Ilikuwaje watu wakaamini kwamba Tanzania inaweza kuendelea bila kushirikiana na dunia?

To be honest i admire your reasoning. Umeandika vyema.

I believe 'diplomacy is an art of compromise'

Sasa kwa magufuli hili lisingewezekana hawezi 'kucompromise' maana deep down kiasili yeye ni mtu wa kuamini anachokiamini yeye tu, hashauriki na hili amelisema mara kadhaa ata hadharani kwamba 'mimi ni jiwe' , 'siyumbishwi' , 'sishauriki' , 'tena mkijaribu kunishauri ndo mnakua mnaharibu kabisa' . Vitu vingi katika international scale kaviharibu kabisa na it will take time kuvirepair, kaua soko la korosho, kavunja mikataba mingi kiholela, ndege zimekamatwa nje, nchi imefunguliwa kesi nyingi za madai kwenye mahakama na wawekezaji waliofukuzwa au kuvunjiwa mikataba yao bila kufuata utaratibu, wakati dunia ikijitahid kupambana na janga la korona ye anakwambia korona haipo hiyo ni michezo tu ya wazungu, n.k. n.k

Mtu yeyote yule anayekataa au anayebisha kwamba Magufuli hajairudisha nyuma Nchi katika nyanja na sera za uhusiano wa kimataifa basi huyo atakua tu naye ni mbishi wa kiasili kama magufuli na hatuna budi bali inabidi tumpuuze

Sasa turudi kwenye hoja yako ya msingi ambayo ningependa pia wachangiaji wanaofuta wajikite nayo ni kwamba 'vichwa vyetu au think tanks wa nchi hii kwenye vyombo vyetu nyeti vya ulinzi na usalama vilikua wapi wakati haya yote yanatendeka???'
Hapa ndipo kuna hoja ya msingi inayohitaji majibu ya kina. Na kama walikaa kimya na mpaka leo wapo kwenye nafasi zao hata kama Uongozi wa juu umebadilika tutawaamini vipi kama wataweza kutuvusha salama sisi kama taifa.
 
Hivi mtoa mada unadhani kabisa hayo mambo uliyoyaandika hapo juu jiwe angeyajua kweli?

Yeye nje ya mabarabara hakua anajua chochote kile khs Mambo ya diplomasia, uchumi, usalama etc
Trust me JPM was no fool. He was very intelligent. Alijua kujenga hoja. Kwa namna ya kipekee kabisa alijua pia namna ya kuwaaminisha watu yale aliyotaka watu wayaamini. He was well informed. He had access to every inch of information you can imagine of. He was a hard worker. Alisoma sana kila taarifa aliyopewa na wasaidizi wake. He always slept late. A very hard working man. The question is why did he act the way he acted while he knew all that was required to be done yet he did the exact opposite.
 

Hahahah hivi ni kazi ya rais kusema eti nalala na ma file kitandani na unakuja kusema hadharani?Ili uonekane hard worker?Unajua maana ya segregation of duties?Unajua maana ya ku-delegate?

Zaidi ya kujua KM za barabara kwny mambo mengine alikua mweupe.Naked truth.
 
Amekuepushia na kiongozi muovu bila kumwaga damu!

Vipi sasa mko vizuri sana uovu umeisha, madini mna share za 50/50? Hamuibiwi tena, nchi sasa iko mikononi mwa wazalendo. Mko vizuri ee?
 
Watu hawakuwa wanaamini ule utapeli, bali ilikuwa ni shuruti. Na ilikuwa ukionyesha kwenda kinyume na ule utapeli unatekwa, kuuwawa au kubambikiwa kesi. Yaani tulipata kiongozi muovu, hisia zake akawa anatulazimisha tuziamini!
Usilalamike sasa!

Mshukuru mungu wako sasa hivi uko vizuri sana
 
Kwa hiyo mkataba hata kama ni mbovu wa kinyonyaji unatakiwa kuchekelea tu? Ndio diplomacy hiyo?
 
Mambo mengine kama yapi?

Hao waliokuwa wanajua mambo mengine walikufikisha wapi kama nchi?
 

Alipenda kusema vile ili kupata public sympathy ni dalili ya mtu muoga ambae hajiamini jinsi anavyotekeleza wajibu wake. Anachokisema Malcolm wachangiaji wengine hawajamuelewa na hawataki kutulia kusoma ili waelewe. Kwe lugha nyepesi "diplomasia" ni upatanishi ambao unaanzia ndani mpaka nje ya mipaka ya nchi na ndio msingi wa uhusiano wa kimataifa. Kwenye anga za diplomasia sisi tulikuwa vizuri Sana kwa sababu kwanza Umoja wetu wakitaifa ulikuwa imara na pili tuliweza kushirikiana vizuri na nchi zingine kwenye mambo mbalimbali hata kutatua migogoro.

