Ili ufanikiwe unahitaji kufeli

Ili ufanikiwe unahitaji kufeli

King999 said:
Shida yako ni grammar yangu au idea nlotaka ku present hapa?
"Grow up pls"
Mkuu usichukulie NEGATIVE pengine yeye alichukulia POSITIVE.

Don't take it personal.
 
Hapa kwenye kuzikimbia changamoto ndio shida ya wengi. Hivi unadhan ukizikimbia huku, kule unakoenda hakuna?

unajua tunapofeli ni kurithi na kuona tatizo na kulifanya mazoea,wengi wanafanya hili na wanaacha hivyo limekuwa kama mazoea hata pale ambapo anaona sio sawa,kwa sababu ya mazoea anaacho..utasikia mimi nilijaribu jaribu sana nikafeli hadi kufika hapa.hivyo tumeifanya kujaribu jaribu kuwa rasmi bila kuangalia madhara yake.
 
Mwanzo nilikua nikijipa tamaa sana ndio maana kila ninapofeli maumivu huwa makali sana ila sasa kila ninachofanya naeka kufeli coz nimeshafeli sana ila nakua sikati tamaa, iko day nitafika malengo

Hongera Mkuu ukijiwekea hivyo hata asilimia za ufanikiwa zinaongezeka,sababu unafanya kitu ukiwa na utulivu wa mwili na akili,hata mawimbi yanapokuja unajua jinsi ya kutuliza dhoruba kwa kuwa wewe mwenyewe umetulia. Hongera kwa kuweza kulitambua hilo.
 
Ni kweli ila tatizo kubwa lipo toka kwenye mifumo ya elimu yetu, unakuta mwanafunzi akifeli mtihani anaonekana hawezi na hana kitu kabisa .Hii inapelekea hata kwenye maisha ya upambanaji kila unapokumbana na vikwazo unajihisi hufai kabisa na huwezi endelea tena kitu ambacho siyo kweli.TUNAHITAJI KUBADILI MTAZAMO KUANZIA KWENYE ELIMU YEU.
Nawasilisha
 
Elisha Chuma,
You are totally right...
Winston Churchill : Success is not final, failure is not fatal: it is the courage to continue that counts.
 
Naona wakuu wote tuko kwenye mstari mmoja,rai ni inabidi tujitahidi kujenga fahamu za vizazi vyetu zaidi ya maneno,tunaweza kuwa sisi tumeanguka na kuona tatizo liko wapi tusirithishe pia na kwa vizazi vyetu..wanetu wawe chachu ya kujifahamu tangu wakiwa wadogo inamsaada sana kwa vizazi vyote na mafanikio ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla yataanzia hapo.

Tunapoteza nguvu kazi kubwa na taifa la kesho kwa sababu ya kuzembea kujenga ufahamu sahihi kwa wanetu na wale ambao tunapata nafasi ya kuwaathiri makuzi ama malezi yao.
 
Back
Top Bottom