GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Siwatetei Wakoloni, lakini, nafikiri kulikuwa na umuhimu wa wao kutawala baadhi ya nchi kwa kipindi hicho, hasa za Kiafrika, kama walivyofanya. Walinufaika na rasilimali za Afrika, lakini Waafrika nao hawakubaki kama walivyokuwa. Wamechangia mabadiliko chanya.
1. Walisadia kutokomeza baadhi ya mila potofu
Kwa mfano, baadhi ya makabila yalikuwa yakiamini kuwa kuzaa watoto mapacha au Zeru Zeru ni mkosi na hivyo walikuwa wakitupwa. Sheria walizozianzisha, pamoja na Elimu iliyopatikana kupitia taasisi za Kielimu na Kidini, zilisadia sana kupunguza na hata kutokomeza hizo mila mbaya
2. Elimu waliyoitoa iliwazaa "great thinkers!"
Nawataja baadhi yao: Julius K. Nyerere, Kwame Nkurumah, Robert Mugabe, Jomo Kenyatta, Nelson Mandela, Benjamin W. Mkapa, n.k. Huwa najiuliza, ikiwa Elimu ya Kikoloni ilikuwa ni dhaifu kuliko Elimu iliyotolewa baada ya Ukoloni kama tulivyokuwa tukifundishwa "mashuleni", iliwezaje kuwatengeneza Waafrika waliokuja kuwa viongozi mashuhuri duniani?
Mimi ninafikiri, pamoja na athari mbaya za Ukoloni, kuna faida pia ambazo wanafunzi huwa hawaambiwi. Wanakazaniwa tu kulishwa nusu taarifa kuwa umasikini wa Afrika ulichangiwa na Wazungu.
Viongozi, huo ni mtazamo wangu, lakini nipo tayari kuelimishwa!
Naomba kuwasilisha