Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

JK bado ana kura yangu ya kumfikisha 2015

Kibunango,

Inanikumbusha historia ya kabila la Waganda - kama katika pitapita yake, Kabaka akimtamani mkeo basi inakuwa sifa isiyo kifani. Kinachofuatia ni wewe kumsindikiza mwandani wako kwa Kabaka na kumkabidhi kwa vifijo na vigelegele.

Inahuzunisha lakini ni kweli kuwa hata shetani hakosi wafuasi ambao wako tayari kuongozana naye hadi motoni. Lakini katika hili mtapambana tu na sisi ambao tumeamua kuwa huu uozo tulio nao lazima tuuzike tuondokane na harufu ya uvundo. Vipi wewe mwenzetu, mmmh !!!
 
Jamani post yangu ya elfu 2 hii nisingependa kuiandika hivi.

Mwanakijiji achana na hizo bado tunakuhitaji hapa Tanzania na mchango wako. Askari gani wewe unaeacha kupigana vita kwa ajili ya kamanda mmoja kuwa sio mshupavu?, kumbuka unapigania NCHI na sio KAMANDA.

Nchi sio kamanda, wananchi wa kijijini wanakuhitaji sana.

Baada ya hayo naomba hii hoja/topic iwe merged na Hotuba ya rais ili tupate muendelezo mzuri!
 
Mimi mpaka leo sielewi kwa nini watu walipagawishwa na Kikwete. Tokea hata kabla hajatangaza nia yake ya kuwa raisi mimi nilijua hafai, hafai, na hafai kabisa. I'm glad I saw this before the get go. Nilibishana sana na watu mpaka nikaonwa mimi ni "hater". Oh well, what else can I say.....Miafrika Ndivyo Tulivyo....

The same for me....nilikuwa nawauliza mashabiki wake ni kipi kinachowafanya muone Kikwete ni bora kuliko wengine wote, ni zipi rekodi zake za ufanyaji kazi ambazo zinawafanya watu muweweseke kiasi hicho
 
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

Good point Mwanakijiji. You know, I hardly ever agree with you most of the time, but today, I have nothing to disagree with you, but rather to tip my hat to you, sir.

I'm very impressed by the fact that finally you have decided to move back to my original position. Action, action, action.

Unajua kila siku nimekuwa nasema the same thing hapa JF lakini watu wamekuwa wakiniona as if nimedata. Let's take action, please! ACTION. Maneno matupu hayatupeleki popote waungwana! It would be a brilliant move kama tungeanzisha some sort of movement fulani ili kutia-presssure/hakikisha kwamba wale wote wanaohusishwa na ufisadi hawaingii/rudi tena kwenye system. For instance, let say Karamagi ni Fisadi kweli. Then, movement ichange pesa, itafute alternative figure, kisha ground work ifanywe [kufa na kupona] kuhakikisha kuwa Karamagi harudi tena bungeni. It's that simple wananchi. I mean, Tarime wanaweza wakatufundisha hizo mbinu maana nasikia kulikuwa na jamaa mmoja anaitwa Kisyeri Werema Chambiri (former MP, Tarime) ambaye alikuwa amelewa madaraka na kuanza tabia mbya ya kutukana wananchi waliomchagua akisema, "mpenda msipenda mimi nitakuwa mbuge wa Tarime forever." Oh, shit! Watu wakaji-organize, wakaanzisha a sort of movemet aimed kumung'oa Chambiri. Nasikia siku ya uchaguzi, hata baada ya kuwa wamemaliza kupiga kura, people hazikuondoka vituoni! Walipiga kambi nje ya vituo vya kura mpaka, kura zikahesabibwa, hadi kikaeleweka! Matokeo yake: Wakampeleka "mpiganaji Wagwe" Dodoma. Hivyo ndivyo tutakavyobadili nchini. Lakini hili la kushindana kuona nani ana type fast hapa JF, halitupeliki popote kabisa.

I'm glad umeanza na hilo la "Cheche Za Fikra." I'm very willing kuungana na wewe ili tuwaelimishe watanzania wengi [hususani walioko vijijini] kuhusu wapi nchi yao ilipo, na wapi nchi yao inaweza ikafika endapo kama watafanya maamuzi ya busara mwaka 2010.
 
Kibunango,

Inanikumbusha historia ya kabila la Waganda - kama katika pitapita yake, Kabaka akimtamani mkeo basi inakuwa sifa isiyo kifani. Kinachofuatia ni wewe kumsindikiza mwandani wako kwa Kabaka na kumkabidhi kwa vifijo na vigelegele.

Inahuzunisha lakini ni kweli kuwa hata shetani hakosi wafuasi ambao wako tayari kuongozana naye hadi motoni. Lakini katika hili mtapambana tu na sisi ambao tumeamua kuwa huu uozo tulio nao lazima tuuzike tuondokane na harufu ya uvundo. Vipi wewe mwenzetu, mmmh !!!

Kabla hajampiga fito mwandani wangu itabidi aruke maiti yangu kwanza.
Ni afadhari kufa kuliko kuishi kwa fedheha ya aina yeyote ile.

