Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Kama kuna ambaye alikuwepo na hajaingia kusema kwamba alikuwepo, hiyovji shida yake. Kwa waliochangia.. ukisoma wanachoandika utajuwa tu hakuwepo.Kumbuka humu ndani tumo takribani 370,000 bila kuangalia drop outs, deceased na Kenyans. Ni wangapi kati ya hawa wana-fall kwenye hiyo 1-4?
Mkuu ulichonifurahisha ni pale uliposema wakati huo ulikuwa kounoni umetulia tuliii... kuna wengine wanautazama uzi huu kama dharau kwao, wakati ni kweli hawakuwepo...Kwani kutokujua ni dhambi mkuu, au wewe unajua kila kitu
Ni POWER MABULA.Kiingilio kwa Power Mwanamabula ilikuwa sh 5/= kwa mwanafunzi.
Usisahau na ile blue tulioweka ktk shati za Shule, kisha buibui wa pasi ktk shati.Embe mnang'ata kwa zamu mpaka mnafikia kokwa.
Teh teh teh naona jamaa alikuwa akijiita "sauti ya chuma" kweli mziki ni majigambo.Immaculata_ Bima Lee
Haloo Immaculata mama
Vipi Immaculata mama
Nakutafuta sikuoni mama
Napiga darubini sikupati mamaa
Napiga tarumbeta sikupati mamaa
Ni umbali gani ulipooo
Nipigie simu namba 26561
Hakyamungu nakupenda Immaculata natoka jandoni mama nishike mkono nipeleke mbele ya wazee
Nafanya nini nderakendr ?
Nakupendaaaa aa.................. Endelea mwenyewe
Hapo unawakuta jamaa waliotoka NGINDE Mulenga "Spoiler" gitaa la Solo, Mwanyiro "Computer" Bass Gitaa, Abdallah Gama, Rhythm Guitar wakiambatana na Shabaan Dede huku wakiwakuta wenyeji Nguli mwenyewe Jerry Nashon Dudumizi akina Roy Bashekanako, Momba "sauti ya chuma" etc
Huo ulikuwa muziki halisia wa Kitanzania na ubunifu wa hali ya juu bila kusaidiwa na Kompyuta!
Hivi hizi zilikuwa ni nguvu asilia au ni mazingaombwe?Humu ndani wamejaa watoto, ingawa tuna pidhana nao humu humu na tunawaita kwa jina pendwa (mkuu) mubashara, na walipojua matumizi ya nywila kuingia jf, basi hatu hemi kabisaaa......View attachment 452475
Kama kuna ambaye alikuwepo na hajaingia kusema kwamba alikuwepo, hiyovji shida yake. Kwa waliochangia.. ukisoma wanachoandika utajuwa tu hakuwepo.
Si unajua kuna watu wakiandika, wengine hukomenti...SHULE ZIMEFUNGWA? hii maana yake nini?
Inaitwa masalaHapo mfukoni una kipande cha gazeri umeviriga chumvi iliyochanganywa na pilipili kichaa na ikasagwa pamoja
Hatukuwa na hayo majina wakati huo...Inaitwa masala
Halafu mnasema maisha yalikua mazuri kila kitu foleniDuka la ushirika kununua sukari tena kilo za kuamuliwa, lazima ununue na sindano hutaki acha sukari
Nakumbuka foleni za unga wa yanga.
Hivi ubaya wa maisha ni foleni pekee? kwani leo hakuna foleni?NMB, NBC, barabarani zile siyo foleni?Halafu mnasema maisha yalikua mazuri kila kitu foleni
Kwanza huyu jamaa alikua ni pande la jitu, kwa lugha ya kisasa tungemuita giant.Hivi hizi zilikuwa ni nguvu asilia au ni mazingaombwe?