Uchaguzi 2020 Ili uweze kuwa kiongozi wa Taifa lolote hapa Duniani ni lazima uwe na uungwaji mkono na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa husika

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Uongozi ni pamoja na wewe kuungwa mkono na kamati husika niliyoitaja hapo juu tofauti na hapo ni kupoteza muda tu.

Kamati hii inawajumuisha wafuatao:

Rais aliyepo madarakani japokuwa si muhimu akuunge.

Mkuu wa majeshi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Mkuu wa Magereza.

Mkuu wa Uhamiaji.

Kamishna wa kudhibiti madawa ya kulevya.

...na Marais wastaafu japokuwa ni waalikwa.

Ndugu yangu bila uungwaji wa mkono na hao jamaa hapo juu wala huna haja ya kupoteza muda.

Kwa gharama "yeyote" na kwa namna "yeyote" ili uweze kufanikiwa kuwa mkuu wa Nchi lazima baadhi ya hao wawe upande wako na kama ni vinginevyo bora Nchi waichukie wao kuliko kikaragosi fulani..
 
Sio kamati hata kambi moja ya kijeshi inaweza kubadili kila kitu au wananchi.
 
Afrika ndivyo tulivyo ,mmesha yaunganisha Majeshi na wana Siasa na kutengeneza Mfumo kandmaizi baaasi ni kubaki Madarakani tu na kutumbua Maisha.Uchaguzi ni kiini Macho tu kwenye Nchi washirika ,nyuma ya hapo ni Uchafuzi tu wa Kodi za Wananchi.
 
John Okelo alikubalina na hao unaosema?
Kule Mali mwaka huu kwani walikubaliana na hao uliotaja.
 
Huyu mpuuzi inaonekana anajua wameishia na pumzi ndio maana kaja na huu uharo!
Amesahau kuwa kura za wengi ndio zinamuweka kiongozi madarakani, na sio hao aliwataja! wakikuweka hao ukue umepora madaraka au ni mapinduzi ya kijeshi na ambayo hayana nafasi tena ktk dunia ya leo.
 
Sasa ni mgombea gani anaungwa mkono na hao?
 
Kwamba Adama Baro alivyomuangua Yahya Jammeih wa Gambia alikuwa anaungwa mkono na hiyo list yako sio ?
 
Mkuu wazungumza tu, majukum ya waheshimiwa ulio wataja ni zaidi Kama uyajuavyo ,hao wanakula viapo vya nchi yao sio kiapo Cha chama chochote ,ni bahati mbaya Sana mnawavuruga, na mungu awapambanie natamani siku moja wawe vyombo huru kwa manufaa ya taifa hili,
Wanauza nyanya, wanatembeza sum za panya ,ni matingo,ni bodaboda, ni walim,ni madactari, yote kwa ajili ya taifa lao, so mungu kwa nguvu yako ya ajabu ukawapiganie,Asante mungu kwa kibali ichi ,nami kwako najua sio chochote
 
Mmeanza kupagawa siyo? Hao makumi ya viongozi walioondolewa na wananchi sehmu nyingine duniani huku vyombo vya dola vikiwa vinaongozwa na ndugu zao walishindwa nini hasa? Wenye nchi ni wananchi na wakiamua hakuna wa kusema jingine. Watu wamechoka kuongozwa na mtu anayefanya maamuzi kama kichaa. Hata hivyo vyombo vya dola vyenyewe wengi kabisa hawampendi. Alijidanganyaka kuwa anapendwa baada ya kuzuia mawazo ya upande wa pili na sasa anaona hali halisi ilivyo. Kuharisha hakufungi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…