Enzi zile mababu zetu waliuza nchi kwa kupewa shanga za kuvaa viunoni mwao.
Nilidhani hilo la shanga liliishia zama hizo za kale kumbe si kweli.
vilembwe na vining'ina vyao waishi karne ya 21 akina Chenge Mkapa Lowassa na Kikwete bado wanaendelea tabia hiyo ya kuhongwa shanga na wanaume wa kizungu ili wao na wake zao watukoge wazivaapo viunoni na shingoni mwao.
Vishangingi na vijisenti kaa vile vya Chenge vikilinganishwa na mwanya wautoao kwa wawekezaji kujichotea mali toka Tanzania, thamani yake ni sawa kabisa na shanga zile za enzi ya Karl Peters.

Kibaya zaidi kuna wenzetu wengi humu JF na kila kona ya Tanzania wanazitamani sana shanga hizo katika viuno vya nilio wataja kiasi kwamba wako tayari kujifedhehesha kwa kila hali ili tu waonekane wako karibu sana na wavaa shanga mbumbumbu hawa wa karne ya 21.
 
Kwa kweli huyu tunayemwita Rais mimi siko tayari kumwita hivyo.
Amepoteza muda wa watanzania wengi kumbe anakuja kuongea utumbo mtupu.
Anastahili kuadhibiwa huyu kwa sababu ame prove failure.
Porojo kuongoza taifa.Thats why he dont know Tanzania the reason of Tanzania being poor.
 
Kwa style yao ya kuiba kura na kununua kura kama kawaida

Nadhani anastahili kipindi cha pili and i think even the third term.kwa sababu hamna kosa analolifanya.Amefanya mengi mazuri ya maendeleo only blind man cannot see.And those who have hatred against CHama CHA MAPINDUZI. Lakini hata hao wapinzani wakipewa uongozi wana fanya nini la maana.Kwa sababu hadi sasa sera zao ni wasiwasi hakuna lolote walilo advocate.ambalo utaona hawa jama wako serious exept for individual person like ZITO and Dr SLAA ,HAMAD RASHID ambao upinzani wao ni wa kujenga nchi.Lakini wengi kama baadhi ya wana JF hamna kitu ni kupinga bila kutoa mawazo yako .ni kutoa kashfa za kwenye vijiwe vya kahawa tuu.
 
Kitila, kwa kweli baada ya kusikilia hotuba hii umenifanya niwe upande wako; Kawaida yangu siyo kwenye siasa tu lakini hata katika maisha ya kawaida napenda kuamini kuwa wanadamu ukiwapa nafasi ya kufanya wema watafanya wema; Nimejifunza kumpa mtu nafasi ya kukosea na kujisahihisha. Nimejifunza kutokuwa na hukumu kali sana kwa mwanadamu mwingine.

Lakini katika hilo pia nimejifunza kuwa kuna mipaka isiyovukwa na kuna mambo ambayo mtu hatakiwi kupewa nafasi ya pili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini kuwa somehow Kikwete atajikuta anakaa peke yake na kujikuta yuko peke (alone and lonely) na kutambua uzito alionao wa kuliongoza Taifa. Nimekuwa nikitumaini na kuombea kuwa Kikwete atatambua wajibu wake mkubwa na kuamua kufanya kile ambacho viongozi wa kweli hufanya.

Hivyo mara kadhaa (wakati Baraza limevunjika) niliamini kuwa JK atasimama na kuuteka wakati na hivyo kuanza upya; haikutokea hivyo. HIvyo hotuba hii jinsi ilivyopambwa na kutokea kwake wakati na saa kama hii niliamini kuwa labda amejifunza kitu na sasa yuko kweli anataka kufanya kitu; nilikuwa nimekosea.

Kikwete hawezi kuongoza; Kikwete si kiongozi ni mwanasiasa mpiga porojo; Kikwete si kiongozi ambaye Watanzania walitarajia kuwaongoza kutoka kwenye kilindi cha umasikini kuelekea kwenye mafuriko ya mafanikio. Rais Kikwete na niliandika wiki mbili zilizopita ni mtu ambaye amepewa nafasi nyingine kufunga goli ambapo amebakia yeye na golipa na mara zote amekuwa akifika golini anabakia kukaa chini na kusubiri mtu mwingine aje ampasia afunge goli wakati mashabiki wamekaa pembeni wakishangalia na kuombea afunge kwa sababu ni Kapteni wa timu na alinunuliwa kwa bei kubwa.

Unaposhinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 80 unaweza kabisa kusababisha mabadiliko makubwa ya Kitaifa na kuongoza Taifa. Unapopata support ya watu wa mjini na kijijini, maskini na matajiri unakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ambapo ni wewe tu unajua ukiuwekeza vizuri utalipa. Lakini kwa kushindwa mikakati, kugwaya, kuogopa kuudhi watu n.k unabakia na mtaji huo ambao pole pole unazidi kumemenyuka.

Kikwete ni kilele cha kukatisha tamaa na mfano dhahiri wa nini kiongozi asiwe. Kikwete anasimama leo hii kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza na anabakia kuitwa kiongozi. Rais Kikwete amebakia kuwa yule mwenye "simba wa kuchora" ambaye anasimama kuunguruma kwenye picha na watoto wanabakia kucheka.

