Imani Yetu Kuhusu Uwepo wa Mungu Inakiuka Uwezo Wetu wa Kufikiri Katika Kupatia!!!

Imani Yetu Kuhusu Uwepo wa Mungu Inakiuka Uwezo Wetu wa Kufikiri Katika Kupatia!!!

Kwanza tukubaliane kuwa binaadamu ana fundi aliyemuunda,ama aliyeunda mazingira na sababu za kupatikana binaadamu,Kuhusu dizaina wa huyo alietudizaini sisi huo ni mjadala mwengine.
Siwezi kukubali kwa sababu hakuna uthibitisho ambao ni convincing.Argument unayotumia ni argument ya first cause au design ambayo haina nguvu.

Ukisema binadamu mwili wake ni complex hivyo lazima awe na designer, then hata Mungu atahitaji awe na designer pia.

Je Mungu designer wake ni nani?
 
chige

At the risk of sounding pompously self congratulating and uppity.

Kwa mtu aliyesoma statistics na kujua standard /bell curve/ normal distribution ataelewa umeandika nini hapo.

Na kwa nini napata tabu sana kuelezea Mungu hayupo, kwa sababu nabishana na majority iliyo chini ya bell curve.
Mfano mfu sababu hauendani na mada husika ya mtoa mada.
 
Kwa uelewa wangu mkuu huku kusema kwamba masuala ya Mungu hayapaswi kuhojiwa,huja pale watu wanapotaka kuhoji vitu ambavyo hatuna elimu navyo. Kuna mambo ambayo hatuyajui kwa sababu hatuna elimu nayo,na ndiyo hapa nilipopakusudia mimi na ndiyo nikasema hakuna wa kuhojiwa hayo masuala.

Kwahiyo yale ambayo tuna elimu nayo wapo wa kwenda kuwauliza,ila zaidi ya hapo huko ndiyo nadhani penye makatazo.
HAKIKA.

MFANO;

Unapolala kila siku unaelewa ni kipi kinachokufanya ulale(catalyst)?

Unalalaga saa ngapi na ni kipi kinachokuamsha?

Ndoto unazootaga ni nani anazianzisha ukiwa usingizini kila siku?

Na kwanini huyo anayekuanzishia hizo ndoto zipo zitazotafsirika na zingine hazitatafsirika, je kwanini akupangie masharti kwa namna ya hizo ndoto zitakavyokujia?

So upeo wetu Binadamu ni 0% kwa aliyetupatia pumzi/uhai, sema tu sababu "kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani" ndiyomaana unakutana na mbegu zisizojielewa kama akina hawa waleta mada.

Maana tunajiuliza vitu ambavyo hata tukipewa miaka 1000 ya kuvifanyia utafiti, bado hatutaweza kuvipatia ufumbuzi, maana yeye aliyetuumba tayari alishatuwekea ukomo wa ufahamu wetu kwa vile ambavyo hatupaswi kuvifahamu.
 
Siwezi kukubali kwa sababu hakuna uthibitisho ambao ni convincing.Argument unayotumia ni argument ya first cause au design ambayo haina nguvu.

Ukisema binadamu mwili wake ni complex hivyo lazima awe na designer, then hata Mungu atahitaji awe na designer pia.

Je Mungu designer wake ni nani?
Kama bado tunatafautiana kuhusu uwepo ww muuundaji mkuu,itakuwa ngumu kujadili kuwa huyu alietuunda sisi na yeye kaundwa na nani.
Kwanza tujadili uwepo ama kutokuwepo kwa muundaji,tukishakubaliana kwenye hilo ndio tunaweza kuanza kujadili origin yake.
Swali langu kwako ni je tumeundwa na muundaji au la na kama hatuna muundaji tumeundikaje?.
 
Mimi nasoma biblia lakini sijaona Mungu kakataza kumhoji, Isaya 43:26 unikumbushe na tuhojiane, eleza mambo yako upate kupewa haki yako.

