Ilikuwaje ukawa mshabiki wa Simba au Yanga?

Ilikuwaje ukawa mshabiki wa Simba au Yanga?

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Nimekuwa mshabiki wa Simba kwa muda mrefu.

Chanzo ni kwamba; jirani na nyumba niliyokuwa nikiishi mkoani Mwanza walikuwa wakifika wachezaji wa Yangu akina Abeid Mziba na Omary Hussein. Watoto wote ikawa ni Yanga kasoro baba yangu. Nikaamua kujiunga naye na kuwa mwekundu.

Nini kilikufanya uwe shabiki wa Yanga au Simba?
 
Mie shabiki wa Simba. Kilichonifanya niwe shabiki ni kuwa baba yangu alikuwa anapenda michezo sana na ikifika 1945hrs lazima asikilize kipindi kile RTD. Sasa miaka hiyo 1990 na kuendelea hasa 1992 na 1993 kila ukisikiliza mechi ni Simba tu hasa za CAF. Basi Simba kipindi kile ilikuwa balaa nikajikuta nimeipenda maana mie nimeanza kuifahamu Simba kabla ya Yanga
 
Wapambanapo wawili huwa napendelea mnyonge ashinde sasa hawa SIMBA walizidi kuonewa walionizunguka wote yanga yanga mm nikabaki kwa mnyonge hadi Leo SIMBA damu ila siwezi kuvunja viti kwa kuwa lengo langu ni kuifariji si kuitia hasara
 
Nimeiona simba ikisimama kama timu ya mpira.Haina usiasa ndani yake.Ni timu ya ccm na ukawa wote tumo huko.Yanga ina mapropaganda ya kichama chama.Ndiyo maana imekua ovyo katika uwakilishi wake nje.
 
Nimeiona simba ikisimama kama timu ya mpira.Haina usiasa ndani yake.Ni timu ya ccm na ukawa wote tumo huko.Yanga ina mapropaganda ya kichama chama.Ndiyo maana imekua ovyo katika uwakilishi wake nje.
Hao wanaowakilisha vizuri wameishachukua kombe lipi la CAF?
Ndoa ni kumuweka mke ndani sio kuishia kutongoza, kupeleka barua, kutoa mahari nk. Hayo yote hayana maana kama kitendo cha kufunga ndoa (kuchukua kombe) hakikufanyika!!
 
Hili linataka kugeuka jukwaa la Simba. Hivi watu wa naona aibu kuwa Yanga?
 
mi yanga bhana nliipenda tu,tangu nikiwa mdgo baada ya kuona baba angu mdgo anashabikia timu hyo.na ilikuwa ikiadhibu timu zngne kitambo toka nikiwa mdgo dats why mpaka lep niko yanga
 
Apo awali sikuwa mshabiki wa timu za nyumbani.Manchester niliona inatosha kbs.kuna siku wkt yanga ikipokea vipigo mfululizo,ilishinda mechi moja kwa bao la Bernard mwalala.sasa nikashangaa daddy angu anapiga simu na kusema "BOLA TUMEWAFUNGA HAWA JAMAA MANAKE WANAONGEA" nikaona hii timu ina kitu special tofauti na simba ndo mpaka Leo
 
Iikuwa mwaka 1991, mechi ya simba na yanga. Tulikuwa tunaishi kota za kilimo huko kilosa morogoro, basi wafanyakazi wenzake na mzee wangu walikusanyika sehemu moja kusikiliza mpira redioni, walikuwa wanabishana sana. Basi pale nyumbani watoto tukawauliza wazazi wao wanapenda timu ipi; Baba akajibu anapenda simba na mama anapenda yanga basi watoto tukajigawa, wanao mfuata mama au baba. Mimi nilimfuata mama yanga, kaka yangu akamfuata baba. Tokea mwaka huo nilikuwa na umri chini ya miaka kumi mpaka leo naipenda yanga. SIKUMBUKI timu gani ilishinda ila mzee alikasirika.
 
Mimi ni mshabiki mkubwa wa Simba. Nimeipenda Simba toka nazaliwa (nina miaka 41 sasa) kwa sababu karibu ukoo wangu wote ni washabiki wa Simba (Lushoto kwa upande wa baba na Muheza kwa mama). Ingawa nilikuwa nacheza kikapu kwenye ujana wangu, nilikuwa sikosi mechi za Simba uwanja wa zamani wa Taifa. Kilele cha upenzi wangu ni mwaka 1996. Nilikuwa nampenda sana Hussein Marsha. Mjomba wa rafiki yangu ni Juma Amir Maftah, wakati huo nae anaichezea Simba. Basi akafanya maarifa tukaenda kumchukua Maftah halafu tukaenda kumchukua Marsha kwake na gari yangu. Nikawapeleka mazoezini uwanja wa Karume siku hiyo. Sitaweza kusahau siku ile. Marsha alikuwa ananifurahisha sana, pamoja na George Magere Masatu na Mohammed Mwameja. Pia sitasahau shughuli za Zamoyoni Mogella miaka ya 80 pamoja mwanzoni mwa miaka ya 90 nikimshuhudia akiiongoza Simba dhidi ya Sports Club Villa kwenye CECAFA cup. Kwa sasa ninaishi nje ya nchi kwa miaka 20 lakini ninaifuatilia timu yangu kuliko hata watu waliopo Tanzania. Nikirudi kutembelea ndugu zangu, huwa ni lazima nihudhurie mechi zake. Hii timu kamwe sitaacha kuishabikia mpaka mwisho wa maisha yangu.
 
Ile historia ya kuwatoa kamas mehalla el kubra misri ndo imenifanya shabiki
 
Back
Top Bottom