Ilikuwaje ukaibiwa simu??

Uzembe ahahah
Hapana sio uzembe, niliweka charge kwenye saloon ya kiume ya mtoto wa mama yangu mkubwa kisha nikatoka kdg kama nusu saa ile narudi nakuta waya wa charge unanining'inia peke yake na yule ndugu yangu akanambia yeye alikua busy na kunyoa mtu sasa kuna kijana aliingia anahisi yeye ndo amechukua kwa asilimia πŸ’―.Tulimbana yule kijana akakana ina nikaona nipotezee tu mama nikisema nilipeleke kisheria hata yule ndugu yangu angewekwa ndani.
 
Daaah sema mkuu upendi tu kuweka mambo complicated ila ingekua mimi hapo ningekinukisha aiseee
 
I wish ungeenda deep kwenye hiyo simu ya tatu.
 
Nimeibiwa na kupoteza Simu kama mara kumi.

πŸ‘‰πŸΎHivi mara 2 nilangusha kwenye bajaj,Hii ilikuwa ni Iphone na Oppo K3 hii simu ilikuwa iko vizuri mno.,tena hizi simu kwa nyakati tofauti nilikuwa na chati na watu niliokuwa naenda kumeet nao kwa ajili ya kukutana ule ubusy wakati wa kushuka nikasahau.

πŸ‘‰πŸΎMara 2 kwenye Dala dala tena hiyo moja nakumbuka nilikuwa nimevaa na earphone kabisa mpka leo sielewi ilikuwaje.Moja ilikuwa Nokia Asha hii jamaa alichomoa kwenye Dala dala pale Azizi Ally na Nokia 5.2 hii nikiwa na earphone sema nilikuwa na wenge la usingizi hatari picha linaanza nimeshavushwa vituo kadhaa nashuka na earphone tu bila simuπŸ˜…

πŸ‘‰πŸΎ Mara 1 nimeibiwa nikiwa mazingira ya Shuleni siku nimemaliza mitihani ya advance naenda ofisini kuchukua nakuta mwingine kaondoka nayo na Mimi nikaondoka na Pasi na vifaa vingine vya Electronics ili kufidia simu yangu maana vifaa vyote vya umeme vilichukuliwa na kutunzwa sehemu moja so ikawa ni mjanja kuwahi.

πŸ‘‰πŸΎMara moja nyumbani kwangu jamaa kaiba usiku wa manane. Hii ilikuwa Samsung A8 plus.

πŸ‘‰πŸΎMoja nayo ilikuwa Samsung nilisahau dukani kwa Mtu sema kuna kipengele kwenye ile simu ulikuwa unaweza kuweka namba mbili za emergence kama mtu mwingine akiweka lain basi ile namba mpya inakutumia ujumbe kwenye Emergence namba .

Basi Jamaa kila akiweka line nyingine ninae ilimradi tu awe na salio au kifurushi cha ujumbe. Hii ilibidi jamaa amtumie mtu kunirudishia maana kila anaempa lazima nimpigie naomba urejeshe simu, tena na mwambia hiyo simu inadetails muhimu naomba usifanye chochote kile.

πŸ‘‰πŸΎMara mbili nimepoteza kwenye private car mpaka leo sielewi nini kilitokea moja ilikuwa Techo nyingine Samsung. Nikama zilitokomea kimiujiza.

πŸ‘‰πŸΎMoja nikiwa Jeshini. Hii nilidondosha wakati wa Gwaride. Na kuna siku tukiwa out kuna jamaa nikamuona nayo nikanfuata nikamwelekeza akagomea nikachana nae. Hii ilikuwa Nokia 2700 nilikuwa naitumia kuchungulia Jamii Forum kwaa miaka ile.
 
Chuo gani hicho waizi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hii kaliii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…