Ilikuwa mwaka 1981

Ilikuwa mwaka 1981

Kumbuka humu ndani tumo takribani 370,000 bila kuangalia drop outs, deceased na Kenyans. Ni wangapi kati ya hawa wana-fall kwenye hiyo 1-4?
Kama kuna ambaye alikuwepo na hajaingia kusema kwamba alikuwepo, hiyovji shida yake. Kwa waliochangia.. ukisoma wanachoandika utajuwa tu hakuwepo.

Si unajua kuna watu wakiandika, wengine hukomenti...SHULE ZIMEFUNGWA? hii maana yake nini?
 
Kwani kutokujua ni dhambi mkuu, au wewe unajua kila kitu
Mkuu ulichonifurahisha ni pale uliposema wakati huo ulikuwa kounoni umetulia tuliii... kuna wengine wanautazama uzi huu kama dharau kwao, wakati ni kweli hawakuwepo...
 
Daftari zimeandikwa HALIUZWI. Na lina nembo ya .ADAM NA HAWA.
 
Kule Morogoro kwenda wilaya zake tulipanda MORETCO.
 
Meeting points zilikuwa bombani, mtoni, kisimani au njiani wakati wa kutoka shule!
 
Shule za Sekondari zilikuwa za aina mbili tu, za SERIKALI na za KULIPIA. Na walionda hizo za KULIPIA tuliwaona......!
 
Immaculata_ Bima Lee

Haloo Immaculata mama
Vipi Immaculata mama
Nakutafuta sikuoni mama
Napiga darubini sikupati mamaa
Napiga tarumbeta sikupati mamaa

Ni umbali gani ulipooo
Nipigie simu namba 26561

Hakyamungu nakupenda Immaculata natoka jandoni mama nishike mkono nipeleke mbele ya wazee

Nafanya nini nderakendr ?

Nakupendaaaa aa.................. Endelea mwenyewe

Hapo unawakuta jamaa waliotoka NGINDE Mulenga "Spoiler" gitaa la Solo, Mwanyiro "Computer" Bass Gitaa, Abdallah Gama, Rhythm Guitar wakiambatana na Shabaan Dede huku wakiwakuta wenyeji Nguli mwenyewe Jerry Nashon Dudumizi akina Roy Bashekanako, Momba "sauti ya chuma" etc

Huo ulikuwa muziki halisia wa Kitanzania na ubunifu wa hali ya juu bila kusaidiwa na Kompyuta!
Teh teh teh naona jamaa alikuwa akijiita "sauti ya chuma" kweli mziki ni majigambo.
 
Kama kuna ambaye alikuwepo na hajaingia kusema kwamba alikuwepo, hiyovji shida yake. Kwa waliochangia.. ukisoma wanachoandika utajuwa tu hakuwepo.

Si unajua kuna watu wakiandika, wengine hukomenti...SHULE ZIMEFUNGWA? hii maana yake nini?

Nakubaliana na wewe kama alichosema [HASHTAG]#sky eclat[/HASHTAG] kinamaanisha waliochangia so far kwenye thread hii yaani aliposema 'humu' alimaanisha 'thread hii'.
 
Nimemkumbuka power Kyela alivyo kuwa anazuia gari mbili kwa mikono,ajabu alifariki kwa kugongwa na Peugeot 504 na kufariki papo hapo
 
Back
Top Bottom