Ilikuwa mwaka 1981

Ilikuwa mwaka 1981

Kingunge Sakayo but I am happy for you for taking care of your responsibilities to the maximum of your ability
🙂🙂
Mmmmmh!!!
Thanks anyway!!!

Halafu nakutafuta, seriously!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nna 6yrs hapo. Chama kimeshika hatamu, bidhaa madukani hakuna, tumetoka kumchapa nduli Idd Amin dada, only Radio ni RTD. Miziki ya Congo ya akina Lwambo Lwanzo Makiadi, Nzaya Nzayadio, wale wa Kavasha ndo unaipata kwenye tape. Mimi mpenzi sana wa DDC mlimani park, wakati ule nyimbo km Duniani kuna mambo ilitesa vilivyo. Wale wa Sumbawanga miaka Ile mtakumbuka Datoo Studio na Lyambaa. Radio za nje hasa Radio Deustch welle idhaa ya kiswahili ilitamba sana .
 
Hahahahaha kuna njemba huwa inapenda kujigamba enzi zake ilijirusha sana Mkirikiti Bar ndiyo nikamuuliza iko wapi hiyo Bar akaniambia iko kwa Mussa Hassan (Msasani)

Hahaaa, mkuu mitaa ya Maandazi Road utakuwa unaijua.
 
Mkuu....,
Sikuzile Kinondoni ilkuwa inawaka moto kwa Vijana siku ya Jumapili. Lang'ata ambayo baadae ilikuja kuwa Club ASET na sasa kanisa, palikuwa ndo ukumbi wa Dansi za kuanzia mchana kwa Bendi ya Maquis. Ukija hapa mbele Vijana Jazz Pambamoto awamu ya pili chini ya uongozi wa Hemed Maneti walikuwa nao kila Jumapili mchana wanaporomosha Dansi, na siku hiyo ilipewa jina Vijana Day. Kwa kweli Maquis walikuwa wanajaa watu na Vijana wanajaa watu. Kulikuweko na wapenzi wa kudumu wa Vijana kama ilivyokuwa Maquis. Wakati huo nyimbo kama Ngalula, Makumbele zilikuwa zinalia Lang'ata huku Vijana wanateremsha Shingo feni, Ngapulila, Azda. Ushindani huu ulilazimisha bendi kujitahidi kupiga vizuri na kwa displine au la wapenzi wanahamia bendi jirani. Kuna wakati Vijana Jazz walikuwa wanaanza muziki saa kumi na moja jioni na kupumzika saa tatu na nusu usiku kisha kumaliza dansi saa nne. Maquis wakawa wanaanza saa kumi na kumaliza saa tano usiku. Na wakaanza kuruhusu mtu yeyote atakayekuwa kapigwa muhuri wa kuruhusu kutoka nje ya ukumbi Vijana Jazz,aliruhusiwa kuingia Maquis bure. Vijana wakabadili ratiba na kuanza kupiga saa 9 mchana, kwa mtindo wa bandika bandua, yaani muziki nonstop. Na kufuta kupumzika hadi saa tano. Hiyo ndo ilikuwa raha kwa wapenzi. Vijana haikuwa na show wakati wa Maneti, Lakini show ilikuja baadae katika kukabili show ya Maquis ambayo ilikuwq nzuri sana chini ya mwalimu wao Wabangoi. Majina makubwa yalitawala madansi hayo Maquis kulikuwa na Dekula Vumbi kwenye solo,second solo Mbwana Cox (aliyetoka Vijana Jazz), banza Mchafu Bass, Nguza Viking, Adios, Tshimanga Assossa,Parashi Lukumbule Vijana Jazz kulikwa Shaaban Wanted, Hemed Maneti, Eddy Sheggy, Adam Bakari, Kida Waziri, Abou Semhando, Rashid Pembe na wengine wengi, basi raha kila jumapili ilikuwa kama tamasha
This is so deep,thnxs.
 
Mambo ya bima Lee orchestra siyoo?
Nakumbuka miaka ile (1982-1983) baadhi ya nyimbo kali za wakati huo zilizoifanya bendi ya Bima Lee kuvuma ni pamoja na Aziza, Kipepeo, Bilionea wa mapenzi, Shangwe ya Harusi, Zenaba, Kununanuna na Dunia Duara.
Na bila kusahau nyimbo nyingine za bendi hiyo ambazo mwimbaji wake kiongozi alikuwa ni marehemu Jerry Nashon (Dudumizi) ni pamoja na Mwamvua, Makulata. Enzi hizo nyimbo hizo hazikuwa tu kali bali zilikuwa zikitoa mafunzo kwa kila aliyekuwa akizisikiliza.
Nambukuka siku zile wanamuziki walio ifanya Bima Lee kung'ara ni pamoja na Jerry Nashon, Joseph Mulenga, Abdallah Gama, Athuman Momba, Dancun Ndumbalo na Suleiman Mwanyiro.
Nakumbuka Bima Lee ilitukonga na mtindo waliokuwa wakitamba nao wa Magnet 84 na baadaye wakauboresha na kuwa Magnet Tingisha. Wakati huo mashabiki tulimpachika Shaban Dede jina la utani tukamwita Mzee Tingisha kutokana na alivyouteka ulimwengu wa muziki kwa mtindo huo.
 
Mkuu unaonekana uko deep sana na bima lee
 
Mkuu unaonekana uko deep sana na bima lee
Sio Bema Lee pekee mkuu, nilikua mdau mkubwa wa muziki wa Dansi. Na ukizingatia miaka hiyo ndio nilikua kijana, na kama ujuavyo ujana maji ya moto....[emoji2] [emoji2]
 
Back
Top Bottom