Ilikuwaje ukaibiwa simu??

Ilikuwaje ukaibiwa simu??

Uzembe ahahah
Hapana sio uzembe, niliweka charge kwenye saloon ya kiume ya mtoto wa mama yangu mkubwa kisha nikatoka kdg kama nusu saa ile narudi nakuta waya wa charge unanining'inia peke yake na yule ndugu yangu akanambia yeye alikua busy na kunyoa mtu sasa kuna kijana aliingia anahisi yeye ndo amechukua kwa asilimia 💯.Tulimbana yule kijana akakana ina nikaona nipotezee tu mama nikisema nilipeleke kisheria hata yule ndugu yangu angewekwa ndani.
 
Hapana sio uzembe, niliweka charge kwenye saloon ya kiume ya mtoto wa mama yangu mkubwa kisha nikatoka kdg kama nusu saa ile narudi nakuta waya wa charge unanining'inia peke yake na yule ndugu yangu akanambia yeye alikua busy na kunyoa mtu sasa kuna kijana aliingia anahisi yeye ndo amechukua kwa asilimia 💯.Tulimbana yule kijana akakana ina nikaona nipotezee tu mama nikisema nilipeleke kisheria hata yule ndugu yangu angewekwa ndani.
Daaah sema mkuu upendi tu kuweka mambo complicated ila ingekua mimi hapo ningekinukisha aiseee
 
story za watu zinachekesha mno..!!

simu ya kwanza kupotea, hii nahisi sikuibiwa nilifanya uzembe, nilikuwa nachat kwenye daladala tulikuwa wanachuo wengi tunaenda zetu Coco beach, enzi hizo tunajikuta wajanja balaa, nikawa nachat zangu nairudishia mapajani, muda wa kushuka kwenye daladala nikanyanyuka tu na mkoba wangu shwaaaaaaa, nahisi ilidondoka na zile purukushani sikuhisi chochote..!!
Nafika chini sioni simu na daladala ishayeyaa, ilikuwa bado mpya iliniuma balaa..!!

Simu ya pili, mzee hii nilikabwa Arusha na vibaka,😂😂
Hili tukio huwa linachekesha sana lakini lilinifanya kuwa traumatized vibaya mno, usiombe kubananishwa ukutani na majamaa wawili halafu kuna mvua flani na kigiza giza hivi, na hapo nipo hatua chache mno kufika nyumbani jumlisha nimevaa ki skirt kifupi cha kumwaga, niliwatolea mpaka hela Mimi mwenyewe ili wasije waza vitu vingine, siwezi sahau hii..!!

Simu ya tatu, walaqhi' Mimi nimeshindikana, japo story zote hizi zimetokea miaka mingi mno iliyopita, hii sasa ukiskia uzembe ndiyo huu, hii huwa hata siwaambii watu maana ni aibu, nilitapeliwa hii simu kijinga sana walaqhi', nilikuja kujicheka baadaye kabisa nikajiona bonge moja ya phaller..!!

Simu ya nne, hii ni Ile style ya kupuliziwa dawa ya usingizi dirisha mpaka linafunguliwa hujui, unaamka asubuhi unaskia kichwa kizito balaa, hakuna simu wala pochi yenye Pesa za kazini na miwani ya macho, wale wajinga waliiba mpaka lipstick halafu mkoba wakautupa nje huko, hii ilinikuta nikiwa Tanga, mzee ukiskia kudata ndiyo hii, hii hata sikulia tena, nilihuzunika tu sababu ya Pesa za watu baasii, ila kwenye simu nilikuwa nimeshakuwa gaidi..!!

Simu zote nilizotumia hivi karibuni sasa, it's either nigawe, iharibike yenyewe ama niuze, nimekuja kuwa makini balaa, enweiz, si sana sababu hakuna aijuaye kesho..!!😂😂
I wish ungeenda deep kwenye hiyo simu ya tatu.
 
Nimeibiwa na kupoteza Simu kama mara kumi.

👉🏾Hivi mara 2 nilangusha kwenye bajaj,Hii ilikuwa ni Iphone na Oppo K3 hii simu ilikuwa iko vizuri mno.,tena hizi simu kwa nyakati tofauti nilikuwa na chati na watu niliokuwa naenda kumeet nao kwa ajili ya kukutana ule ubusy wakati wa kushuka nikasahau.

👉🏾Mara 2 kwenye Dala dala tena hiyo moja nakumbuka nilikuwa nimevaa na earphone kabisa mpka leo sielewi ilikuwaje.Moja ilikuwa Nokia Asha hii jamaa alichomoa kwenye Dala dala pale Azizi Ally na Nokia 5.2 hii nikiwa na earphone sema nilikuwa na wenge la usingizi hatari picha linaanza nimeshavushwa vituo kadhaa nashuka na earphone tu bila simu😅

👉🏾 Mara 1 nimeibiwa nikiwa mazingira ya Shuleni siku nimemaliza mitihani ya advance naenda ofisini kuchukua nakuta mwingine kaondoka nayo na Mimi nikaondoka na Pasi na vifaa vingine vya Electronics ili kufidia simu yangu maana vifaa vyote vya umeme vilichukuliwa na kutunzwa sehemu moja so ikawa ni mjanja kuwahi.

👉🏾Mara moja nyumbani kwangu jamaa kaiba usiku wa manane. Hii ilikuwa Samsung A8 plus.

👉🏾Moja nayo ilikuwa Samsung nilisahau dukani kwa Mtu sema kuna kipengele kwenye ile simu ulikuwa unaweza kuweka namba mbili za emergence kama mtu mwingine akiweka lain basi ile namba mpya inakutumia ujumbe kwenye Emergence namba .

Basi Jamaa kila akiweka line nyingine ninae ilimradi tu awe na salio au kifurushi cha ujumbe. Hii ilibidi jamaa amtumie mtu kunirudishia maana kila anaempa lazima nimpigie naomba urejeshe simu, tena na mwambia hiyo simu inadetails muhimu naomba usifanye chochote kile.

👉🏾Mara mbili nimepoteza kwenye private car mpaka leo sielewi nini kilitokea moja ilikuwa Techo nyingine Samsung. Nikama zilitokomea kimiujiza.

👉🏾Moja nikiwa Jeshini. Hii nilidondosha wakati wa Gwaride. Na kuna siku tukiwa out kuna jamaa nikamuona nayo nikanfuata nikamwelekeza akagomea nikachana nae. Hii ilikuwa Nokia 2700 nilikuwa naitumia kuchungulia Jamii Forum kwaa miaka ile.
 
1. Ya kwanza niliibiwa nikiwa form 5, nilipoteza funguo ya chumba nikabaki na funguo ya akiba
Sikujisumbua kutafuta funguo iliyopotea.
Asubuhi nimeenda shule nikaacha simu kwenye chaji, niliporudi, kuingia ndani simu haipo.

2. Niliibiwa chuo mwaka wa 1, nimeingia kwenye paper, simu nikaacha kwenye begi nikaweka mbele
Nilipomaliza paper kwenda kuchukua begi simu hamna.
Chuo gani hicho waizi
 
Mimi sikuibiwa ila nilikaa kwenye gari na dada mmoja mzuriiii, ikabidi nimpe simu aandike namba zake, akaipokea akawa anaandika namba ikatokea dereva kagonga dog, ikawa tafrani pale nikashuka haraka nikapanda gari lingine bila kusahau nimempa simu yule manzi....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hii kaliii
 
Back
Top Bottom