Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 12,463
- 27,556
Sina uhakika hapo zamani za kale Palestina waliishi wanyama.
Kiasili lile eneo ni jangwa hadi leo yaani ni kame ikiwa pamoja na Israeli.
Maandiko yanasema.
Walipofika huko kwenye mashamba ya mizabibu, mwanasimba mmoja akatokea akamngurumia Samsoni. Basi, roho ya Mwenyezi-Mungu ikamwingia Samsoni kwa nguvu, akamrarua simba huyo kama mtu araruavyo mwanambuzi.
Huyu simba kwenye mashamba ya mizabibu alitoka wapi?
Sina uhakika kama hapo zamani hizo kulikuwa misitu kiasi kwamba hata simba na wanyama wengine wali survive mwenye kujua atujurishe kwa maandiko tu. Na sio porojo.
Swali la ziada. Soma hapa
Baada ya siku chache alirudi huko Timna kumchukua huyo msichana. Alipokuwa njiani akageuka pembeni kuuona mzoga wa yule simba, na kumbe kulikuwa na nyuki ndani ya mzoga na asali. Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake.
swali
Sote tunajua yakuwa kiumbe hai hasa wanyama akisha kufa hatua inayofuata huoza na kushambuliwa na wadudu au wanyama wanakula mizoga. Hili la samsoni kuona Asali na kutoa kisha kuanza kula kwenye mzoga wa simba. Je hiyo asali ilitoka wapi?
Karibu tupeane uzoefu wa kimaandiko sio kwa ubaya tueleweshane tu.