Ili ufanye harusi au sherehe Moshi lazima ulipe Kodi za Manispaa Tsh. 230,000

inafika mahalai nchi inakuwa kama si yakwetu! hakuna kitu ambacho hulipii sasa kila kitu malipo!,kwa uchumi gani au wanatuona sisi mazwazwa sana...??!
 
Nani akalipe gharama hizo kufanya sherehe? Naenda kanisani nafungishwa ndoa narudi nyumbani kula ugali na mke wangu, imetoka hiyo
 
Hii imewalenga wale wanaopenda kufanya sherehe za kifahari za bajeti za juu. Moshi wanapenda sana kufanya sherehe hata kwa mambo madogo kama arobaini ya mtoto na mambo mengine ya kidini kama kipaimara na ubatizo
 
Kwa wasio na taarifa, tangazo hili hapa!View attachment 2997156
Mazishi nayo ni sherehe. Yanakuwa na
Mc
Muziki
Chakula
Vinywaji na
Eneo la kufanyia mazishi

Yenyewe tozo yake ikoje?

Pia swali la ufahamu:
Hawa manispaa ya Moshi wanavyotaka tozo ya chakula na vinywaji wanakuwa wameingia gharama gani? Je watakaokuwa vinywaji kwenye viosk nao wanatozwa tozo?
 
Naunga mkono hoja, naungana na mkurugenzi. Huenda mkapunguza kidogo masherehe makubwa yasiyo na maana yoyote.

Ndoa zenyewe zipo hoi kweli kweli.
 
Shida ni flat rate kungekuwa na viwango kulingana na bei ya kukodi ukumbi. Hela ndogo hiyo kwa wenyewe chupa moja ya whisky fulani. Ila kwa wengine itakuwa ada kubwa kutoa.
 
View attachment 2997156

Manispaa ya Moshi chini ya Sheria ndogo za (ada na ushuruj ya Mwaka 2019, Tangazo in Serikali Na. 148 la Tarehe 15/02/2019, imeainisha ada na tozo mbalimbali katika kuendesha sherehe kwenye kumbi na maeneo ya starehe.

Mchanganuo wa ada na tozo hizo ni kama ifuatavyo;
  • Tshs. 60,000.00, Kibali cha kufanya sherehe
  • Malipo kutoka kwa mpambaji wa sherehe Tshs. 50,000.00 Tshs. 50,000.00
  • Malipo chakula na vinywaji Tshs. 30,000.00
  • Mshercheshaji wa sherehe (MC) Tsh. 30,000
  • Mpiga picha wa sherehe Tshs. 20,000.00
  • Muziki Tshs. 20,000,00
JUMLA KUU: Tshs 230,000.00

Fedha hizi zinatakiwa kulipwa na Mwenye sherehe ndipo apatiwe kibali cha kuendesha sherehe husika. Aidha mmiliki wa Ukumbi anapaswa kuhakikisha kwamba Mwenye sherehe anakupatia nakala ya kibali kabla ya kumruhusu kutumia Ukumbi. ANGALIZO: Iwapo wakala hatakuta kibali ukumbini, sherehe itazuiwa kufanyika kuanzia muda huo.

Kwa barua hii namtambulisha kwenu ULOFAMO AUCTIONEER AND COURT BROKERS LTD, wakala atakayehusika na usimamizi wa ukiukwaji wa ada na tozo tajwa kifungu cha 3 hapo juu.
Tanzania Nationa e- Procurement system yaaani TANePS....

envelope single

Bid ID ni 693709

Financial Value Tzs 1050.000.00.00( hii inasomeka Tsh ngapi?)*
Ambako yeye anasomeka kama
Erick Clement Mphuru

Box 7859 Moshi
Phone 0673883800
Email: ulofomaauctioneer@gmail.com
 
naona sasa wazee wa kataa ndoa wanapaishwa sana mawinguni kama ndege ya raisi wa iran
 
Tanzania Nationa e- Procurement system yaaani TANePS....

envelope single

Bid ID ni 693709

Financial Value Tzs 1050.000.00.00( hii inasomeka Tsh ngapi?)*
Ambako yeye anasomeka kama
Erick Clement Mphuru

Box 7859 Moshi
Phone 0673883800
Email: ulofomaauctioneer@gmail.com
Takukuru huko Kilimanjaro, fuatilieni hii tenda.