Mungu katoa ruksa kumhoji kwa lengo la kufaham ili tusiwe na mashaka mioyoni, shida tunayowauliza hao viongozi was dini wao pia hawayajui hapo lazima wakusukumie issue ya kukufuru.
Kwa kifupi hatujui mengi hata Yesu alilisema hilo "bado nikali ninayo mengi ya kuwambia lakini nikiwambia sasa mtaburst vichwa(mtakua machizi). Ndo maana kuna level za kujifunza level one, level two till advanced one, hivyo kaa mbele za Mungu anza kuuliza na kuhoji yeye anajua namna atakavyokuletea majibu ya matamanio ya moyo wako.
Tatizo je mtoa mada anajua namna ya kumuhoji Mungu(VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA)???
 
Unaona sasa... "Mungu ametoa ruksa ya kumhoji kwa lengo la kumfahamu..."

Ukiangalia hiyo sentensi ni kwamba, mosi unatakiwa kuamini kwanza uwepo wake na ndipo uhoji hili na lile ili upate kumfahamu vizuri! Na hata ukienda kwenye Imani 12 za Kikristo, ya kwanza kabisa ni kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu.... na ndivyo ilivyo kwa Waislamu na Wayahudi.

Kwa maana nyingine, as long as wewe ni Mkristo, tayari unakuwa umeshaamini uwepo wa Mwenyezi Mungu! Na kama umeshaamini, huwezi tena kuhoji uwepo wake!
UWONGO WA HALI YA JUU SAAAAANA.

NANI KAKWAMBIA KUWA UKISHAAMINI MUNGU YUPO BASI HUPASWI KUMUHOJI?

MBONA MIMI NAMUHOJI MUNGU NIWAPO NAYE KATIKA MAZUNGUMZO NA ANANIJIBU KATIKA MATOKEO ANAYONIAHIDI KUNIDHIHIRISHIA?

USIPOKUWA NA IMANI, BASI UMESHAFELI KATIKA KILA JAMBO SI HAPA DUNIANI TU, HATA KATIKA KUURITHI UFALME WA MBINGUNI.
 
Hatujakataa kuwa dizaina yupo ila mnapaswa kuthibitisha kuwa mnayemtaja ndo yeye haswa?
sikuliona hii comment ama skumbuki kama nilikujibu,

Ni hivi kama tunakubaliana kuhusu kuwa dizaina yupo basi mimi na wewe tuko on the same page.Kuhusu kuthibitisha kuwa nayemwamini mimi ndiye hasa huyo dizaina nadhani ni mjadala mwengine,Hoja yangu ilikuwa kuwa dizaina yupo.
 
Kwa mantiki hiyo tunategemea huyo designer atakuwa complex kuliko sisi alio tudizaini.Hivyo tutataka tujue je yeye alidizainiwa na nani? Na series itaendelea na kuendelea
Ni sawa na wewe unavyokutana na mke wako mkijamiiana akiwa katika tarehe hatarishi kwa kushika ujauzito.

Hatimaye mke wako hupata ujauzito ambapo wote hamjui namna ulivyojitunga, si sekunde, dakika, saa, siku, mwezi, mwaka wala aina ya kiumbe kilichojitunga tumboni mwa Mke kwa wakati husika wa kutungwa kwa huo ujauzito(kiumbe).

So tuwe wapole tu kwa vitu vilivyotuzidi maarifa na uwezo maana ndivyo tulivyoumbwa hivi.
 
mkuu jibu langu la haraka haraka ni kuwa dizaina yupo na zaidi ya kudizaini na kutuunda sisi pia ndiye alieunda sayari hii ambayo kwa kiasi kikubwa iko suited kwa maisha ya binaadamu na viumbe,na ndie aliyeunda laws of nature na laws of the universe,na kwakuwa yeye ndie masta dizaina wa kila kitu hata reality yake yaweza kuwa tafauti na reality yetu hapa duniani,kama imewezekana black hole kuwa tafauti na solar system yetu,kuna uwezekano pia kuna reality,logic tafauti nyengine ya uumbaji na maisha.
AMINA
 
Ni ngumu kukubaliana kwa sababu hakuna ushahidi au uthibitisho convincing.Dhana unayoitumia wewe ni argument of first cause na design ambazo zote ni mfu.

