi ndani mashabiki huwa wanaona na wanajua kabisa hili ni kosa ama siyo kosa na refa anastahili kutoa kadi au kupuliza filimbi.

kuna baadhi ya timu zinalalamikiwa sana kuwa zinahonga marefa ili wapate ushindi na pointi tatu muhimu katika mchezo na kweli ukiangalia refa anavyochezea unaona kabisa kuna namna imetumika timu kupata point tatu muhimu, Tff na Bodi ya ligi inapaswa kubuni mbinu za kuwakamata marefa wanaokula rushwa na kutoa adhabu kali sana kwa wahsika

(2) tuzo zitolewe kwa wakati , hii inafanya ligi ichangamke sana tena mno lakini kilichofanyika msimu uliopita ni madudu matupu na aibu kwa Tff na bodi ya ligi yaani msimu kuisha na tuzo kutolewa msimu mwingine unaoanza kwa kweli imefanya ligi yetu kukosa mvuto kabisa, Tff wanapaswa kutoa ligi kwa wakati.

(3)Viwanja vikaguliwe kwa wakati na siyo mpaka Simba na Yanga wacheze ndiyo vionekane ni vibovu, ligi inafatiliwa sana hii ni aibu kubwa viwanja havikaguliwi haswa viwanja vya mikoani mpaka Simba na Yanga wakicheza na mashabiki kuanza kulalamika ndipo Tff na Bodi ya ligi hujitokeza na kufungia uwanja, kwa mantiki hiyo watendandaji hawafanyi kazi mpaka washituliwe na kelele za mashabiki .
Tff iliangalie sana hili suala la uakaguzi wa viwanja kwanni viwanja bora huleta hamasa katika ukuaji wa ligi

(4) Marefa walipwe stahiki zao na waboreshewe posho , marefa hawana pa kulalamika kutoka kwenye vyanzo vyangu vya ndani marefa hawapewi posho zao kwa wakati na muda mwingine wanadhurumika kabisa , sasa kwa hali kama hii lazima refa auze mechi lakini akipewa stahiki zake kwa wakati hii itapunguza lawama za refa kuuza mechi, Tff na bodi ya ligi waangalie hili suala.

(5) Zitolewe semina na elimu ya kutosha kwa marefa , hili ni jambo la ,muhimu sana kuna makosa madogo madogo hufanywa na marefa ya kushindwa kutafsiri sheria za mpira na kufanya timu pinzani kujipatia pointi tatu muhimu lakini kama Tff na bodi ya ligi itaandaa mkakati maalumu wa kuchukua marefa wanaohudhuria training na semina za kila muda wanapohitajika itafanya ligi yetu ikue.

(6) iboreshwe sheria inayohusu imani za kishirikina kama ipo na kama haipo itungwe lakini iwe na uthibitisho kwa timu itakayotuhumiwa, kuruka ukuta, kutoa taulo kuchimba katikati ya uwanja n.k Tff na Bodi ya ligi imekua ikipiga faini kwa timu zitakazoonesha viashiria vya imani za kishirikina, ombi langu kama hii sheria ipo basi iboreshwe maana limekua ni suala la kujirudirudia.

Endapo haya niliyoyaorodhesha yatapuuzwa basi tusitegemee kuona ligi yetu ikikua bali itaendelea kudumaa kwani kwa mujibu wa utafiti sasa tunashika nafasi ya sita kwa ligi bora africa, kwa mantiki hiyo tumepolomoka kutoka nafsi ya tano mpaka nafasi ya sita.
Kwenye viwanja ndo muhimu sana ni kiwa na maana pitch ya kiwanja vyote vitkavyo kuwa vnatumiwa vwe na hadhi ya uwanja wa taifa tutaenjoy mpira kwa sisi watazamaji na hao wachezaj pia
 
Kwenye viwanja ndo muhimu sana ni kiwa na maana pitch ya kiwanja vyote vitkavyo kuwa vnatumiwa vwe na hadhi ya uwanja wa taifa tutaenjoy mpira kwa sisi watazamaji na hao wachezaj pia
Well said mkuu
 
Back
Top Bottom