6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waungwana,
Kwa wale wakongwe wenzang wa enzi zile za miaka ya 80s kurudi nyuma, na hasa wazawa halisi wa mkoa wa Dar es salaam nafikiri mnamjua au kumkumbuka mzee fulani kwa jina mzee Majambo aliekuwa anazunguka mkoa wote wa Dar es salaam na marimba yake akiimba nyimbo zake za kitamaduni ktk lugha yake ya kigogo, wakati mungine akionesha kuguswa na kutingisha tingisha kichwa kuonesha anaguswa na kile akiimbacho.
Mzee yule alikuwa haoni, lakin alikuwa na uwezo mkubwa wa kuuzunguka mji, kuimba na kupiga marimba yake kwa kutumia mikono yake na muda mungine miguu yake. Sasa yule mzee alipoteaje poteaje?
Mbona alifaa kupewa heshima yake na taifa, na ikiwezekana historia yake ingekuwa inafundishwa shulen kuhusu mzee huyo aliekuwa kivutio kikubwa sio tu kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, bali hadi kwa wageni pia wakiwemo watalii kutoka ktk nchi mbali mbali za dunia hii.