Ilichofanya TAMISEMI ndio demokrasia ya kweli kwa sasa, Shukran Ummi Mwalimu na mama Samia

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Dah!! Haya mambo tumeyazoea kuona kwenye nchi kama Marekani, Uingereza n.k

Kitendo alichofanya huyu dogo Josephat kama ungekuwa utawala wa mwendazake sasa ungekuta wazazi wanamtafuta huyu kijana.
Kwanza angepotezwa kwa kuidhalilisha serikali bila kusikilizwa hoja zake,angepigwa na kuvunjwa miguu ili iwe funzo kwa madogo wengine.

Hongereni TAMISEMI kwa busara mliyotumia,sasa ni wakati wa demokrasia chini ya Samia Suluhu hakuna ubabe tena,hakuna kejeli wala kutosikizwa kama tulivyozoea.

Mods niwekeeni ule uzi wa TAMISEMI YAMEJIBU MWANAFUNZI ALIEVAA MABANGO ili watu waelewe hoja yangu
 
Huyo dogo nimemkubali sana
 
Wamejibu kwa busara sana,heb waza dogo kama huyo anajibiwa na serikali!!! Ni ajabu sana
Mkuu Kwanini unaona km ni ajabu???. Kwani Serikali ipo kwaajili ya akina nani?. Kweli mfumo kandamizi ni mbaya sana yaani haki Yako unaona km Surprise?!!.
 
Mkuu Kwanini unaona km ni ajabu???. Kwani Serikali ipo kwaajili ya akina nani?. Kweli mfumo kandamizi ni mbaya sana yaani haki Yako unaona km Surprise?!!.
Mkuu ni haki yangu lakini geresha tu,ww uliwahi kupata haki kabisa? Japo ni haki yangu lakini ni ajabu sababu sijazoea
 
Mkuu ni haki yangu lakini geresha tu,ww uliwahi kupata haki kabisa? Japo ni haki yangu lakini ni ajabu sababu sijazoea
Upo sahihi Mkuu, kwasababu tulishawekwa kwenye mifuko ya watu.In short tushazoea kugandamizwa.
 
Mimi bado najiuliza, dogo hakuona kama kachaguliwa Ualimu!

Badala yake akaona kachaguliwa ECA...
 
Mimi bado najiuliza, dogo hakuona kama kachaguliwa Ualimu!

Badala yake akaona kachaguliwa ECA...
Mm ukiachana na hoja ya dogo,mm nashamgaa vitendo tu.
 
Nyie sifieni tu nyuma ya pazia huyo mtoto ana majanga mengi atakayokumbana nayo
 
Hakika, hakuna nguvu iliyotumika bali maeleweshano...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…