JK bado ana kura yangu ya kumfikisha 2015
JK bado ana kura yangu ya kumfikisha 2015
Mimi mpaka leo sielewi kwa nini watu walipagawishwa na Kikwete. Tokea hata kabla hajatangaza nia yake ya kuwa raisi mimi nilijua hafai, hafai, na hafai kabisa. I'm glad I saw this before the get go. Nilibishana sana na watu mpaka nikaonwa mimi ni "hater". Oh well, what else can I say.....Miafrika Ndivyo Tulivyo....
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.
Kibunango,
Inanikumbusha historia ya kabila la Waganda - kama katika pitapita yake, Kabaka akimtamani mkeo basi inakuwa sifa isiyo kifani. Kinachofuatia ni wewe kumsindikiza mwandani wako kwa Kabaka na kumkabidhi kwa vifijo na vigelegele.
Inahuzunisha lakini ni kweli kuwa hata shetani hakosi wafuasi ambao wako tayari kuongozana naye hadi motoni. Lakini katika hili mtapambana tu na sisi ambao tumeamua kuwa huu uozo tulio nao lazima tuuzike tuondokane na harufu ya uvundo. Vipi wewe mwenzetu, mmmh !!!
Kwa style yao ya kuiba kura na kununua kura kama kawaida
Kitila, kwa kweli baada ya kusikilia hotuba hii umenifanya niwe upande wako; Kawaida yangu siyo kwenye siasa tu lakini hata katika maisha ya kawaida napenda kuamini kuwa wanadamu ukiwapa nafasi ya kufanya wema watafanya wema; Nimejifunza kumpa mtu nafasi ya kukosea na kujisahihisha. Nimejifunza kutokuwa na hukumu kali sana kwa mwanadamu mwingine.
Lakini katika hilo pia nimejifunza kuwa kuna mipaka isiyovukwa na kuna mambo ambayo mtu hatakiwi kupewa nafasi ya pili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini kuwa somehow Kikwete atajikuta anakaa peke yake na kujikuta yuko peke (alone and lonely) na kutambua uzito alionao wa kuliongoza Taifa. Nimekuwa nikitumaini na kuombea kuwa Kikwete atatambua wajibu wake mkubwa na kuamua kufanya kile ambacho viongozi wa kweli hufanya.
Hivyo mara kadhaa (wakati Baraza limevunjika) niliamini kuwa JK atasimama na kuuteka wakati na hivyo kuanza upya; haikutokea hivyo. HIvyo hotuba hii jinsi ilivyopambwa na kutokea kwake wakati na saa kama hii niliamini kuwa labda amejifunza kitu na sasa yuko kweli anataka kufanya kitu; nilikuwa nimekosea.
Kikwete hawezi kuongoza; Kikwete si kiongozi ni mwanasiasa mpiga porojo; Kikwete si kiongozi ambaye Watanzania walitarajia kuwaongoza kutoka kwenye kilindi cha umasikini kuelekea kwenye mafuriko ya mafanikio. Rais Kikwete na niliandika wiki mbili zilizopita ni mtu ambaye amepewa nafasi nyingine kufunga goli ambapo amebakia yeye na golipa na mara zote amekuwa akifika golini anabakia kukaa chini na kusubiri mtu mwingine aje ampasia afunge goli wakati mashabiki wamekaa pembeni wakishangalia na kuombea afunge kwa sababu ni Kapteni wa timu na alinunuliwa kwa bei kubwa.
Unaposhinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 80 unaweza kabisa kusababisha mabadiliko makubwa ya Kitaifa na kuongoza Taifa. Unapopata support ya watu wa mjini na kijijini, maskini na matajiri unakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ambapo ni wewe tu unajua ukiuwekeza vizuri utalipa. Lakini kwa kushindwa mikakati, kugwaya, kuogopa kuudhi watu n.k unabakia na mtaji huo ambao pole pole unazidi kumemenyuka.
Kikwete ni kilele cha kukatisha tamaa na mfano dhahiri wa nini kiongozi asiwe. Kikwete anasimama leo hii kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza na anabakia kuitwa kiongozi. Rais Kikwete amebakia kuwa yule mwenye "simba wa kuchora" ambaye anasimama kuunguruma kwenye picha na watoto wanabakia kucheka.
Leo kwa hakika ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Rais Kikwete kuonesha uongozi Tanzania badala ya kupiga zogo. Kama alitaka kuelezea hali ya Muungano wetu na ya Taifa yetu alikuwa na wakati mzuri pale Aprili 26, Mei Mosi, Nane Nane n.k au kila mwanzoni mwa mwaka kama wanavyofanya Wamarekani. Lakini hili la kuiweka roho juu nchi na kwenda na magwaride na uongozi mzima wa serikali kwenye hotuba maalumu ya Rais Bungeni ni kuchezea hisia za wananchi. Ni kutuzuga kulikotukuka ambako kwa hakika kunamfanya astahili kupewa nishani iya Uzugaji uliotukuka daraja la kwanza na la pili!
