Naona wakuu wote tuko kwenye mstari mmoja,rai ni inabidi tujitahidi kujenga fahamu za vizazi vyetu zaidi ya maneno,tunaweza kuwa sisi tumeanguka na kuona tatizo liko wapi tusirithishe pia na kwa vizazi vyetu..wanetu wawe chachu ya kujifahamu tangu wakiwa wadogo inamsaada sana kwa vizazi vyote na mafanikio ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla yataanzia hapo.
Tunapoteza nguvu kazi kubwa na taifa la kesho kwa sababu ya kuzembea kujenga ufahamu sahihi kwa wanetu na wale ambao tunapata nafasi ya kuwaathiri makuzi ama malezi yao.