Ilikuwa ni muhimu kwa baadhi ya nchi kutawaliwa na wazungu

Ilikuwa ni muhimu kwa baadhi ya nchi kutawaliwa na wazungu

Ni

Ni kweli, lakini itahitajika gharama kubwa sana ya muda na hata maisha ya watu. Maana mfumo tulionao umesha jiambukiza kwenye DNA zetu.
Swali la kujiuliza, tumeshaanza mchakato wa mabadiliko ya kifikra? Tumeshafanya maamuzi ya kubadilika kwa gharama yoyote Ile?

Ni kweli, kutakuwepo na gharama, tena siyo ndogo. Itahitaji kuacha ubinafsi, na kuwa "generational thinker". Ni lazima kujitahidi na hata kujitoa "sadaka' ikibidi, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni gharama sana, na sidhani kama mabadiliko makubwa yalishawahi kuwa marahisi. Lakini nia dhabiti ikiwepo, matokeo yatafikiwa, hata kama mchakato utagharimu sana.
 
Mkuu Charles177, mbona miaka 20 ni mingi sana?

Kwa rasilimali tulizo nazo, na kiwango cha Sayansi na Teknikojia iliyofikiwa duniani, miaka 10 tu ya "useriousness" yanatosha kuibadili Tanzania kabisa.

Ilimchukua miaka mingapi Mcanada, Dr. Williamson kuujenga mji wa Mwadui? Inasemekana kampuni ya Almasi ya Mwadui ilianzishwa mwaka 1940, lakini kufikia 1947, kupitia uwekezaji alioufanya, alikuwa ameshafanikuwa kupafanya Mwadui miongoni mwa miji ya kisasa Afrika.
Uko sawa kabisa. Rwanda wametokea kwenye vita. Watu milioni moja wameuwa, nguvu kazi kubwa ilipotea ndani ya miaka ishirini watoto wanatumia laptop kujifunza, kuna viwanda vya ku-assemby Volkswagen, wanatengeneza mobile phone na kuna usalama mkubwa, unaweza kulala milango wazi.

Hawana rasilimali yoyote ya maana, wanategemea bandari ya Dar na chakula kingi kutoka Tanzania. Imagine wangekuwa na nchi kama TZ.
 
Back
Top Bottom