Rais anapoenda kuzungumza Bungeni iwe kwa kweli jambo muhimu, zito, na ambalo kwa hakika linastahili mahali kama hapo. Kusimamisha shughuli za Bunge ili uje upigiwe makofi na saluti wakati mijadala muhimu ya Taifa inaendelea ni kuwapotezea muda wananchi na wabunge. Hotuba yake jinsi alivyoitoa ingeweza kutolewa na Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au hata Salva Rweyemamu! Haikuwa hotuba inayoendana na Urais kwani kwenye suala muhimu la Muungano alitakiwa kutoa msimamo badala ya "kuwaomba" viongozi wenzake.
Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.
So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.
I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!
Mwanakijiji,
Msimamo wako unajulikana kabla na hata baada ya Hotuba, kujifanya sasa ndio ume-make mind ni uongo mkubwa!
Anyway mwaka 2005 Kikwete alikosa 20% ya kura za Watanzania na hizi zitakuwa pamoja za ya kwako... kama at least utaweza piga kura 2010...
Lakini ukweli ni kwamba your mission is well known.
Kikwete anaweza kupata kura kwa sababu ya kuongea lugha Rais ambayo wananchi wanamwelewa wakati ninyi mnataka technical language kama ya Mkapa ambayo wananchi walikuwa hawamuelewi.
Tuendelee kujenga taifa na difference za Mawazo ambazo Kikwete anaziheshimu.
La maana katika kujadili matatizo ya ndoa yetu ni kusema kuwa kwanza ndoa ipo na halali; kwamba Muungano upo na halali. Na la pili ni kukubali ‘on principle' and in fact kuwa zile nchi mbili zilizoungana hazipo tena (siyo kuwa moja ipo nyingine haipo) na kilichopo ni nchi moja. Ni kutoka hapo ndipo mjadala wa kero za Muungano unaweza kufanyika. Hili la kusema ati mmoja bado ni nchi na mwingine siyo nchi ni kuzugana.
Mwanakijiji...Anyway mwaka 2005 Kikwete alikosa 20% ya kura za Watanzania na hizi zitakuwa pamoja za ya kwako... kama at least utaweza piga kura 2010...
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF ............ Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF.
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.~~ Mzee Mwanakijiji
Mkulu MMJ,
Naona kama ulikuwepo kichwani mwangu, maneno mazito sana haya na mimi nimeamua kuyatafakari kwa makini sana.
Kilichotokea leo ni heart breaking, ninafikiria kukuunga mkono na mapumziko ya muda, kama sio permanent! Kwa kweli inauma sana.
Let's take action, please! I mean, ACTION. Maneno matupu hayatupeleki popote waungwana! It would be a brilliant move kama tungeanzisha some sort of movement fulani ili kutia-presssure/hakikisha kwamba wale wote wanaohusishwa na ufisadi hawaingii/rudi tena kwenye system. For instance, let say Karamagi ni Fisadi kweli. Then, movement ichange pesa, itafute alternative figure, kisha ground work ifanywe [kufa na kupona] kuhakikisha kuwa Karamagi harudi tena bungeni. It's that simple wananchi. I mean, Tarime wanaweza wakatufundisha hizo mbinu maana nasikia kulikuwa na jamaa mmoja anaitwa Kisyeri Werema Chambiri (former MP, Tarime) ambaye alikuwa amelewa madaraka na kuanza tabia mbya ya kutukana wananchi waliomchagua akisema, "mpenda msipenda mimi nitakuwa mbuge wa Tarime forever." Oh, shit! Watu wakaji-organize, wakaanzisha a sort of movemet aimed kumung'oa Chambiri. Nasikia siku ya uchaguzi, hata baada ya kuwa wamemaliza kupiga kura, people hazikuondoka vituoni! Walipiga kambi nje ya vituo vya kura mpaka, kura zikahesabibwa, hadi kikaeleweka! Matokeo yake: Wakampeleka "mpiganaji Wagwe" Dodoma. Hivyo ndivyo tutakavyobadili nchini. Lakini hili la kushindana kuona nani ana type fast hapa JF, halitupeliki popote kabisa.
