Hapana... sijazungumzia kabisa suala la dini! Ukirejea post yako ya kwanza kwangu, umenielewa vizuri sana na umeeleza vizuri sana!!!
Hoja yangu ni kwamba, kila panapohitajika matumizi ya akili, basi kwenye any population, mara nyingi kama sio zote wachache wanakuwa ndo wapo kwenye right side! Kinyume chake, kwenye complex issue kama ya God's existence, over 55% percent of the world population believe in God's existence!
Now, ikiwa kwenye mambo mengi kama siyo yote yanayohitaji kutumia akili and/or reasoning, larger population inakuwa kwenye wrong side, should we consider it as exceptionalism kwamba though the largest world's population believe in God's existence but still hawa ndio wapo sahihi contrary to my belief kwamba wengi wanakuwa kwenye wrong side?!
Above is just a wise version of arguing "does it imply God doesn't exist" cuz' no one point in time the largest population ever been right against the few!!!
Kwa hiyo argument yako ni kwamba kuna watu wachache wenye maisha mazuri na ambao hawaamini uwepo wa Mungu na pia kuna wengi wenye maisha mabaya na ambao wanaamini uwepo wa Mungu, siyo? Hapana sina uhakika na huu utafiti, siwezi kutoa comment juu ya hilo.
Hata hivyo, kama kweli kuna utafiti umeonyesha hivyo, basi yawezekana kabisa kuwa tatizo letu linaweza kuwa kwenye post niliyoiweka hapo chini. Naomba uisome post hiyo hapo chini. Wengi wetu huwa hatushiki kitu kimoja. Japo post hii inaongelea case ya Afrika, lakini watu wote huwa tuko hivyo, when it comes to religious beliefs, na si Afrika tu. Ukitaka ku-excel vizuri katika maisha, unatakiwa uchague kimoja tu na si vyote. Hao wachache unaowaona wana maisha mazuri, naamini ni wale walioshika kimoja tu na si vinginevyo, na ninaamini idadi kubwa ya hao ni wale wanaoamini uwepo wa Mungu.
Otherwise inabidi u-provide emperical data kunifanya niamini otherwise. Tudadavulie hapa JF tuone hizo data zako wewe umezipata kutoka wapi! By the way, wewe unaamini uwepo wa Mungu? Ni maskini? Na kama ni maskini, unadhani kuwa umaskini wako umetokana na kuamini kwako kwa uwepo wa Mungu?
SOMA HAPA CHINI🙁 Ni post imewekwa humu na Evarist Chahali iDec 3, 2018 la sikupenda kuweka link yake kwa sababu content na title havina uhusiano)
Kabla sijaingia kwa kina kwenye mada hii, naomba kutanabaisha background yangu kidogo. Nilipokuwa mwaka wa tatu UDSM nilibahatika kusoma kozi ya Sosholojia ya Dini (Sociology of Religion). Na kwa bahati zaidi, mwalimu wetu alikuwa Dkt Father Sivalon, Padre wa Kanisa Katoliki huyu, ambaye PhD Thesis yake ni rejeo muhimu kwenye stadi za mahusiano kati ya Dini na dola Tanzania (itafute ukipata wasaa).
Katika kozi hiyo pamoja na mambo mengine tulifundishwa kuhusu "imani" kuu tatu nchini Tanzania. Ya kwanza ni kiitwacho African Traditional Religions (ATRs), Uislamu na Ukristo. Both Uislam na Ukristo zinafahanika kama "dini za kimapokeo" yaani zilizokuja baada ATRs.
Ni hivi, kabla ya ujio wa dini hizo za kimapokeo, babu na bibi zetu walikuwa na imani kwenye mizimu. Na mizimu hiyo ilikuwa ya aina mbili, the living dead na the dead dead. The living dead ni mizimu ya watu waliokufa na kuzikwa kwa kuzingatia mila za jamii husika na inaendelea kuenziwa kwa vitu kama kuwapatia watoto wachanga majina ya babu zao waliofariki au matambiko.
The dead dead on the other hand ni mizimu iliyosahaulika. Na hadi leo hii, maeneo ambapo kunatokea vifo vinavyopelekea baadhi ya marehemu "kusahaulika" mfano Kitonga, Machinjioni (Dar), Wami, nk yamekuwa yakihusishwa na the dead dead kwa maana ya "hasira ya mizimu hiyo kutelekezwa."
Naomba kukumbusha kuwa somo hili lilikuwa linafundishwa na Padre. Na in some way lilikuwa lina conflict vs imani yake kama Mkatoliki. Lakini kama tujuavyo kwenye usomi, sentiments hazina fursa vs facts.
Kama ilivyo kwa Waislamu na Wakristo wanavyoamini katika Mungu, kwenye ATRs concept ya "mungu" ilikuwa ya kibinadamu zaidi, kwa sababu "miungu" were in fact watu waliowahi kuishi na jamii husika, wakaenziwa wakati wa vifo vyao, na baada ya vifo vyao.
Lakini pia kulikuwa na watu wenye majukumu mbalimbali katika jamii ikiwa ni pamoja na matabibu. Mind you hakukuwa na hospitali wakati huo. Hawa ni watu walioweza kuponya wagonjwa na kuzuwia majanga.