Niwakumbushe pa kuanzia, DED alifanya send off,ya bint yake wa KAZI,kwenye ukumbi upi?

Na alipatiwa risiti ya efd mashine, kutoka kwa hao madalali?

Je risiti hiyo inasomeka muda Gani na tarehe ngapi?

Je alipa Tsh 230,000????

Nchi imekuwa ngumu sana hii!!
 
Hapo mnapigwa huyo Hofolo ndio nani? Kama kutokulipa hizo pesa kosa kwanini wasitumie asakali wa jiji
 
Kwa kweli nchi ikikosa watu makini wenye ubunifu na malengo halisi ya kusaidia nchi haya ndio matokeo yake.
Sahihi Yaani mwenye ukumbi alipe Kodi ya mapato na Bado mwenye sherehe alipe huu wizi Sasa

Mtu ana leseni ya ukumbi na anatambuliwa kuwa anafanya hiyo biashara na kazi za kumbi zinaeleweka miziki,nk ndio kazi yake Vibali hivyo vingine vya Nini Tena? Huo ni wizi na u hukuaji Pesa mara mbili Kwa biashara Ile Ile

Kazi ya leseni ya ukumbi ni Nini?
 
Ada za kijinga sana hizo ni sawa
Mwenye ukumbi ni muuza duka ansuza ukumbi mwenye sherehe mteja mnunuzi

Kwa hiyo unamwambia mteja ukitaka kwenda dukani lipa kwanza kiingilio halmashauri Cha kwenda dukani.kununua kitu unachotaka

Halmashauri Ina maana wameweka kiingilio kwenye kumbi za watu ambazo wao hawakujenga Wala kushiriki kujenga

Hizo ada ni viingilio vinavyolipwa halmashauri ili sherehe iingie ukumbi ni

Wizi mtupu
 
Sahihi Yaani mwenye ukumbi alipe Kodi ya mapato na Bado mwenye sherehe alipe huu wizi Sasa

Mtu ana leseni ya ukumbi na anatambuliwa kuwa anafanya hiyo biashara na kazi za kumbi zinaeleweka miziki,nk ndio kazi yake Vibali hivyo vingine vya Nini Tena? Huo ni wizi na u hukuaji Pesa mara mbili Kwa biashara Ile Ile

Kazi ya leseni ya ukumbi ni Nini?
 
View attachment 2997156

Manispaa ya Moshi chini ya Sheria ndogo za (ada na ushuruj ya Mwaka 2019, Tangazo in Serikali Na. 148 la Tarehe 15/02/2019, imeainisha ada na tozo mbalimbali katika kuendesha sherehe kwenye kumbi na maeneo ya starehe.

Mchanganuo wa ada na tozo hizo ni kama ifuatavyo;
  • Tshs. 60,000.00, Kibali cha kufanya sherehe
  • Malipo kutoka kwa mpambaji wa sherehe Tshs. 50,000.00 Tshs. 50,000.00
  • Malipo chakula na vinywaji Tshs. 30,000.00
  • Mshercheshaji wa sherehe (MC) Tsh. 30,000
  • Mpiga picha wa sherehe Tshs. 20,000.00
  • Muziki Tshs. 20,000,00
JUMLA KUU: Tshs 230,000.00

Fedha hizi zinatakiwa kulipwa na Mwenye sherehe ndipo apatiwe kibali cha kuendesha sherehe husika. Aidha mmiliki wa Ukumbi anapaswa kuhakikisha kwamba Mwenye sherehe anakupatia nakala ya kibali kabla ya kumruhusu kutumia Ukumbi. ANGALIZO: Iwapo wakala hatakuta kibali ukumbini, sherehe itazuiwa kufanyika kuanzia muda huo.

Kwa barua hii namtambulisha kwenu ULOFAMO AUCTIONEER AND COURT BROKERS LTD, wakala atakayehusika na usimamizi wa ukiukwaji wa ada na tozo tajwa kifungu cha 3 hapo juu.
nafanyia home kwangu tu, simple.
 
Kwani wanaume mkigoma kuoa mtawekewa kodi ya ubachela? Gomeni muwaachie manispaa hao wanawake.
 
Back
Top Bottom