Ilikuwaje ukaibiwa simu??

Ilikuwaje ukaibiwa simu??

story za watu zinachekesha mno..!!

simu ya kwanza kupotea, hii nahisi sikuibiwa nilifanya uzembe, nilikuwa nachat kwenye daladala tulikuwa wanachuo wengi tunaenda zetu Coco beach, enzi hizo tunajikuta wajanja balaa, nikawa nachat zangu nairudishia mapajani, muda wa kushuka kwenye daladala nikanyanyuka tu na mkoba wangu shwaaaaaaa, nahisi ilidondoka na zile purukushani sikuhisi chochote..!!
Nafika chini sioni simu na daladala ishayeyaa, ilikuwa bado mpya iliniuma balaa..!!

Simu ya pili, mzee hii nilikabwa Arusha na vibaka,πŸ˜‚πŸ˜‚
Hili tukio huwa linachekesha sana lakini lilinifanya kuwa traumatized vibaya mno, usiombe kubananishwa ukutani na majamaa wawili halafu kuna mvua flani na kigiza giza hivi, na hapo nipo hatua chache mno kufika nyumbani jumlisha nimevaa ki skirt kifupi cha kumwaga, niliwatolea mpaka hela Mimi mwenyewe ili wasije waza vitu vingine, siwezi sahau hii..!!

Simu ya tatu, walaqhi' Mimi nimeshindikana, japo story zote hizi zimetokea miaka mingi mno iliyopita, hii sasa ukiskia uzembe ndiyo huu, hii huwa hata siwaambii watu maana ni aibu, nilitapeliwa hii simu kijinga sana walaqhi', nilikuja kujicheka baadaye kabisa nikajiona bonge moja ya phaller..!!

Simu ya nne, hii ni Ile style ya kupuliziwa dawa ya usingizi dirisha mpaka linafunguliwa hujui, unaamka asubuhi unaskia kichwa kizito balaa, hakuna simu wala pochi yenye Pesa za kazini na miwani ya macho, wale wajinga waliiba mpaka lipstick halafu mkoba wakautupa nje huko, hii ilinikuta nikiwa Tanga, mzee ukiskia kudata ndiyo hii, hii hata sikulia tena, nilihuzunika tu sababu ya Pesa za watu baasii, ila kwenye simu nilikuwa nimeshakuwa gaidi..!!

Simu zote nilizotumia hivi karibuni sasa, it's either nigawe, iharibike yenyewe ama niuze, nimekuja kuwa makini balaa, enweiz, si sana sababu hakuna aijuaye kesho..!!πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Simu 5 nimeibiwa kwa ajili ya ulevi wa bia. Simu 1 tu ndio niliibiwa kawaida niliacha dar nikaenda mkoa mwingine, kuna watu nikawapigia simu wafanye usafi ndio wakasepa na simu nilipoweka.
Nilipowauliza wakasema hawakuiona.
 
Wabongo wana asili ya wizi na udokozi
Ni tabia ya kishenzi sana
Bora nikabwe na ninyang'anywe simu kuliko huu wizi wa kidokozi
 
Mimi sikuibiwa ila nilikaa kwenye gari na dada mmoja mzuriiii, ikabidi nimpe simu aandike namba zake, akaipokea akawa anaandika namba ikatokea dereva kagonga dog, ikawa tafrani pale nikashuka haraka nikapanda gari lingine bila kusahau nimempa simu yule manzi....
 
Mimi sikuibiwa ila nilikaa kwenye gari na dada mmoja mzuriiii, ikabidi nimpe simu aandike namba zake, akaipokea akawa anaandika namba ikatokea dereva kagonga dog, ikawa tafrani pale nikashuka haraka nikapanda gari lingine bila kusahau nimempa simu yule manzi....
Haha dog kaharibu mipango yote🀣🀣
 
1. Ya kwanza niliibiwa nikiwa form 5, nilipoteza funguo ya chumba nikabaki na funguo ya akiba
Sikujisumbua kutafuta funguo iliyopotea.
Asubuhi nimeenda shule nikaacha simu kwenye chaji, niliporudi, kuingia ndani simu haipo.

2. Niliibiwa chuo mwaka wa 1, nimeingia kwenye paper, simu nikaacha kwenye begi nikaweka mbele
Nilipomaliza paper kwenda kuchukua begi simu hamna.
Hii ya pili ni uzembe wa kiwango cha lami
 
Mteja alikuja dukani duka lilikuwa jipya akawa anaagiza vitu vingi Kwa mkupuo , alikuwa anaagiza vitu vinavyohitaji kupanda na ngazi. Baadae akaghaili kununua hata hivyo vitu. Akawa ameondoka na simu.
Kama mimi vile ndio simu ya kwanza na ya mwisho kuibiwa
 
Back
Top Bottom