Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mm nimeachana nae sabab alikosa uvumulivu wa muda mfupi na akaamua kutoa ujauzito wangu binti yule,Wakuu kwema?
Kila mtu amewahi kupitia kwenye mahusiano. Kuna kipindi mtu anakuwa kwenye mahusiano yenye furaha isiyo kifani hadi anaona kama dunia yote ni ya kwake. Ila mambo yanapogeuka, anajikuta kwenye stress nzito hadi anatamani dunia imdondokee afe tu.
Sasa hebu tushare inakuwaje wapenzi wale waliokuwa wakipendana na kwa dhati, wanatokea kuachana vibaya vibaya, sababu hasa huwa nini?
Binafsi, nilimuacha kwa sababu alikuwa hatulii, ana tamaa ya kupitiliza, pesa, ngono, maisha mazuri. Nikaona ataniletea stress mbeleni. Wewe je?