Leo kwa hakika ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Rais Kikwete kuonesha uongozi Tanzania badala ya kupiga zogo. Kama alitaka kuelezea hali ya Muungano wetu na ya Taifa yetu alikuwa na wakati mzuri pale Aprili 26, Mei Mosi, Nane Nane n.k au kila mwanzoni mwa mwaka kama wanavyofanya Wamarekani. Lakini hili la kuiweka roho juu nchi na kwenda na magwaride na uongozi mzima wa serikali kwenye hotuba maalumu ya Rais Bungeni ni kuchezea hisia za wananchi. Ni kutuzuga kulikotukuka ambako kwa hakika kunamfanya astahili kupewa nishani iya Uzugaji uliotukuka daraja la kwanza na la pili!

Rais anapoenda kuzungumza Bungeni iwe kwa kweli jambo muhimu, zito, na ambalo kwa hakika linastahili mahali kama hapo. Kusimamisha shughuli za Bunge ili uje upigiwe makofi na saluti wakati mijadala muhimu ya Taifa inaendelea ni kuwapotezea muda wananchi na wabunge. Hotuba yake jinsi alivyoitoa ingeweza kutolewa na Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au hata Salva Rweyemamu! Haikuwa hotuba inayoendana na Urais kwani kwenye suala muhimu la Muungano alitakiwa kutoa msimamo badala ya "kuwaomba" viongozi wenzake.

Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.

Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.

I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!

Mkuu tuko pamoja kwa hili,
Wengi tumeingiwa na huzuni kuu baada ya kusikiliza hotuba hii.Naamini kabisa kuwa kama viongozi wetu watabaki kuwa kama akina Kikwete basi nchi yetu itaendelea kuwa masikini daima na wananchi wake wataendelea kuwa masikini milele.
Ningeomba JF tuweke siku ya maombolezo!! tunahitaji njia mbadala hapa.Tunahitaji kuzicharge fikra zetu na kuzipa akili zetu faragha na amani moyoni kabla ya kuanzisha mapinduzi makuu na matakatifu!

Huku kwetu Ukraine wananchi waliamua kuingia mitaani na kudai haki zao.Ni mfano tosha kabisa ambao unahitajika kwa sasa katika nchi yetu.
Hivyo walizishinda ndimi za uoga,walikubali kukaa kwenye baridi usiku kucha! bila ya usingizi pale Independence square in Kiev na kudai haki zao mpaka pale walipozipata.

Haya machache tu ndiyo yaliyosemwa na "Yushchenko" naomba kunukuu.....

" "Ukraine is on the brink of a civil conflict," Mr Yushchenko warned. "We have two choices: either the answer will be given by the parliament, or the streets will give an answer."

One hand pressed against a 300-year-old Bible, and the other raised above his head Mr Yushchenko first sang the national anthem, then read the oath of office before opening a window and speaking to supporters outside. He said that Ukraine could be engulfed by unrest if the will of the people was not obeyed. As his voice - relayed by loudspeakers - boomed across the square, the crowd roared back its answer: "Yushchenko, Yushchenko!"
Mr Yushchenko later reappeared in the vast Independence Square, urging the crowds to disregard the cold, stay out overnight and guard the tent city that has sprung up on Kiev's main street.

"What we started today must be defended every day," he said. "We urge you to come to the square in the same numbers. Tomorrow you will be especially needed for the country."


-Wembe.
 
Mwanakijiji,

Msimamo wako unajulikana kabla na hata baada ya Hotuba, kujifanya sasa ndio ume-make mind ni uongo mkubwa!

Anyway mwaka 2005 Kikwete alikosa 20% ya kura za Watanzania na hizi zitakuwa pamoja za ya kwako... kama at least utaweza piga kura 2010...

Lakini ukweli ni kwamba your mission is well known.

Kikwete anaweza kupata kura kwa sababu ya kuongea lugha Rais ambayo wananchi wanamwelewa wakati ninyi mnataka technical language kama ya Mkapa ambayo wananchi walikuwa hawamuelewi.

Tuendelee kujenga taifa na difference za Mawazo ambazo Kikwete anaziheshimu.
 
Mwanakijiji,

Msimamo wako unajulikana kabla na hata baada ya Hotuba, kujifanya sasa ndio ume-make mind ni uongo mkubwa!

Kasheshe hujui msimamo wangu mimi. Unajua what you think you know.. msimamo wangu mimi naujua mimi na nafsi yangu. Kwa hiiyo ni uongo usio kifani kudai kuwa unajua msimamo wangu kwa kusoma ninachoandika. Huna uwezo huo, huwezi kuwa na uwezo huo na na kamwe hautakuwa na uwezo huo hata kama unaota unao.

Anyway mwaka 2005 Kikwete alikosa 20% ya kura za Watanzania na hizi zitakuwa pamoja za ya kwako... kama at least utaweza piga kura 2010...

Wrong, alipata kura yangu. na mwaka 2010 God willing hatachaguliwa tena au hatakuwa na Bunge alilonalo sasa (I prefer the later).

Lakini ukweli ni kwamba your mission is well known.

By who? My mission is not well know but speculated by people like you. My mission is mine and mine alone. You have no idea what it is.
Kikwete anaweza kupata kura kwa sababu ya kuongea lugha Rais ambayo wananchi wanamwelewa wakati ninyi mnataka technical language kama ya Mkapa ambayo wananchi walikuwa hawamuelewi.

Wrong, nina uwezo wa kuandika lugha technical, katika maandishi yangu hakuna lugha technical; lugha yangu ni ile inatumiwa na mtu wa kawaida kabisa.


Tuendelee kujenga taifa na difference za Mawazo ambazo Kikwete anaziheshimu.

