Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanaume (mmoja, Adamu) na yule yule) mwanamke (mmoja Hawaa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane (tu basi, siyo mkejeliane). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule ambaye mcha Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote)". (49:13).
Kumbe Mwenyezi Mungu baada ya kutuumba kutokana na nafsi moja, bado alitugawa katika mataifa na makabila tofauti tofauti, lakini si kwa lingine bali ili tuweze kujuana.
Hebu na turejee katika Hadithi ya Mtume (s.a.w.) iliyosimuliwa na Abi Nadhrah, kwamba alimsimulia mtu aliyesikia khutuba ya Mtume (s.a.w.) aliyoitoa katikati ya siku za Tashriq akisema:
"Sikilizeni, hakika Mola wenu ni mmoja na hakika baba yenu ni mmoja. Hakuna ubora kwa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu wala hakuna ubora wa mwekundu kwa mweusi wala mweusi ju ya mwekundu. Isipokuwa kwa kumcha Mwenyezi Mungu
UNAYO HOJA NYENGINE?