Ilikuwa mwaka 1981

Kingunge Sakayo but I am happy for you for taking care of your responsibilities to the maximum of your ability
🙂🙂
Mmmmmh!!!
Thanks anyway!!!


Halafu nakutafuta, seriously!!
 
Reactions: BAK
Nna 6yrs hapo. Chama kimeshika hatamu, bidhaa madukani hakuna, tumetoka kumchapa nduli Idd Amin dada, only Radio ni RTD. Miziki ya Congo ya akina Lwambo Lwanzo Makiadi, Nzaya Nzayadio, wale wa Kavasha ndo unaipata kwenye tape. Mimi mpenzi sana wa DDC mlimani park, wakati ule nyimbo km Duniani kuna mambo ilitesa vilivyo. Wale wa Sumbawanga miaka Ile mtakumbuka Datoo Studio na Lyambaa. Radio za nje hasa Radio Deustch welle idhaa ya kiswahili ilitamba sana .
 
Hahahahaha kuna njemba huwa inapenda kujigamba enzi zake ilijirusha sana Mkirikiti Bar ndiyo nikamuuliza iko wapi hiyo Bar akaniambia iko kwa Mussa Hassan (Msasani)

Hahaaa, mkuu mitaa ya Maandazi Road utakuwa unaijua.
 
This is so deep,thnxs.
 
Mambo ya bima Lee orchestra siyoo?
Nakumbuka miaka ile (1982-1983) baadhi ya nyimbo kali za wakati huo zilizoifanya bendi ya Bima Lee kuvuma ni pamoja na Aziza, Kipepeo, Bilionea wa mapenzi, Shangwe ya Harusi, Zenaba, Kununanuna na Dunia Duara.
Na bila kusahau nyimbo nyingine za bendi hiyo ambazo mwimbaji wake kiongozi alikuwa ni marehemu Jerry Nashon (Dudumizi) ni pamoja na Mwamvua, Makulata. Enzi hizo nyimbo hizo hazikuwa tu kali bali zilikuwa zikitoa mafunzo kwa kila aliyekuwa akizisikiliza.
Nambukuka siku zile wanamuziki walio ifanya Bima Lee kung'ara ni pamoja na Jerry Nashon, Joseph Mulenga, Abdallah Gama, Athuman Momba, Dancun Ndumbalo na Suleiman Mwanyiro.
Nakumbuka Bima Lee ilitukonga na mtindo waliokuwa wakitamba nao wa Magnet 84 na baadaye wakauboresha na kuwa Magnet Tingisha. Wakati huo mashabiki tulimpachika Shaban Dede jina la utani tukamwita Mzee Tingisha kutokana na alivyouteka ulimwengu wa muziki kwa mtindo huo.
 
Pale tabora tulikuwa na KAUTA, wengine walikuwa na Kagera Retco, Kauma, Shinyanga Retco, Kaudo, Mbeya Retco, sijui nchi hii tulijikwaa wapi tu
CCM ndio chanzo cha yote hayo
 
Mkuu unaonekana uko deep sana na bima lee
 
Mkuu unaonekana uko deep sana na bima lee
Sio Bema Lee pekee mkuu, nilikua mdau mkubwa wa muziki wa Dansi. Na ukizingatia miaka hiyo ndio nilikua kijana, na kama ujuavyo ujana maji ya moto....[emoji2] [emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…