Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
NI dhahiri kuwa siku ya leo Alhamisi (23/4/2026) macho ya watanzania yatakuwa mubashara kufuatilia ripoti ya Tume ya uchunguzi ya matukio ya tarehe 29 octoba 2025 inayotarajiwa kukabidhiwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ni muhimu kama taifa tufahamu kuwa "Tume ya uchunguzi" iliundwa kwa lengo chanya la kufuatilia chanzo Cha matukio Yale na ilijikita zaidi Katika ushirikishwaji wa wananchi Katika utoaji wa maoni na utatuzi wa kudumu wa mambo hayo.
Tume hiyo imefanya kazi zake kwa weledi sana na ilijumuisha watu muhimu na wenye uzoefu wa kutosha wakiwemo majaji wakuu wastaafu wa mahakama ya tanzania (Jaji Chande na Prof Jumaa), pia yupo IGP mstaafu Said mwema, mabalozi na watu wengine waliolitumikia taifa Katika sekta nyeti na muhimu kama vile JWTZ.
Katika kipindi hiki Kuna kundi la watu ambao wanajaribu kutengeneza picha hasi inayoharibu taswira ya Tume ya uchunguzi. Wanajaribu kuuaminisha umma kuwa Tume haijafanya lolote la maana na wanataka ipuuzwe.
Ni wakati sahihi wa taifa kutafakari mambo mawili kabla ya kuwasikiliza wanaharakati wanaoichafua taswira ya Tume.
Kwanza; Taifa linahitaji uponyaji wa kudumu na sio mgawanyiko wa kudumu. Inapotokea mwanaharakati yoyote anaanza kuichafua Tume kabla hata haijaja hadharani kutoa ripoti yake hadharani ni wazi kuwa huyu halitakii mema taifa na wengi wao wanaendesha Maisha yao kwa Kazi hii. Lazima tuwakatae kwa nguvu zote.
Pili; Maisha yanatakiwa kuendelea, kilichotokea oktoba 29 sio mwisho wa kuendelea kuishi Maisha yetu yenye kuhamasisha umoja wa kitaifa na uzalendo kama hapo awali, yaliyotokea yametokea kwenye nchi nyingi sana tena kwa ubaya zaidi ya yaliyotokea kwetu.
Nawaomba na kuwaasa sana watanzania tuungane kuisikiliza ripoti ya Tume ya uchunguzi siku ya tarehe 3/4/2026. Tusikubali kuanza kujazwa maneno ya uongo na wahuni wachache ambao wapo kimaslahi binafsi.
Nchi yetu ni moja, mbali na yote yaliyotokea hatuna budi kuendelea kuilinda kwa moyo Thabiti usio na mawaa.