Tofauti nyingine za mawazo siyo za kuziheshimu bali za kuzishinda; Ndio maana nilikataa kwenye makala ya jumatano kuwa suala la Zanzibar siyo tofauti ya kimawazo kama alivyosema yeye kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi. Na ni yeye aliyekubaliana na mimi zaidi leo kwenye hoja yangu kuhusu Zanzibar: Angalia nilichoandika Jumatano na alichosema Kikwete leo:

La maana katika kujadili matatizo ya ndoa yetu ni kusema kuwa kwanza ndoa ipo na halali; kwamba Muungano upo na halali. Na la pili ni kukubali ‘on principle' and in fact kuwa zile nchi mbili zilizoungana hazipo tena (siyo kuwa moja ipo nyingine haipo) na kilichopo ni nchi moja. Ni kutoka hapo ndipo mjadala wa kero za Muungano unaweza kufanyika. Hili la kusema ati mmoja bado ni nchi na mwingine siyo nchi ni kuzugana.

Nina interest kubwa zaidi na ninasukumwa na kitu ambacho siamini kama kinaweza kukuingia mawazoni. It is something greater and noble than ambition, desire or dreams for anyithing you might think. You need to be me to understand what I'm talking about. Otherwise, yours was very lame and futile attempt of psychonalyzing me. And your resistance to the power of my arguments is futile too!
 
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF ............ Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF.

Mkulu MMJ,

Naona kama ulikuwepo kichwani mwangu, maneno mazito sana haya na mimi nimeamua kuyatafakari kwa makini sana.

Kilichotokea leo ni heart breaking, ninafikiria kukuunga mkono na mapumziko ya muda, kama sio permanent! Kwa kweli inauma sana.
 
Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.~~ Mzee Mwanakijiji


Mkulu MMJ,

Naona kama ulikuwepo kichwani mwangu, maneno mazito sana haya na mimi nimeamua kuyatafakari kwa makini sana.

Kilichotokea leo ni heart breaking, ninafikiria kukuunga mkono na mapumziko ya muda, kama sio permanent! Kwa kweli inauma sana.

Mkuu Marshall, I couldn't agree with you more. Nimemwandikia reply kama hiyo Mwanakijiji [early today]. At least for now nimekuwa vindicated [na Kikwete] kwa kile nilichokuwa nikikisema sikuzote:

Let's take action, please! I mean, ACTION. Maneno matupu hayatupeleki popote waungwana! It would be a brilliant move kama tungeanzisha some sort of movement fulani ili kutia-presssure/hakikisha kwamba wale wote wanaohusishwa na ufisadi hawaingii/rudi tena kwenye system. For instance, let say Karamagi ni Fisadi kweli. Then, movement ichange pesa, itafute alternative figure, kisha ground work ifanywe [kufa na kupona] kuhakikisha kuwa Karamagi harudi tena bungeni. It's that simple wananchi. I mean, Tarime wanaweza wakatufundisha hizo mbinu maana nasikia kulikuwa na jamaa mmoja anaitwa Kisyeri Werema Chambiri (former MP, Tarime) ambaye alikuwa amelewa madaraka na kuanza tabia mbya ya kutukana wananchi waliomchagua akisema, "mpenda msipenda mimi nitakuwa mbuge wa Tarime forever." Oh, shit! Watu wakaji-organize, wakaanzisha a sort of movemet aimed kumung'oa Chambiri. Nasikia siku ya uchaguzi, hata baada ya kuwa wamemaliza kupiga kura, people hazikuondoka vituoni! Walipiga kambi nje ya vituo vya kura mpaka, kura zikahesabibwa, hadi kikaeleweka! Matokeo yake: Wakampeleka "mpiganaji Wagwe" Dodoma. Hivyo ndivyo tutakavyobadili nchini. Lakini hili la kushindana kuona nani ana type fast hapa JF, halitupeliki popote kabisa.

I'm glad Mwanakijiji ameamua ku-embrace/adopt philosophy like "Cheche Za Fikra." I'm very willing kuungana naye ili tuwaelimishe watanzania wengi [hususani walioko vijijini, ambao ndio watakaoirudisha CCM madarakani tena 2010]—kuhusu wapi nchi yao ilipo, na wapi nchi yao inaweza ikafika endapo kama watafanya maamuzi ya busara mwaka 2010. Coz hii approach ya ku-debate tu hapa JF (bila kuchukua action yeyote) ime-prove kuwa haitatupeleka popote kabisa. Mfano mzuri, ni jinsi Kikwete alivyoamua kuichekesha dunia leo
 
Nadhani anastahili kipindi cha pili and i think even the third term.kwa sababu hamna kosa analolifanya.Amefanya mengi mazuri ya maendeleo only blind man cannot see.And those who have hatred against CHama CHA MAPINDUZI. Lakini hata hao wapinzani wakipewa uongozi wana fanya nini la maana.Kwa sababu hadi sasa sera zao ni wasiwasi hakuna lolote walilo advocate.ambalo utaona hawa jama wako serious exept for individual person like ZITO and Dr SLAA ,HAMAD RASHID ambao upinzani wao ni wa kujenga nchi.Lakini wengi kama baadhi ya wana JF hamna kitu ni kupinga bila kutoa mawazo yako .ni kutoa kashfa za kwenye vijiwe vya kahawa tuu.

Hata Nyerere mwenyewe wazo la kupigania Uhuru wa Tanganyika alilitoa katika vijiwe vya kulonga huko UK enzi hizo.
Naamini kungekuwa na Internet yeye naye angekuwa Madela kabla hajawa Nyerere huko Ground Zero.
Wewe subiri tushuke huko Ground Zero, kama alivyonena Anne Kilango kule bungeni, patakuwa hapatoshi kabisa.
Ila msianze kulialia kwamba tuko backed up na CIA.
 
MKJJ....!

Nakubaliana na mawazo yako lakini naomba ujaribu kuangalia na upande mwingine wa shilingi....!

Hivi umeshawahi kujiuliza kazi za Raisi ni nini haswa? Naomba usome katiba ya Jamhuri wa Muungano ndo utajua kazi za Rais....! Kazi za Raisi sio za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya Rais ni usimamizi wa serikali pamoja na kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa...!

Aidha, kuongoza nchi sio kama kuongoza kampuni ambapo unaweza ukatoa amri asubuhi na ikatekelezwa hapo hapo...! Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!

Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!

Pia Unapokua raisi changamoto ni nyingi sana na mambo ni mengi sana tena kwa wakati mmoja....! Jaribu kufukiria kwamba unakua Raisi halafu kuna wizara 22 (Mambo ya ndani, maji, mifugo, sheria na katiba, elimu, afaya, fedha, mambo ya nje, miundombinu, sayansi etc) ziko chini yako na kila moja inamatatizo makubwa ya kutolea maamuzi tena maamuzi mzito, usipokua makini, ndio hivyo unaweza ukaishia kuwa dictecta kwa sababu utataka kufanya maamuzi ambayo utataka kuona matokeo yake mara moja...!

Kwa mfano, mimi nilimuelewa sana Kikwete alipozungumzia suala la kiwafukuza kazi wale walihusika kwenye EPA, embu chukulia kama Kikwete angekua na hasira/maamuzi ya haraka haraka akamua kuwafukuza kazi wale wote waliotajwa kule ndani, sio kwamba angwafaidisha kwani wangeenda kufungua kesi kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria?

Mimi naomba uwe unajaribu kujiweka kwenye viatu vya Kikwete na sio ku-mcritisize tu, jaribu kuchuukulia kama wewe ungekua Rais je ungekutwa na changamoto kama anazokumbana nazo wewe ungekua unafanya nini au ugeamuaje? Pia jaribu kuangallia kwamba tanzania ni nchi changa, nilikua nasoma takwimu za taifa jana, nikaona kwamba kati ya watu milioni 38.9 tuliopo tanzania, ni wananchi laki nne tu wenye digree moja...! Hizi takwimu zilikua zinafanya estimate kwamba tokea uhuru watu waliograduate unversity walikua ni watu 7,000 kila mwaka, ukizidisha 7,000X mara miaka 44 ya uhuru utapata jibu kamili...!

Sasa hebu asuume wewe ndio Rais unayeongoza taifa la namna hio, ambalo sehemu kubwa ya wananchi hawana elimu, wewe ungekua unafanyaje?

Tatizo lako ni kwamba unajaribu kulinganisha Tanzania na Marekani au na Uingereza, lakini umejuiliza Marekani au Uingereza inawasomi kiasi gani? au Ilipata lini uhuru? Pia, usilaumu tu ukiwa huko nje ya nchi, njooo huku tanzania uje uijenge nchi yako, usiishie kujenga nchi za watu halafu uishie kulaumu nchi yako na viongozi wako....!

Pia, usisahau kwamba ROME WAS NOT BUILD IN ONE DAY, tusifikiri tutaweza kulala na kuamka tukakuta kesho tanzania imebadilika, kama sisi wananchi wenyewe hatuwezi kubadilika suitegemee hata tungeletewa malaika kutoka mbinguni nchi yetu itabadilika....! Hayo ni maoni yangu mbadala tu....!
 
la ajabu ni kuwa ikifika mwaka 2010, watu watapewa vitu vidogo vidgo kama TShirts, baseball caps, na khanga zilzioandikwa Changua Kikwete, vikisindikizwa na mapilau kwa wing na watasahau yote haya. Kikwete atapita 85%. Miaka mitano mingine ya ubabasihaji itafutia
 
MKJJ....!

Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!

Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!

Mhafidhina, ujumbe mzito sana huu.

MMKJJ, siku utaandika postings zako kwa kuchambua pande zote mbili nitakuwa miongoni mwa wapenzi wa postings zako.
 
MMKJ, hata kama ungekuwa huna hiyo mission ya kijarida bado ningekushauri uchukue 'holiday', wengi wetu hapa tu part timers tu tofauti na wewe fulltimer- upo hapa kila siku ukishusha vitu vya nguvu, I really admire your hard working attitude. Go for it, take a brake, at least huko kwenye kijarida hutakuwa ukiburuzwa kwenye malumbano yasiyokuwa na kichwa wala miguu na matusi yasiyo na sababu.

Having said that, bado najiuliza tumchague nani awe Rais baada ya 2010 kama sio JK? Sioni nafasi ya urais ikiangukia kwa wapinzani, hata kama itatokea miujiza CCM ikamtosa JK!! mwingine yeyote atakayepitishwa atashinda! Tusitegemee upinzani kuchukua nchi hivi karibuni kama ruzuku zote zitaendelea kuishia makao makuu, CCM ina matawi na wanachama hadi vijijini, kwa uozo uliopo kwenye vyama vya upinzani kwa sasa itachukua miaka mingi sana kwa wao kufika huko.
 
