shuka chini
JF-Expert Member
- Feb 27, 2024
- 842
- 1,928
Utakuja kufa kwa kupenda sifa za kijinga.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umekosea kufanya mambo makubwa na watoto.Kuna mtoto wa jirani mtaa wa pili kamezoea kila nikipita kakiniona lazima kanipungie, japo hajawai kuniona ana kwa ana basi tu hivyo.
Kakiona gari kanaikimbilia na kuipungia. Sasa leo nimepita kwa mguu nilivokaona nikakaita, nikamuuliza jina na ufaham wa hapa na pale. Lakini kakaniomba hela kakadai kana njaa hawajala, mama yao kaenda kwenye kibaruani (ni mtoto km miaka minne ivi).
Basi nikamuita mkubwa wake ambae ana umri km miaka 8,9 ivi nikaenda nako dukani nikamuemelea mchele, sukari, mafuta, chumvi, na mahitaji muhimu ya kula. Nikampandisha kwenye boda ninaemfahamu na kunifahamu akampereka nyumbani.
Nashangaa boda huyo ananipigia simu eti kamkuta mamake mtoto karudi yuko nyumbani, amekataa kupokea huo mzigo eti siku izi watu wanachukua nyota za watu kupitia misaada izo, kanamwambia boda arudi navyo.
Kwaio ananihisi huo msaada wangu una lengo lake.
Kwa mazingira ya hiyo familia na hivyo huyo mtoto alivyonambia ana njaa ndo ikanishawishi nimsaidie na ni kweli alionekana ana njaa,na niliplan kumfanyia mengine zaidi. Na si kwamba mamake hanifahamu, ananifahamu.
Kwanini maskini ukimpa kitu cha bure anahisi ni mtego na ukimwambie akilipie anaona ni gharama au unataka umuibie!?
Nimelishangaa sana hili.
kama hufahamiani na mtu vizuri usijaribu tena kumpa hata zawadi unaweza kuuwawawa kwa kuhisi watekaji wa watoto. ( Yes...yaliwatokea puani juzi hapo manyara..Tena pipi tu
Taikon wa fasihi...namnukuu..'maskini wache wafe;MKUU angali wema unaponza kuna ulawiti utanunua kesi kwa gharama kubwa wabongo sio watu wazuri
Mi naona wewe pia una imani za kishirijina. Kwa nini usimpatie fedha akanunue hitajio lake?Kuna mtoto wa jirani mtaa wa pili kamezoea kila nikipita kakiniona lazima kanipungie, japo hajawai kuniona ana kwa ana basi tu hivyo.
Kakiona gari kanaikimbilia na kuipungia. Sasa leo nimepita kwa mguu nilivokaona nikakaita, nikamuuliza jina na ufaham wa hapa na pale. Lakini kakaniomba hela kakadai kana njaa hawajala, mama yao kaenda kwenye kibaruani (ni mtoto km miaka minne ivi).
Basi nikamuita mkubwa wake ambae ana umri km miaka 8,9 ivi nikaenda nako dukani nikamuemelea mchele, sukari, mafuta, chumvi, na mahitaji muhimu ya kula. Nikampandisha kwenye boda ninaemfahamu na kunifahamu akampereka nyumbani.
Nashangaa boda huyo ananipigia simu eti kamkuta mamake mtoto karudi yuko nyumbani, amekataa kupokea huo mzigo eti siku izi watu wanachukua nyota za watu kupitia misaada izo, kanamwambia boda arudi navyo.
Kwaio ananihisi huo msaada wangu una lengo lake.
Kwa mazingira ya hiyo familia na hivyo huyo mtoto alivyonambia ana njaa ndo ikanishawishi nimsaidie na ni kweli alionekana ana njaa,na niliplan kumfanyia mengine zaidi. Na si kwamba mamake hanifahamu, ananifahamu.
Kwanini maskini ukimpa kitu cha bure anahisi ni mtego na ukimwambie akilipie anaona ni gharama au unataka umuibie!?
Nimelishangaa sana hili.
Mkuu ratizo la vijana show off na mbwembwe vinawaharibu. Wanakosa akili ya kujiongeza.Hakuna Mtu Mwenye akili timamu atachukulia poa Msaada uletwe Kupitia mwanae.Yaani hiyo ni aibu kubwa Sana.Yaani ukiona mwanao anakuja na kitu na amepewa unatamani akitupe.Tukiwa wadogo tukiambatana na mama zetu Kwa Majirani,hata kama tuna njaa,kwa Majirani kuna msosi,mama alikuwa anapiga jicho 1 la kukwambia ukome.Utakula nyumbani.Marehem mama yangu nikiwa sekondari aliwahi niambia,Mwanangu kama Karo na Matumizi ya Shule hutapewa hapa ndani usiende Kwa Mjomba wala Kwa shangazi,vumilia Hadi utumiwe Kwa posta.Baadaye niligundaua hekima iliokuwa ndani Yake.Shule inapoisha hata ambaye hakukusaidia anaanza Kupiga mayowe tumekusomesha.Marehem Mkapa akiwa Rais hakuwa anapenda Mawaziri wawe wakitangatanga Kwa donors Kuomba msaada.Nenda straight Kwa Mkuu wa Kaya saidia.