Ili tuanze kumfunga Mwarabu, tujifunze kutegemea zaidi Wakristo tukiwa tunashindana nao

Sina cha kuongeza
 
Kama una amini hivyo,basi tengeneza team ya Kanisa,itakua inachukua kila kombe lililo mbele yake,

Ni ujinga kuingiza mambo ya dini kwenye mpira.
 
Na tukifika kombe la dunia halafu tunakutana na Uingereza...timu nzima ya wakristo tuitimue...tulete waislam watupu??
Mfano wako ni mzuri ila conclusion uliyotoa siyo sahihi. Nchi hii kuna watu ambao mzungu akiwa mbele yake anakosa kujiamini pamoja na kwamba anaweza kuwa na ujuzi au elimu nzuri tu. Hii inaweza kusababishwa na vingi lakini dini ya muhusika inaweza kuwa inachangia.

Hili kama taifa lazima tulizingatie katika mashauri yote ya nje kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa na kuwekwa mbele. Najua wenye uwezo wa kutafakari mambo kwa upana wananielewa.
 
Mleta mada ni katika wale wanaoitwa "Islamophobes".
Watanzania hampendi kabisa kushughulisha bongo zenu. Ni wapi niliposema Uislamu ni mbaya? Mimi nimejaribu kuangalia uhalisia wa haya mambo. Nasikilizaga kwa makini kauli zinazotolewaga na watu timu zetu zinapoendaga huko Uarabuni nikagundua moja ya shida tuliyonayo ni hii.

Na hata nimejaribu kutoa mfano tofauti wa Vatican kuonyesha mazingira yangekuwa ya upande mwingine, bado approach inatakiwa kuwa ile ile.
 

Hili unalo ongea ni sahihi only kwenye uongozi wa kitaifa sio Mpira
 

Uko sahihi Kwa kiasi fulani hasa mambo kama mikataba na diplomasia...lakini sio Mpira

Mimi naaamini huna chuki na waislam..lakini approach yako haiwezekaniki....
 
Acha chuki za kidini mkuu. Halafu simba hajawahi kupata ushindi uarabuni, Wape Yanga Maua yao ndio timu pekee afrika inayoweza kumpiga mwarabu huko huko Uarabuni
Simba alimtoa zamalek akiwa congo?
 
Uko sahihi Kwa kiasi fulani hasa mambo kama mikataba na diplomasia...lakini sio Mpira

Mimi naaamini huna chuki na waislam..lakini approach yako haiwezekaniki....
Tunaweza tusitumie approach hii 100% kwa maana ya kuwabagua wachezaji wa kiislamu ila kutambua hili tatizo la kisaikolojia lipo tunapocheza na Waarabu kwa baadhi ya wachezaji wetu ni hatua moja mbele. Linaweza kutatulika kwa njia nyingine hasa kwa kutumia wanasaikolojia ila ni muhimu tulitambue hili tatizo lipo kwa kiasi fulani.
 
Samahani huyo mazembe kavunja kanisa au? Mbona sasahivi dhooflhal
 

Kuna thread nyingi Sana nimeweka humu kuhusu watu weupe...na Sisi watu weusi... mentally slavery waliyo tulisha na jinsi inavyo tuumiza...

Nyerere aliwahi kusema wapo waswahili upumbavu ukisemwa Kwa kiingereza wanaona jambo la maana Sana...
 
Kuna thread nyingi Sana nimeweka humu kuhusu watu weupe...na Sisi watu weusi... mentally slavery waliyo tulisha na jinsi inavyo tuumiza...

Nyerere aliwahi kusema wapo waswahili upumbavu ukisemwa Kwa kiingereza wanaona jambo la maana Sana...
Ni tatizo kubwa. Tunapojifunza au kufundishwa hizi tamaduni za nje tunapoteza kabisa kujiamini. Mara nyingi tunapocheza na Mwarabu ikiwemo jana ninachokionaga ni Mwarabu anaipambania sana PRIDE au FAHARI yake. Sisi tunadhani ni ishu ya mpira tu.
 
Umeandika pumba yaani hata hueleweki[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Sa100 kwenye hotuba yake moja aliongelea hili
 
Eti Waislamu wanaheshimu sana Waarabu hivyo hawawezi kuwafunga.
Jinga sana kwani umeambiwa waislamu wanaabudu waarabu!
 
Mkuu hongera sana kufafanua jambo muhimu kwa mifano hai kabisa.
Nakupa mfano mwingine mzuri.
Hapa Zanzibar linapokuja swala la kutetea maslahi ya Zanzibar basi wanawekwa mbele watu wa upinzani, ndio wanaopiga nyundo bila huruma wala bila uoga.
Na hata kabla ya serikali yenye muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa walikuwa wakifanya kazi pamoja ikibidi dhidi ya bara.

Hili hasa ndio lililosababisha Aman Karume kutaka serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ili wapinzani ndio wajibishane na bara huku CCM wakiunga mkono na kuchekea shavuni. Matokeo yake matakwa yote ya Zanzibar yameshinda na sasa panajengwa hadi maporini na ufisadi hamna mfano duniani kwa upigaji na bado hamna tatizo la fwedha.
 
Nakuunga mkono mkuu maana Malawi yenye waislam tupu inaifunga Egypt kila siku na lakin Senegal yenye wakristo watupu inapigwa kila ikikutana na Egypt.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…