Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Ili Magufuli aibadilishe Tanzania, ni lazima awe Rais kwa zaidi ya miaka kumi

Kwa hali ilivyo wazo hilo ni baya mleta mada, afadhali kama jamaa angekuwa Democrat , lakini kwa haya kuamka asubuhi katamka hivi na vile hapana jamani.

Vinginevyo hayo mawazo yanayochipuka yakipaliliwa na wabunge wetu hawa wa NDIYOOOOOOOO, basi tutaishi kama kuku wa kizungu
Unataka asitamke?
 
Usi ishie kwenye manenu tuu, hakuna faida ya moja kwa moja na hao wafanyakazi hewa wako karibu kila nchi huwa hawaishi kwa kuwa bureaucracy ina wa akifelitu wajanja wengi.
Wabongo acheni kujidanganya katika histria ya Dunia vitu anavo vifanya magufuli havija wahi kuleta maendeleo mcheki mwenzie buhari mbona ana feli!!?
Mi siwez kumchukia Rais wa nchi maana najua akifeli yeye nchi nzima ita feli so usiniseme kwa mameno nipe ushahidi in reak life kiongozi gani aliwahi fanya kama Magufuli halafu aka fanikisha maendeleo makubwa ya ki uchumi.
Usikariri
 
Kipindi chake cha pili asimamie Kura ya maoni ya katiba mpya atapata kile kipindi cha miaka ya mpito
 
Leo nyang'anya wenyeviti wote mihuri, kesho nunua Ndege 6 keshokutwa sitaki siasa nchini kwangu, wape wanafunzi wote mkopo siku inayofuata ni wale tu tunaowataka, mtondogoo teua fukuza etc . Hata kama yote yanefanyika kwa nia njema lakini si uongozi.
Uongozi ukoje
 
hatuwezi kuendelea kwa kunyamazisha mawazo ya watu wengine na kumtazama mtu mmoja. kila mtu ana mchango wake katika maendeleo hivo kila mtu apewe nafasi.
Uko sahihi kabisa. Magufuli is not omnipotent.
Magufuli is more of a" single decision maker type of person "
 
Mpaka sasa kafeli. Urais sio kama baba jinsi anavyoongoza familia yake.
Urais ni taasisi inayoshirikiana kikamilifu na taasisi nyingine kama Bunge na Mahakama tukeleza katiba ya nchi.
JPM angeweza kulifanya bunge kuwa huru na yeye kutekeleza yale yanatopendekezwa bungeni basi tungekua mbali.
Tatizo lake anataka kila kitu afanye yeye,kodi za ajabu zilizoanzishwa ndio zimekausha bandari. Wakati anajua bandari inachangia zaidi ya 50% ya pato la nchi. Kwenye utalii nako kavuruga,kaweka kodi zisizokua na nyuma wala mbele. Kaachana na kilimo anakimbilia viwanda,hivi kuna nchi imeendelea kiviwanda bila ya kuwekeza kwanza kwenye kilimo? Kama ipo naomba jibu.

Uyu kafeli na hawezi kutufikisha kokote zaidi ya kuharibu nchi tu.
 
- Shirikisha mihimili mingine na siyo kuziamulia
- pili angalau onya hata mara moja
- Wapinzani wapo kikatiba wasibanwe wapewe nafasi wafanye siasa zao bila kunyanyaswa na ma RPC/OCD.
Unajuaje kama hashirikishi mhimili mingine? Mhimili mitatu tu.
 
Huwa najitahidi kuongea ukweli, japo mara nyingine watu wananikasirikia. Nakumbuka mapema sana, kabla hata jina Bulldozer halijajulikana kitaifa na kimataifa, nilisema humu JF Magufuli ni mchapa kazi sana, lakini labda ningependelea awe na nafasi ya Waziri Mkuu badala ya Raisi, kwa sababu anafanya kazi kama bulldozer, nikimaanisha alihitaji mtu ambaye sio "impulsive" kumwongoza, kama ilivyokuwa kwa Nyerere na Sokoine. Baadaye nilishangaa kuona jina Bulldozer limemnasa Magufuli.