Ukisema binadamu ni complex lazima awe na designer, then hata Mungu lazima naye atatakiwa awe na designer.

Je aliyemdesign Mungu ni nani?
"ETC" END OF THINKING CAPACITY.
 
UWONGO WA HALI YA JUU SAAAAANA.

NANI KAKWAMBIA KUWA UKISHAAMINI MUNGU YUPO BASI HUPASWI KUMUHOJI?

MBONA MIMI NAMUHOJI MUNGU NIWAPO NAYE KATIKA MAZUNGUMZO NA ANANIJIBU KATIKA MATOKEO ANAYONIAHIDI KUNIDHIHIRISHIA?

USIPOKUWA NA IMANI, BASI UMESHAFELI KATIKA KILA JAMBO SI HAPA DUNIANI TU, HATA KATIKA KUURITHI UFALME WA MBINGUNI.
Pamoja na kuandika kwa herufi kubwa kama ishara ya shouting but unfortunately you're shouting out of the context!!!

Sasa ikiwa umeshaamini kwamba yupo, how come tena uhoji uwepo wake?! Unahoji vp uwepo wake wakati unadai unamuhoji wakati unapokuwa nae?!

Unahoji uwepo wake au unahoji uwezo wake?!
 
Kama bado tunatafautiana kuhusu uwepo ww muuundaji mkuu,itakuwa ngumu kujadili kuwa huyu alietuunda sisi na yeye kaundwa na nani.
Kwanza tujadili uwepo ama kutokuwepo kwa muundaji,tukishakubaliana kwenye hilo ndio tunaweza kuanza kujadili origin yake.
Swali langu kwako ni je tumeundwa na muundaji au la na kama hatuna muundaji tumeundikaje?.
Hapa ameshalazwa kwa presha, huwa wanakamatikaga katika maswali kama haya hawa viumbe.

Akishindwa kukujibu, basi ni lazima ajilete kwako kwa kukuuliza maswali mengine ambayo ni tofauti na ulivyomuuliza.

Hiyo staili huifanya ili waweze kujilinda/kujikinga(SELF DEFENSIVE MECHANISM) mara nyingi tu na kwao ni bora zaidi kuliko kushindwa/kukubali.
 
Kwa nini unakadhania muundaji na isiwe tulitokea tu,kutokana na forces kwenye space
 
Hapa ameshalazwa kwa presha, huwa wanakamatikaga katika maswali kama haya hawa viumbe.

Akishindwa kukujibu, basi ni lazima ajilete kwako kwa kukuuliza maswali mengine ambayo ni tofauti na ulivyomuuliza.

Hiyo staili huifanya ili waweze kujilinda/kujikinga(SELF DEFENSIVE MECHANISM) mara nyingi tu na kwao ni bora zaidi kuliko kushindwa/kukubali.
Hili swali wanalikimbiaga I don't know why
 
Pamoja na kuandika kwa herufi kubwa kama ishara ya shouting but unfortunately you're shouting out of the context!!!

Sasa ikiwa umeshaamini kwamba yupo, how come tena uhoji uwepo wake?! Unahoji vp uwepo wake wakati unadai unamuhoji wakati unapokuwa nae?!

Unahoji uwepo wake au unahoji uwezo wake?!
Inamaana wewe huwa huna akili?

Haujawahi kujihoji kuwa una akili/utakuwa na akili kabla ya kufanya/kuamua kutenda kitu chochote katika maisha yako?

Kwa hapo sasa ndipo inamaanisha kuwa huna akili kwa sababu unajihoji matokeo(positively & negatively) ya kitu utachokitenda kabla ya kukitenda?

Akili yako si ndiyo inayokuongoza katika kutenda jambo lolote?

Kwanini ujiulize na kujijibu kabla ya kufanya kitu chochote na kwanini hiyo akili yako ndiyo itayokuruhusu na kukuchagulia ufanye kipi au usifanye kipi na kwa muda upi?

My name is...
 
Back
Top Bottom