Tanzania tulikuwa vinara kwenye upatanishi (diplomasia) tuliweza kusimamia maridhiano ya Burundi, Kenya hata kuleta amani kwenye visiwa vya anjuani kumuondoa kanali Bakari. Kwenye biashara zakimataifa tulikuwa vizuri sana tuliweza kufanya biashara ya mazao na malighafi zetu vizuri japo changamoto hazikosi. Mwaka 2012 dola ya marekani ilikuwa sawa na 1500 ya Tanzania nchi ilikuwa na hela ndio maana Kikwete aliajiri Sana, alipandisha madaraja kila mwaka watumishi wa umma waliweza kujenga nchi ilifunguka watu waliuza mpaka mbaazi nje kwa bei nzuri. Tatizo JPM alikuwa mshamba na Muoga sana kujivisha uzalendo wa hovyo aliamini kwenye mabarabara akasahau umoja wa kitaifa na upatanishi wakimataifa
 
Mambo mengine kama yapi?

Hao waliokuwa wanajua mambo mengine walikufikisha wapi kama nchi?
Wewe unaona umefika wapi kama nchi, acha kuwa mjinga basi Taifa lolote duniani ni kama mtoto anakuwa taratibu, Nyerere alipoishia mwinyi alianzia pale. JPM hakuwa malaika alifanya fyongo tu na wala nchi haijafika popote. Sema niwatanzania Wangapi wamekuwa lifted from poverty line. Uongozi wenye makelele mengi ya propaganda kutumia media bias matokeo yake ndio haya, nchi yetu imetoka mbali sana kama hujui tunu yetu kubwa tangu Taifa hili linazaliwa ni (diplomasia) upatinishi ndio Taifa kama msumbiji linatueshimu Sana. Jiulize kwanini mkapa aliwekeza sana kwenye jeshi, Sisi tulikuwa tunauwezo wakuchezea majirani tunavyotaka hata Rais nkrunzinza wa Burundi tuna mkono wetu kwa hiyo ilikuwa rahisi kuingiza chumvi yetu ya uvinza kutoka kigoma, tulienda Congo kumfurusha Kagame maana hao niwatoto wetu, mseveni wa uganga alikuwa hawezi kujamba mbale yetu tunachapa kiboko. Acha ushamba wewe, ulishafika udom ukaona uwekezaji wa serikalii, chuo Nelson Mandela, hospital ya mloganzira na Benjamin mkapa. Najua bado mtoto ukikua utaacha ujinga nchi iliingia mkosi kupata Rais mjinga
 
A good read
 
Sasa mjomba ni kweli huwezi endelea bila kujihusisha na dunia sija bisha lakini mm nimekwambia unabidii uanze kujenga kwanza ndani ndiyo ufwate hivi hukuona like jambo la kwenda uchumi wa kati lingeleta tija Katika uwekezaji. By the way magufuli hatunaye Tena Sasa turudi kwa waliopo Sasa hivi unadhani viongozi wanavyo zunguka ni kuijenga uhusiano wa dunia ni kuleta tija mtu unazunguka nchi za watu kwako umeme ni shida, maji ni shida hafu utaleta uwekezaji ni mwekezaji chizi pekee atakae wekeza kwa ajili ya hasara. Yaani beberu yeye ni mtu wa 1 profit, 2 profit,3 profit huwezi enda na pua yako kwa beberu akategemea kuwini. Hivi hujawahi ishi na mtu kakuzidi kiuchumi mbali lakini akakuheshimu kwa jambo moja ambalo ni dogo kwakuwa yeye haliwezi. Ndio hivyo Tanzania inabidii sisi tutambue nini tunaweza na Nini hatuwezi kile tuchoweza tunakifanya ambavyo hatuviwezi tunashirikiana na wengine hichi ndio ambacho jpm aliweza kutaka mtanzani afikiri anaweza. Sasa kuzunguka zunguka kwa kuomba misaada na kuona Kama wananchi ni visiki hatuwezi chochote.
 
I couldn't agree more mkuu!:
 
Hayo yote yamefanyika kwasababu ya nchi kua na viongozi wabovu.Na kwavile Ccm ndo chama kilichoongoza nchi toka uhuru huwezi kutenganisha ccm na huo ujinga wakutoa madini na kupewa condoms.Kwahiyo tatizo ni sisi wenyewe.Unapokubali kudanganywa na kuibiwa tatizo ni wewe sio muibaji,tena hawaibi bali tunawapa kupitia mikataba tunayosaini wenyewe chumbani.
 
Hao uliowataja ndo waliofikisha hii nchi kua ovyo hivi ilivyo.hakuna kitu humo.
 
Kipi kinamfanya au kumzuia mwafrika asijitambue badala yake amebaki kulia lia huku akiwa maskini?
 
Kwa hiyo mkataba hata kama ni mbovu wa kinyonyaji unatakiwa kuchekelea tu? Ndio diplomacy hiyo?

Kwani dhalimu alifanya nini, au zile brainwash za kwenye TV ndio uliona kapatia? Zile $192 alizoongopa tunawadai Barrick mlilipwa. Kile kushika uchumba cha $300m kimeshalipwa chote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…