MKJJ....!
Nakubaliana na mawazo yako lakini naomba ujaribu kuangalia na upande mwingine wa shilingi....!
Hivi umeshawahi kujiuliza kazi za Raisi ni nini haswa? Naomba usome katiba ya Jamhuri wa Muungano ndo utajua kazi za Rais....! Kazi za Raisi sio za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya Rais ni usimamizi wa serikali pamoja na kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa...!
Aidha, kuongoza nchi sio kama kuongoza kampuni ambapo unaweza ukatoa amri asubuhi na ikatekelezwa hapo hapo...! Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!
Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!
Pia Unapokua raisi changamoto ni nyingi sana na mambo ni mengi sana tena kwa wakati mmoja....! Jaribu kufukiria kwamba unakua Raisi halafu kuna wizara 22 (Mambo ya ndani, maji, mifugo, sheria na katiba, elimu, afaya, fedha, mambo ya nje, miundombinu, sayansi etc) ziko chini yako na kila moja inamatatizo makubwa ya kutolea maamuzi tena maamuzi mzito, usipokua makini, ndio hivyo unaweza ukaishia kuwa dictecta kwa sababu utataka kufanya maamuzi ambayo utataka kuona matokeo yake mara moja...!
Kwa mfano, mimi nilimuelewa sana Kikwete alipozungumzia suala la kiwafukuza kazi wale walihusika kwenye EPA, embu chukulia kama Kikwete angekua na hasira/maamuzi ya haraka haraka akamua kuwafukuza kazi wale wote waliotajwa kule ndani, sio kwamba angwafaidisha kwani wangeenda kufungua kesi kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria?
Mimi naomba uwe unajaribu kujiweka kwenye viatu vya Kikwete na sio ku-mcritisize tu, jaribu kuchuukulia kama wewe ungekua Rais je ungekutwa na changamoto kama anazokumbana nazo wewe ungekua unafanya nini au ugeamuaje? Pia jaribu kuangallia kwamba tanzania ni nchi changa, nilikua nasoma takwimu za taifa jana, nikaona kwamba kati ya watu milioni 38.9 tuliopo tanzania, ni wananchi laki nne tu wenye digree moja...! Hizi takwimu zilikua zinafanya estimate kwamba tokea uhuru watu waliograduate unversity walikua ni watu 7,000 kila mwaka, ukizidisha 7,000X mara miaka 44 ya uhuru utapata jibu kamili...!
Sasa hebu asuume wewe ndio Rais unayeongoza taifa la namna hio, ambalo sehemu kubwa ya wananchi hawana elimu, wewe ungekua unafanyaje?
Tatizo lako ni kwamba unajaribu kulinganisha Tanzania na Marekani au na Uingereza, lakini umejuiliza Marekani au Uingereza inawasomi kiasi gani? au Ilipata lini uhuru? Pia, usilaumu tu ukiwa huko nje ya nchi, njooo huku tanzania uje uijenge nchi yako, usiishie kujenga nchi za watu halafu uishie kulaumu nchi yako na viongozi wako....!
Pia, usisahau kwamba ROME WAS NOT BUILD IN ONE DAY, tusifikiri tutaweza kulala na kuamka tukakuta kesho tanzania imebadilika, kama sisi wananchi wenyewe hatuwezi kubadilika suitegemee hata tungeletewa malaika kutoka mbinguni nchi yetu itabadilika....! Hayo ni maoni yangu mbadala tu....!