Sasa nitawaambia jambo jingine. Tanzania tumegawanyika kwa sasa, pro na against Magufuli. Huko nyuma nilisema pia Tanzania ilikuwa imefikia pabaya sana na hivyo labda ilikuwa vema na wakati muafaka kupata kiongozi wa namna ya Magufuli, angalau kwa miaka kumi. Lakini sasa najua kwamba miaka kumi haitatosha. Najua hii ni kauli ya kuleta hasira, lakini ndio ukweli wenyewe.

Hakuna Raisi duniani anaweza kuibadilisha nchi toka alipoikuta Magufuli kwa kipindi cha miaka kumi tu. Na hatari ya miaka kumi ni kwamba raisi atakayefuata anaweza kuharibu mazuri yote yaliyofanywa, kwa sababu yale mazuri yanakuwa hayajaota mizizi sawasawa (established sustainable systems). Na hiyo ni ukweli wa-kishule (academic truth) kwamba ili nchi iendelee inahitaji mipango ya muda mrefu isimamiwe na mtu ambaye yuko committed kuisimamia (committed leadership to implement strategic national development plans). Hakuna mpango wa muda mrefu wa kuiendeleza nchi utakaotekelezwa chini ya miaka kumi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Ukiangalia historia ya mataifa yaliyoendelea haraka chini ya viongozi wao maarufu, utaona kwamba mafanikio ya nchi hizo hayakuletwa na viongozi waliobadilisha hizo nchi katika kipindi cha miaka kumi tu. Mifano mizuri ni Singapore, Malaysia na hata Rwanda. Singapore kwa mfano, kuna wakati fulani kiongozi wao alilalamikiwa, na hata kukasirikiwa kwa maamuzi magumu aliyofanya, lakini angalia alipoifikisha Singapore, toka taifa masikini sana. Ilimchukua miaka zaidi ya kumi kufanikisha hilo. Malaysia ni hivyo hivyo na Rwanda ndiko wanakoelekea.

Huwezi kuilinganisha Tanzania na nchi kama Marekani, ambao tayari wana "established systems" ambazo hazihitaji raisi mzuri kukaa madarakani zaidi ya miaka nane. Na mie ni wa kwanza kukubali kwamba ukiweka utarataibu wa kutokuwa na kikomo cha uraisi kabla hujampata Raisi mzalendo kama Nyerere au Magufuli, hatari ni kwamba unaweza kumpa nafasi raisi fisadi au mbovu akaharibu sana nchi. Mifano ya nchi za namna hiyo ipo mingi imetuzunguka.

Lakini sasa tunajua Magufuli ni mtu wa namna gani. Yapo ambayo sikubaliani na Raisi Magufuli, na hata kumkasirikia mara nyingine. Lakini ni mengi zaidi ninayokubaliana naye, hasa katika kukabiliana na ufisadi na kuleta nidhamu ya uwajibikaji. Watanzania tulilala sana, tulifikia uozo mbya sana. Niliwahi kuwaambia kuna mke wa raisi alimfokea kiongozi wa bandari kwa kukataa kuyatoa makontainer yake bila kuyalipia kodi. Aliitwa ikulu (na mke) na akaishia kuyatoa bila kupenda.

Na ukweli unabakia, kwamba, kama kweli Tanzania tunahitaji mabadiliko ya kutumia rasilimali zetu tuwe kama Singapore au Malaysia, basi mtu kama Magufuli anahitaji kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Najua hii ni lugha Watanzania wengi, na hasa vyama vya upinzani, hawawezi kuifurahia, lakini huo ndio ukweli. Baada ya hiyo miaka labda ishirini ya Magufuli, basi tunaweza kurudi tena kwenye uraisi wa kiindi cha miaka kumi au hata nane. Tutakuwa tayari tuna "established system" huenda hata kwa kiwango cha Singapore. Kama ikibidi vyama vya upinzani kuungana na CCM kwa sasa ili kufanikisha hilo basi na iwe hivyo.
Mmeshaanza kutokwa miPOVU baada yakuhisi mtukufu uchaguzi ujao atarudi Kuvua samaki
 
Kama hujui kuna faida gani kiuchumi wanapoondolewa wafanyakazi hewa. Kwanini nisikuite hopeless hater.
Usiongozwe na Mihemko.msome tena Jamaa ana Hoja....ukiacha la watumishi Hewa kuna kipi cha maana kinafanyika Sera yetu ya Uchumi niipi au unachanganywa na Porojo zaakina Mwijage wanaotangaza Mafanikio kabla Biashara kuanza
 
Back
Top Bottom