Imani potofu huchangia sana umaskini

Imani potofu huchangia sana umaskini

Forfofo

Senior Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
161
Reaction score
359
Kuna mtoto wa jirani mtaa wa pili kamezoea kila nikipita kakiniona lazima kanipungie, japo hajawai kuniona ana kwa ana basi tu hivyo.

Kakiona gari kanaikimbilia na kuipungia. Sasa leo nimepita kwa mguu nilivokaona nikakaita, nikamuuliza jina na ufaham wa hapa na pale. Lakini kakaniomba hela kakadai kana njaa hawajala, mama yao kaenda kwenye kibaruani (ni mtoto km miaka minne ivi).

Basi nikamuita mkubwa wake ambae ana umri km miaka 8,9 ivi nikaenda nako dukani nikamuemelea mchele, sukari, mafuta, chumvi, na mahitaji muhimu ya kula. Nikampandisha kwenye boda ninaemfahamu na kunifahamu akampereka nyumbani.

Nashangaa boda huyo ananipigia simu eti kamkuta mamake mtoto karudi yuko nyumbani, amekataa kupokea huo mzigo eti siku izi watu wanachukua nyota za watu kupitia misaada izo, kanamwambia boda arudi navyo.

Kwaio ananihisi huo msaada wangu una lengo lake.
Kwa mazingira ya hiyo familia na hivyo huyo mtoto alivyonambia ana njaa ndo ikanishawishi nimsaidie na ni kweli alionekana ana njaa,na niliplan kumfanyia mengine zaidi. Na si kwamba mamake hanifahamu, ananifahamu.

Kwanini maskini ukimpa kitu cha bure anahisi ni mtego na ukimwambie akilipie anaona ni gharama au unataka umuibie!?

Nimelishangaa sana hili.
 
Hujafanya haraka wala hujafanya kosa, ni akili za huyo mama zilipoishia(sio kosa lake ni ukosefu wa elimu na maarifa) hivyo kuwa na amani
Mi nadhani km ni kuhisi ivo basi hata km ningefanya baada ya mda kupita ndo angehisi zaidi
 
MKUU angali wema unaponza kuna ulawiti utanunua kesi kwa gharama kubwa wabongo sio watu wazuri
 
Kuwa makini kaka kutumia hisia kwenye Maisha....
 

Attachments

  • Screenshot_20240906-123504~2.png
    Screenshot_20240906-123504~2.png
    83.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom