Kwa hakika kabisa sahihi hizi mbili ni tofauti. Lakini kama binadamu wenye utashi na kufikiri yapaswa kujiuliza nmaswali kadhaa.
1. Sahihi hizi mbili (ya uwongo na ya kweli) zinatoka kwenye document gani?
2. Saini ya juu ukuangalia ni saini iliyoandikwa kwenye kipande cha karatasi, kikabandikwa juu ya eneo la kuweka sasa, ikapigwa photicopy (ndio maana chini kivuri cha mstari ilipoanzia karatasi mpaka kuishia kimeonekana) aliyefanya hivi alifanya kwa malengo gani?
3. Madai ya wajumbe kudai hati itolewe, hati ikaletwa tayari mtu akawa na saini ya pili mfukoni na kuitoa kwa ulinganisho inatia shaka, alijuajeinayokuja itakua feki?
4. Kwa wanaojua maudhui ya mkataba wa awal, je kunamabadiliko?
5. Tunadhani ni kwa nini kiongozi mmoja aliye hai na inadaiwa saini yake ni fake, nae kahojiwa akakanusha kuwa si fake sahihi ni yake, lakini bado tunang'ang'ana ni fake?