Ilikuwaje hadi Wachina wakampa Rais Kikwete Uprofesa wa heshima?

Unaweza ukamsifia msichana kwamba ana shingo ya upanga, mweupe, mrefu, amejaaliwa, kiuno nyigu hata Kama anatokea Mahenge naye akaamini.
 
Unajua professor huwa ni academic rank kwenye chuo siyo kwamba ni title. Professor wa chuo kimoja anaweza askubalike kuwa profesa wa chuo kingine. Zamani sana alikuwa mwalimu mmoja wa hesabu pale UDSM akitokea India ambako alikuwa profesa, lakini alipofika UDSM akawa senior Lecturere. Sas hawa wanapoiwat honorary professor nadhani ni kuwakubali kwenye chuo chao, ila nilikuwa sijawahi kuisikia. Ninajua Honoris causa za Doctorate tu, ambazo mtu hupewa pamoja na priveleges zake na rights zake kiasi kuwa popote duniani anatambulika kuwa ana honorary doctorate.
 
Prof ni Dokta vile vile.
Hiyo Dokta yenyewe nakumbuka alipewa kimagumashi kwelikweli na kichuo ka uchochoroni kutoka huko magharibi. Hawa watu wanawadharau sana watu weusi, hasa kutoka Afrika.

Samahani, naondoa hilo la watu weusi, na kutoka Afrika. Sijasikia M7 au Uhuru Kenyatta, au mwingine yeyote katika nchi zinazotuzunguka. Naona huu uchizi ni waTanzania pekee ndio wanaoupewa.
 
Hiyo inaitwa "mjinga msifie".Wachina si viumbe wa kuwakaribisha tena katika ardhi ya watanzania.Jamaa walivuna rasilimali zetu ikiwemo wanyama tembo na laiti ujinga ule ungeendelea leo mbuga zetu zingegeuka kuwa maeneo ya makazi.
 
Mwacheni j.k apumzike jwa amani
 
Kweli JK ni "thread maker", kipindi chake JF ilishamiri kwelikweli
Naona Kichuguu amemiss enzi za "Mzee Mwanakijiji, ES Sauti ya umeme, Mwafrika wa Kike, Reverend Kishoka, Mukandala, Gamba la nyoka, Fundi Mchundo, Nyani Ngabu, Echolima" na wengineo. Enzi za kumkoma nyani giladi
 
Inawezekana hata M7 na Uhuru wanatunukiwa vingi tu... lakini Tanzania ndo nchi ambayo title inashikiwa bango kuliko hata uwezo wa mhusika.
Hii ipo sana kwa Madokta, Maprof, waheshimiwa... hadi inaboa...
Sifa za reja reja sana...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…