MKJJ....!

Nakubaliana na mawazo yako lakini naomba ujaribu kuangalia na upande mwingine wa shilingi....!

Hivi umeshawahi kujiuliza kazi za Raisi ni nini haswa? Naomba usome katiba ya Jamhuri wa Muungano ndo utajua kazi za Rais....! Kazi za Raisi sio za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya Rais ni usimamizi wa serikali pamoja na kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa...!


Mhafidhina, umefanya kosa moja kubwa nalo kuonesha kuwa madai yao kuwa "Kazi za Rais siyo za kiutendaji kama unavyofikiria wewe, kazi ya RAis ni usimamizi wa serikali pamoja nakuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa". Kwa maelezo yako haya umethibitisha vitu viwili; hujui Katiba ya Tanzania hujaisoma (hivyo ni wewe unatakiwa uisome kwanza kabla ya kutaka mimi nisome) na pili huijui pia Katiba ya CCM ambayo ungeliijua usingesema kazi ya Rais ni pamoja na "kuhakikisha sera za chama chake zinasimamiwa". You are wrong on both counts.

Kwa vile msingi wa hoja yako is totally, inherently, and clearly flawed and without basis whatsoever, majibu yangu yanayofuatia hapa chini ni courtesy tu. Lakini ningekoma hapa hapa kwani kuendelea kujibu kilichotolewa kwa makosa ni kuzipa hoja hizo heshima isiyostahili. But with one day to go, I'll gladly do this without hesitation. May I.

Aidha, kuongoza nchi sio kama kuongoza kampuni ambapo unaweza ukatoa amri asubuhi na ikatekelezwa hapo hapo...! Uongozi wa nchi unataka burasa, hekima, upeo na maono makubwa sana pamoja na kujaribu kufuata ushauri mbalimbali kabla ya maamuzi, pia kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia katika uongozi wa nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mihimili mingine ya dola (mahakama, bunge na serikali), uheshimu wa utawala wa sheria na utawala bora, uheshimu wa haki za binadamu na mambo mengine mengi...!

Uongozi wa nchi unahitaji mtu kuwa na vitu hivyo wakati wote na mara zote; kiongozi wa nchi ambaye anasubiri kuwa na vitu hivyo baadaye au wakati matatizo yanapotokea hastahili uongozi wa nchi. Lakini zaidi busara, hekima, upeo, na maono makubwa sana hayahusiana hata kidogo na kuwashughulikia wahalifu.

Mtu aliyeghushi na kuiibia serikali hatakiwa kupewa muda kurudisha fedha anatakiwa kupelekwa mahakamani. Katika utawala wa sheria hoja ya hekima na busara is absolutely haina msingi. Ndio maana ukiangalia picha ya "Lady Justice" yule mwanamke wa mizani ya sheria utaona amefumbwa macho na kitambaa huku mkono mmoja ameshika mizani na upande wa pili sime. Haangalii kitu kingine chochote isipokuwa sheria.

Hii haina maana kiongozi wa nchi asiwe na tunu hizo bali anatakiwa awe nazo na awe na kitu ambacho wewe hujakitaja St. Thomas Aquinas anakiita Fortitude. Yaani ujasiri. UJasiri wa kutumia hekima hizo na kujua ni wakati gani kiongozi anatakiwa kuitii sheria unreserverdly and promptly. Rais Kikwete hakufanya hivyo leo na ameonesha hana hiyo hekima, busara, maono na vitu vingine vya njozi ambavyo unafikiri anavyo.

Uongozi wa serikali hauhitaji kutoa maamuzi ya haraka haraka na ya muda mfupi, inahitaji kutoa maamuzi ya muda mrefu na yenye busara...! Pia, sio kila kitu Rais anauwezo wa kukitolea maamuzi au amri, ndio maana kuna taasiri, mamlaka, na asasi mbalimbali za serikali ambazo kazi yake ni kusimamia mambo mbalimbali.... ! Hivyo basi usidhani kwamba uongozi wa Urais ni kazi rahisi...!

Kuna vitu ambavyo ni Rais peke yake ana mamlaka navyo na kama ungejua Katiba (ambayo hujui) ungefahamu kuwa Rais ana madaraka peke yake ya kusimamia watendaji wote wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na chombo kingine chochote chenye majukumu kama hayo hakimzuii sheria kutekeleza wajibu huo.

Ndio maana naamini Rais anatumia madaraka hayo kwa sababu anajua ana uwezo huu. Kama angejua kuna taasisi nyingine zinazoweza kufanya mambo fulani kwanini hakuziacha taasisi hizo kufanya kazi ipasavyo? Si walimpelekea orodha ya "vigogo wa Unga"? kwanini wakati Polisi wana sheria inayoowangoza na yeye akaipokea? Kwanini aliunda timu ya EPA wakati ofisi ya Mwanasheria Mkuu, TAKUKURU na Polisi zipo kwa mujibu wa sheria unless anafikiri ana nguvu zaidi ya kuvifanya vyombo hivyo vifanye anachotaka yeye? vinginevyo kwanini alipokea ripoti ambayo hakuagiza?

