Ilikuwaje hadi Wachina wakampa Rais Kikwete Uprofesa wa heshima?

Ilikuwaje hadi Wachina wakampa Rais Kikwete Uprofesa wa heshima?

Unaweza ukamsifia msichana kwamba ana shingo ya upanga, mweupe, mrefu, amejaaliwa, kiuno nyigu hata Kama anatokea Mahenge naye akaamini.
 
Nimepitiapitia makabrasha hapa nimeona Hata Oxford University wanatoa honorary professorship

Unajua professor huwa ni academic rank kwenye chuo siyo kwamba ni title. Professor wa chuo kimoja anaweza askubalike kuwa profesa wa chuo kingine. Zamani sana alikuwa mwalimu mmoja wa hesabu pale UDSM akitokea India ambako alikuwa profesa, lakini alipofika UDSM akawa senior Lecturere. Sas hawa wanapoiwat honorary professor nadhani ni kuwakubali kwenye chuo chao, ila nilikuwa sijawahi kuisikia. Ninajua Honoris causa za Doctorate tu, ambazo mtu hupewa pamoja na priveleges zake na rights zake kiasi kuwa popote duniani anatambulika kuwa ana honorary doctorate.
 
Prof ni Dokta vile vile.
Hiyo Dokta yenyewe nakumbuka alipewa kimagumashi kwelikweli na kichuo ka uchochoroni kutoka huko magharibi. Hawa watu wanawadharau sana watu weusi, hasa kutoka Afrika.

Samahani, naondoa hilo la watu weusi, na kutoka Afrika. Sijasikia M7 au Uhuru Kenyatta, au mwingine yeyote katika nchi zinazotuzunguka. Naona huu uchizi ni waTanzania pekee ndio wanaoupewa.
 
Hiyo inaitwa "mjinga msifie".Wachina si viumbe wa kuwakaribisha tena katika ardhi ya watanzania.Jamaa walivuna rasilimali zetu ikiwemo wanyama tembo na laiti ujinga ule ungeendelea leo mbuga zetu zingegeuka kuwa maeneo ya makazi.
 
Unajua waswahili kwa kupenda title hatuachwi nyuma: Basi iwe hivi: His Excellency, Professor, Dr, Retired President, Colonel Kikwete.

Unakumbuka His Excellency, President for Life, Field Marshal Alhaji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular, Uncrowned King of Scotland and Professor of Geography.

Waswahili kwa title hatujambo; leo hii mke wangu akijifungua mtoto tukamwita Mchwa, basi itabidi nipewe title kuonyesha kuwa nina mtotot anaitwa Mchwa kwa kuitwa ya Baba Mchwa!
Mwacheni j.k apumzike jwa amani
 
Kweli JK ni "thread maker", kipindi chake JF ilishamiri kwelikweli
Naona Kichuguu amemiss enzi za "Mzee Mwanakijiji, ES Sauti ya umeme, Mwafrika wa Kike, Reverend Kishoka, Mukandala, Gamba la nyoka, Fundi Mchundo, Nyani Ngabu, Echolima" na wengineo. Enzi za kumkoma nyani giladi
 
Hiyo Dokta yenyewe nakumbuka alipewa kimagumashi kwelikweli na kichuo ka uchochoroni kutoka huko magharibi. Hawa watu wanawadharau sana watu weusi, hasa kutoka Afrika.

Samahani, naondoa hilo la watu weusi, na kutoka Afrika. Sijasikia M7 au Uhuru Kenyatta, au mwingine yeyote katika nchi zinazotuzunguka. Naona huu uchizi ni waTanzania pekee ndio wanaoupewa.
Inawezekana hata M7 na Uhuru wanatunukiwa vingi tu... lakini Tanzania ndo nchi ambayo title inashikiwa bango kuliko hata uwezo wa mhusika.
Hii ipo sana kwa Madokta, Maprof, waheshimiwa... hadi inaboa...
Sifa za reja reja sana...!!
 
Back
Top Bottom