Fast forward miaka kadhaa baadaye, ukaja Uislamu na baadaye Ukristo. Na dini zote mbili zilifanya jitihada kubwa kukemea na kupambana na ATRs. Hata hivyo, zote hazikufanikiwa "kuua" ATRs na fast forward 2018, "dini" kubwa zaidi Tanzania ni ATRs, ikifuatiwa na Waislamu na nafasi ya tatu ni Wakristo.
Ni kwamba, baada ya Uislamu na Ukristo kushindwa kuangamiza ATRs, kilichofuata ni co-existence. Kwahiyo miongoni mwa Waislamu kuna "waumini" wa ATRs na hivyohivyo miongoni mwa Wakristo, na ndio maana ATRs ina "waumini" wengi zaidi kuliko dini hizo mbili za kimapokeo. Yaani wakati hakuna Mkristo ambaye pia ni Muislam, na hakuna Muislam ambaye pia ni Mkristo, ATRs zina Waislamu na Wakristo lukuki.
Asili ya ushirikina: kwa kifupi kabisa (maana ni mada ndefu hii) ushirikina ni corruption ya nguvu za asili ambazo awali zilitumika kama taaluma ya utabibu kwenye ATRs. Kwamba zama hizo, hawa watu wenye nguvu za kutibu walikuwa na jukumu moja tu la kutibu wenye matatizo ya kiafya.
However, muingiliano kati ya ATRs na dini za mapokeo uliopelekea nguvu hizo kuwa corrupted ambapo badala ya kutumika kwa nia njema tu (kama kutibu maradhi nk) zilitumika pia kudhuru watu. Kwa kifupi kabisa, hiyo ni asili ya ushirikina.
Fast forward to zama hizi tukizonazo: dini katika asili yake ni jitihada za mwanadamu kiimani kumudu mazingira yake. Dini ni imani. Na dini inahusu zaidi "mazingira" ie uhai, afya, kifo, mafanikio, nk.
Sasa pale dini za mapokeo zinapoonekana kushindwa "kutatua matatizo ya kimazingira" watu wanakimbilia kwenye ATRs. However, hakuna mtu anayekiri kuhusu hili japo ni ukweli usiofichika.
Kwa bahati mbaya au makusudi, ushirikina umekuwa sehemu muhimu katika medani za uongozi, tangu ngazi ya familia hadi kitaifa. Imani huko maofisini ni kwamba huwezi kuongoza kama "upo mweupe." Na kuna imani kuwa "kama hujakwangwa vya kutosha, wabaya wako watakukaanga."
Nirejee kwangu. Kwa bahati nzuri katika ukoo wangu kuna ndugu wawili ambao sio tu ni waganga bali pia ni waumini wa ATRs. Kama "mwana-Sosholojia ya Dini" hii imekuwa fursa muhimu kwangu kufanya "tafitu zisizo rasmi" kuhusu nafasi ya ushirikina katika nyanja mbalimbali za maisha ya Watanzania.
Hali sio nzuri. Ushirikina umevuka kiwango kiasi kwamba sio suala la aibu tena, bali ni sifa muhimu ya kufanywa uogopwe. Ukijua kuhusu "Vita vya kishirikina" zinazoendelea hata muda huu, unaweza kukata tamaa kukesha unapiga kelele kuhusu chama chako na/au viongozi wake.
A number of things. Moja, ajali nyingi zinazoendelea kutokea ni sehemu ya mahitaji ya kishirikina na viongozi mbalimbali. Bwana mmoja huko Singida anadaiwa "kuondoa" zaidi ya watu 100 kwa kusababisha ajali. Watu wa kitengo wanamjua.
To make matters even worse, kumejitokeza trend mpya ambapo u-Freemason umejipenyeza kwa njia mbili: kupitia ushirikina na kutokana na mahitaji ya watu wengi "maarufu" kuhitaji fedha za haraka, na nyingi, na protection." Uzuri wa Freemason ni kwamba mwanachama wao hahangaiki kutafuta waganga. Akiwa na shida, anawasilisha ombi kwa wahusika, nao kama timu moja, wanatafuta ufumbuzi. Sambamba na hilo ni kafara za damu, ambazo kwa namna flani nazo zinachangia wimbi la ajali Tanzania.
Kuna mengi yanaendelea ambayo moja kwa moja yanaathiri medani ya uongozi lakini kwa bahati mbaya HAYAZUNGUMZIKI. Na ukijaribu kuyazungumzia, si ajabu ukaonekana mwehu. Lakini suala hili ni kama janga la Ushoga. Watu wale wale wanaokemea ushoga hadharani ndio hao hao wanalofanya mashoga wawe na followers 100k plus kwenye social media. Kama tunauchukia ushoga that much, hao followers ni akina nani kama sio "wanafiki wanaokemea ushoga hadharani lakini ni waumini faraghani"?
Pengine ni wakati mwafaka wa kuanza conversations kuhusu suala hili ambalo japo tunakwepa kuliongea hadharani, lina impact kubwa katika medani ya uongozi na mustakabali wa Tanzania yetu.
I stand to be corrected.
NB: Jedwali pichani ni hali ilivyokuwa mwaka 2010. Waweza kusoma zaidi hapa
93% believe in #Witchcraft in #Tanzania