Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Nimeshuhudia patashika ya migambo na wafanyabiashara kata ya Buyuni wakiwakamata wafanyabiashara mbalimbali na kuwapeleka ofisi ya mtendaji kata Buyuni iliyopo Chanika kwa kosa la kufanya biashara bila cheti cha afya na cha COVID-19.
Pamoja na mambo mengine msako huu umekuwa mkali kiasi kwamba watu wamefunga ofisi na kurudi majumbani, wametakiwa kulipa faini ya Tsh 500,000/= na wengine laki tatu mpaka 50000 kulingana na biashara ya mhusika.
Watu wa saloon na migahawa, maduka na mafundi viatu wamesombwa na kupelekwa ofisi ya kata. Mpaka naandika hapa bado kuna wafanyabiashara wanashikiliwa hapo Buyuni kata.
Tunaomba ofisi ya mbunge au mtendaji na mamlaka husika zitoe ufafanuzi juu ya ujinga huu unaofanywa kwa maelekezo ya bwana afya na mtendaji wa kata. Tafuteni vyanzo vya mapato acheni kusumbua mama zetu kwa mambo ya kijinga.