Ni kwa sababu Rais wa TAnzania ana nguvu za kisheria kukomesha ufisadi, kuleta nidhamu serikalini, na kimsingi utawala bora kwa kutumia madaraka yake aliyonayo bila haja ya kumpa nguvu nyingine. Ungesoma Katiba ungeelewa hili.
Pia Unapokua raisi changamoto ni nyingi sana na mambo ni mengi sana tena kwa wakati mmoja....! Jaribu kufukiria kwamba unakua Raisi halafu kuna wizara 22 (Mambo ya ndani, maji, mifugo, sheria na katiba, elimu, afaya, fedha, mambo ya nje, miundombinu, sayansi etc) ziko chini yako na kila moja inamatatizo makubwa ya kutolea maamuzi tena maamuzi mzito, usipokua makini, ndio hivyo unaweza ukaishia kuwa dictecta kwa sababu utataka kufanya maamuzi ambayo utataka kuona matokeo yake mara moja...!

Huu ni utetezi wa uzembe, kutokuwajibika na uongozi usiofaa nchini. Kama Rais ameteua watu aambao hawawezi kazi hadi Rais aingilie kati na watu hao wanafanya kazi kwa ridhaa ya RAis, Rais alitakiwa awafukuze na kuweka watu wengine na hao hawawezi anawatimua hadi watu wanaoweza kazi wanapatikana! Haiwezekani kuvumilia uzembe wizarani, kwenye taasisi ati kwa sababu wanasubiri maamuzi ya RAis.

Si yeye mwenyewe hivi majuzi amewakumbusha kule Iringa (kama ulikuwa unafuatilia)? Nakushauri upitie hotuba yake aliyoitoa Ngurdoto aliwaambia nini viongozi wenzake. Wakuu wa Mikoa, Mawaziri n.k wana nguvu za kutosha kabisa kukabiliana na matatizo kwenye sehemu zao na kama hawawezi kuyashughulikia kwa sababu ni waoga au wanasubiri maelekezo toka juu Rais angewatimua.

Si yeye aliwaagiza kina Mwanyika wawachukulie wahusika wa uhalifu huu wa Benki Kuu? Si yeye aliyeutangazia ulimwengu kuwa kilichofanyika BoT kimemuudhi kweli na akawaagiza wawachukulie watu hao hatua za kisheria? Leo alipozungumza ulisikia alitaja sheria gani ilitumika kuwanyang'anya watu hao pasi za kusafiria? ULisikia ni amri gani ya mahakama ilitangaza kutaifishwa mali za watu hao au waliitaifisha kwa sheria gani. Sheria hizo zipo kwanini hatukuambiwa zimetumika?

Je huoni kuwa Rais tayari ana nguvu hizo za kiidikteta ambazo tumempa kisheria? Sasa hili la kusingizia watu wa chini linatoka wapi? The buck stop with the President. Hakuna udhuru, kisingizio, au utetezi utakaondoa hilo.
Kwa mfano, mimi nilimuelewa sana Kikwete alipozungumzia suala la kiwafukuza kazi wale walihusika kwenye EPA, embu chukulia kama Kikwete angekua na hasira/maamuzi ya haraka haraka akamua kuwafukuza kazi wale wote waliotajwa kule ndani, sio kwamba angwafaidisha kwani wangeenda kufungua kesi kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria?

Asingewafukuza hivi hivi kwani kuna aliokuwa na nguvu za kuwakufukuza na wengine kama walifanya wizi unafikisha mahakamani ili mahakama iamue hatia yao. Kutokwenda mahakamani in the first place ni kosa; kuwaacha watu walioshuhudia uhalifu mkubwa ni kutetea uzembe. Msikilize Dr. Slaa kesho kwenye KLHN akifafanua hili vizuri.


Mimi naomba uwe unajaribu kujiweka kwenye viatu vya Kikwete na sio ku-mcritisize tu, jaribu kuchuukulia kama wewe ungekua Rais je ungekutwa na changamoto kama anazokumbana nazo wewe ungekua unafanya nini au ugeamuaje?

To tell you the truth nimefikia ningekuwa mimi yeye ningefanya nini? Easy! Kwa sababu kama Kikwete angekuwa ndio Rais wa Kwanza wa Tanzania katika mazingira haya labda tungemuonea huruma kidogo kwa sababu tunaweza kutoa excuse ishirini elfu za kutofanya mambo fulani. Akiwa ni Rais wa nne wa Jamhuri yetu wakati huu hana udhuru waliokuwa nao Nyerere, au Mwinyi to some extent.

Pia jaribu kuangallia kwamba tanzania ni nchi changa, nilikua nasoma takwimu za taifa jana, nikaona kwamba kati ya watu milioni 38.9 tuliopo tanzania, ni wananchi laki nne tu wenye digree moja...! Hizi takwimu zilikua zinafanya estimate kwamba tokea uhuru watu waliograduate unversity walikua ni watu 7,000 kila mwaka, ukizidisha 7,000X mara miaka 44 ya uhuru utapata jibu kamili...!

Sasa watu hao wote laki nne (assuming your information is correct) wanafanya nini? Kuendesha serikali efficiently huitaji watu wengi wenye digree bali wasomi wenye kujua wanachofanya. Tatizo la hao watanzania siyo kuwa na digrii moja tatizo ni kama hizo digrii moja moja walizonazo zinaonekana wanapofanya kazi. Kuna wengine hata ukiwapa digrii elfu watakuwa vile vile. Unajua Nigeria ina watu wangapi wenye digrii? Kibao!