I'm glad Mwanakijiji ameamua ku-embrace/adopt philosophy like "Cheche Za Fikra." I'm very willing kuungana naye ili tuwaelimishe watanzania wengi [hususani walioko vijijini, ambao ndio watakaoirudisha CCM madarakani tena 2010]kuhusu wapi nchi yao ilipo, na wapi nchi yao inaweza ikafika endapo kama watafanya maamuzi ya busara mwaka 2010. Coz hii approach ya ku-debate tu hapa JF (bila kuchukua action yeyote) ime-prove kuwa haitatupeleka popote kabisa. Mfano mzuri, ni jinsi Kikwete alivyoamua kuichekesha dunia leo
Nadhani anastahili kipindi cha pili and i think even the third term.kwa sababu hamna kosa analolifanya.Amefanya mengi mazuri ya maendeleo only blind man cannot see.And those who have hatred against CHama CHA MAPINDUZI. Lakini hata hao wapinzani wakipewa uongozi wana fanya nini la maana.Kwa sababu hadi sasa sera zao ni wasiwasi hakuna lolote walilo advocate.ambalo utaona hawa jama wako serious exept for individual person like ZITO and Dr SLAA ,HAMAD RASHID ambao upinzani wao ni wa kujenga nchi.Lakini wengi kama baadhi ya wana JF hamna kitu ni kupinga bila kutoa mawazo yako .ni kutoa kashfa za kwenye vijiwe vya kahawa tuu.
MKJJ....!
Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!
Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!
MKJJ....!
Nakubaliana na mawazo yako lakini naomba ujaribu kuangalia na upande mwingine wa shilingi....!
Hivi umeshawahi kujiuliza kazi za Raisi ni nini haswa? Naomba usome katiba ya Jamhuri wa Muungano ndo utajua kazi za Rais....! Kazi za Raisi sio za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya Rais ni usimamizi wa serikali pamoja na kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa...!
Aidha, kuongoza nchi sio kama kuongoza kampuni ambapo unaweza ukatoa amri asubuhi na ikatekelezwa hapo hapo...! Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!
Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!
Pia Unapokua raisi changamoto ni nyingi sana na mambo ni mengi sana tena kwa wakati mmoja....! Jaribu kufukiria kwamba unakua Raisi halafu kuna wizara 22 (Mambo ya ndani, maji, mifugo, sheria na katiba, elimu, afaya, fedha, mambo ya nje, miundombinu, sayansi etc) ziko chini yako na kila moja inamatatizo makubwa ya kutolea maamuzi tena maamuzi mzito, usipokua makini, ndio hivyo unaweza ukaishia kuwa dictecta kwa sababu utataka kufanya maamuzi ambayo utataka kuona matokeo yake mara moja...!
Kwa mfano, mimi nilimuelewa sana Kikwete alipozungumzia suala la kiwafukuza kazi wale walihusika kwenye EPA, embu chukulia kama Kikwete angekua na hasira/maamuzi ya haraka haraka akamua kuwafukuza kazi wale wote waliotajwa kule ndani, sio kwamba angwafaidisha kwani wangeenda kufungua kesi kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria?
Mimi naomba uwe unajaribu kujiweka kwenye viatu vya Kikwete na sio ku-mcritisize tu, jaribu kuchuukulia kama wewe ungekua Rais je ungekutwa na changamoto kama anazokumbana nazo wewe ungekua unafanya nini au ugeamuaje?
Pia jaribu kuangallia kwamba tanzania ni nchi changa, nilikua nasoma takwimu za taifa jana, nikaona kwamba kati ya watu milioni 38.9 tuliopo tanzania, ni wananchi laki nne tu wenye digree moja...! Hizi takwimu zilikua zinafanya estimate kwamba tokea uhuru watu waliograduate unversity walikua ni watu 7,000 kila mwaka, ukizidisha 7,000X mara miaka 44 ya uhuru utapata jibu kamili...!
Sasa hebu asuume wewe ndio Rais unayeongoza taifa la namna hio, ambalo sehemu kubwa ya wananchi hawana elimu, wewe ungekua unafanyaje?
Tatizo lako ni kwamba unajaribu kulinganisha Tanzania na Marekani au na Uingereza, lakini umejuiliza Marekani au Uingereza inawasomi kiasi gani? au Ilipata lini uhuru?
Pia, usilaumu tu ukiwa huko nje ya nchi, njooo huku tanzania uje uijenge nchi yako, usiishie kujenga nchi za watu halafu uishie kulaumu nchi yako na viongozi wako....!
Pia, usisahau kwamba ROME WAS NOT BUILD IN ONE DAY
, tusifikiri tutaweza kulala na kuamka tukakuta kesho tanzania imebadilika, kama sisi wananchi wenyewe hatuwezi kubadilika suitegemee hata tungeletewa malaika kutoka mbinguni nchi yetu itabadilika....! Hayo ni maoni yangu mbadala tu....!