Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Kuna mama mmoja aliandikwa kwenye gazeti, aliunguliwa na nyumba huko SA. Akaanza kulalamika. "Sina ugomvi na mtu, nashangaa kurogwa namna hii." Yaani anaamini moto umeletwa ma wachawi. Mbantu akiumwa anaamini kuwa amerogwa anaenda kuagua, wakati mwenzie mmasai anaenda porini kutafuta miti shamba.
Mwingine anasema, "Lambalamba lazima aje, wachawi wamezidi kututesa. Mtu unalima hadi vinakomaa hauumwi, ukivuna tu unaanza kuumwa. Ukishatumia mavuno yote kujitibu ndiyo unapona."
Imani za kishirikina kwa wabantu hadi kwa waliopita shule zimejaa, "daktari asipoona ugonjwa kwa sababu uwezo wake mdogo utasikia anasema jaribu mambo ya kienyeji."
Mbantu biashara ikienda vibaya anaamini karogwa, mmoja juzi kati namwambia business imeenda hovyo, anasema, "Au mambo ya uchawi!"
Wakati mzungu anahangaika na teknolojia ya kuchimba dhahabu, mbantu anahangaika na waganga wa kienyeji. Mahindi shambani yasipokomaa, badala ya kuangalia quality ya udongo nk, anaamini karogwa.
Unakuta barabara ni mbaya na sehwmu hiyo ni mbaya, ajali Ikitokea mara kwa mara, mbantu anaamini kuna uchawi!
Imani hii kuwa matatizo yanaletwa na wachawi ipo kwa wabantu tu. Pengine ndiyo maana wabantu ndiyo watu maskini zaidi duniani. Wabantu suluhisho ya matatizo yao ni kuagua na mbinu zingine za kichawi. Utamaduni unaamua kwa kiasi kikubwa mafanikio ya jamii fulani, inawezekana adui mkubwa wa maendeleo ya wabantu ni hii imani yao juu ya uchawi. Imani hii inaendesha maisha yetu, hatuumizi kichwa kutatua matatizo bali tunaenda kuagua.