Sasa hebu asuume wewe ndio Rais unayeongoza taifa la namna hio, ambalo sehemu kubwa ya wananchi hawana elimu, wewe ungekua unafanyaje?

Hivi unajua kuna wasomi wangapi kwenye nchi kama Marekani au Uingereza wenye digrii? Hili la kufikiri kuwa na elimu ya digrii ndio suluhisho la matatizo yetu ni kujidanganya. Inasaidia katika kupanua uwezo wa watu kuelewa na kufahamu mambo lakini waliotufikisha leo TAnzania siyo wajinga bali ni wasomi. WAliokwapua fedha za Benki Kuu hawakuwa watoto wa shule ya msingi; walioiba Meremeta n.k ni wasomi na wengine na Uprofesa wao. So tatizo letu siyo kukosekana watu wenye elimu ya juu serikalini kwani wapo wengi tu, tatizo letu ni kuwa hatujavuka from theories to applications. Ningekura Rais ningehakikisha wasomi wanafanya mambo yao kisomi na wenye kuongoza wanaoongoza. Uongozi mzuri siyo neno mbadala la Msomi!!

Tatizo lako ni kwamba unajaribu kulinganisha Tanzania na Marekani au na Uingereza, lakini umejuiliza Marekani au Uingereza inawasomi kiasi gani? au Ilipata lini uhuru?

Wrong nalinganisha Tanzania na nchi kama Namibia, Malaysia, South Korea n.k silinganishi na nchi kama Marekani. Lakini hata nikitaka kulinganisha na nchi hizo bado model ya maendeleo inatudai kufanya better and more than what we are doing today.
Pia, usilaumu tu ukiwa huko nje ya nchi, njooo huku tanzania uje uijenge nchi yako, usiishie kujenga nchi za watu halafu uishie kulaumu nchi yako na viongozi wako....!

Hata wakija watu kutoka mbinguni au kutoka kwa wafu wakafufuka TAnzania hawatasikilizwa. Wengine walioko huko si tulikuwa nao huku na walikuwa wakosoaji na sasa wako serikalini na wamenywea na kutota kama mabua majinii? Na kuikosoa Tanzania haiitaji mtu uwe Tanzania kuikosoa! Natumaini hauna digrii kwa sababu kama unayo hoja yako hiyo inaonesha ni mawazo gani waliyonayo baadhi ya hao watu walioko serikalini. Kwamba wakikosolewa wanataka wakosolewe na mtu aliye nyumbani! Ni hoja dhaifu. Nitawakosoa nikiwa nyumbani, ugenini na ikiwezekana hata nikiwa kaburini!
Pia, usisahau kwamba ROME WAS NOT BUILD IN ONE DAY

Right! angalau wao walikuwa na Kaisari!!

, tusifikiri tutaweza kulala na kuamka tukakuta kesho tanzania imebadilika, kama sisi wananchi wenyewe hatuwezi kubadilika suitegemee hata tungeletewa malaika kutoka mbinguni nchi yetu itabadilika....! Hayo ni maoni yangu mbadala tu....!

Kama mawazo yako yanawakilisha kwa kiasi chochote mawazo ya baadhi ya viongozi wetu kwa hakika tusiotee kubadilika. Hatuna hamu ya kubadilika, hatutamani kubadilika kwa sababu tunataka vitu vitokee vyenyewe tu. Hatuoni wivu wa maendeleo na kushangaa inakuwaje nchi nyingine zilizokuwa sawa na sisi kimaendeleo zimeibuka kwa kasi. Leo hii Rwanda itaipita Tanzania kwa kasi ya ajabu na wewe na watu wengine wenye mawazo kama ya kwako mtaendelea kuwaambia Watanzania wakubali hali halisi kuwa "roma haikujengwa kwa siku moja". Msumbiji itapiga hatua ya maendeleo, and so will Angola, wakati watu wenye mawazo yako wanaendelea kuimba "Rais hana kazi ya utendaji yeye ni msimamizi tu"

Nyinyi ndio watu ambao inabidi tuwapinge mbadilishe fikra zenu na kama Paulo alivyoangaziwa na nuru akielekea Damascus inabidi na nyinyi mpigwe kama na radi ya uzalendo na macho yenu yafunguke na muweze kuwaona kuwa TAnzania yenye neema haiwezekani bali inafanywa iwepo na watu wenye kujitoa kwelikweli. Mmulikwe na muangaziwe na nuru hiyo ili hatimaye mjue kuwa Tanzania haiwezi kufika tunakotaka kufika kwa mawazo ya viongozi waliopo ambao ni waoga kufanya maamuzu, wagumu kuthubutu, na wana ni goigoi wa vitendo.

Yes, I'm done with Kikwete and the people whose thoughts resemble defeat in any way, shape or form. Hamna nafasi ya kuendelea kuongoza nchi yetu na ni jukumu la kila Mtanzania kuwapinga kwa nguvu zote, kuwaumbua na kuwataka mbadilike na msalimishwe mbele ya nguvu ya jina la Taifa letu. Nawapinga sasa, na nitawapinga hadi viongozi waoga wasalimu amri!
 
Back
Top Bottom