Iikuwa mwaka 1991, mechi ya simba na yanga. Tulikuwa tunaishi kota za kilimo huko kilosa morogoro, basi wafanyakazi wenzake na mzee wangu walikusanyika sehemu moja kusikiliza mpira redioni, walikuwa wanabishana sana. Basi pale nyumbani watoto tukawauliza wazazi wao wanapenda timu ipi; Baba akajibu anapenda simba na mama anapenda yanga basi watoto tukajigawa, wanao mfuata mama au baba. Mimi nilimfuata mama yanga, kaka yangu akamfuata baba. Tokea mwaka huo nilikuwa na umri chini ya miaka kumi mpaka leo naipenda yanga. SIKUMBUKI timu gani ilishinda ila mzee alikasirika.