Ilikuwaje siku ya kwanza unachangia jambo humu jf ?

Ilikuwaje siku ya kwanza unachangia jambo humu jf ?

Mimi niliuliza swali kuwa aliechora ramani ya dunia yeye alikuwa wapi au dunia ipi wakati anachora mpaka sasa sijawahi pata hilo jibu
Leo niko huku kidogo.

Angalizo !

Kama uzi utakuwa una fanana au umeshawahi kuwekwa humu,ni aula nikakuzwa.

Sina kumbukumbu vizuri,ila nakumbuka ulikuwa uzi fulani unahusu "Cloning" (Nitasahihishwa juu ya anuani ya uzi husika) katika jukwaa la "Jamii Intelligence", nilijitutumua sana siku hiyo,huku kichwani nina mawazo ya kuwa humu kuna vichwa balaa na wako makini sana na ukikosea lazima uwekwe sawa,papo hapo. Hiyo siku nilikuwa makini sana,yaani nilikuwa naandika huku nafuta futa mara kadhaa. Uoga ulinijaa sana siku ile,nahisi ilikuwa ni sababu ya ugeni na kasumba iliyokuwepo kichwani mwangu.
 
Au thread ipo jukwaani mtu anacoment pm.

Huwa napata shida muda unakuta mtoto umemuelewa halafu kufunguka "Changanyikeni" aibu,ukienda PM kumefungwa,unatamani uwe na uwezo upige ukelele au umshike mkono muhusika.
 
Back
Top Bottom