Imeandikwa kuwa Samson alipambana na simba hadi akamuua yule simba.Swali huyo simba jangwani kama parestina alitoka wapi?

Nimekuelewa mkuu na mto nilikuwa naujua ni jordan tu nimeuliza hivyo nipate ufahamu zaidi..
 
Kilimo cha zazibu sina hakika kama kinahitaji maji bwelele maana dodoma ndo kinakubali sana
 
ungemuuliza wapi israel kuna jangwa? mbona wanalima zabibu tangu hata Yesu hajazaliwa? mbona Ibrahim alifuga mifugo pale majani angepata wapi jangwani? mbona Mfalme Daudi alilima na kufuga, mbona suleiman alikata misitu kadhaa pale kujenga hekalu ambao waislam walikuja kulivunja pale dome of the rock, mbona enzi na enzi hadi leo na kesho wanalima mizeituni (olives) ambazo zinazalisha mafuta ya mzeituni yanasambazwa dunia nzima? hii inamaanisha palikuwa sio jangwa, palikuwa na majani, palikuwa na wanyama poari, simba, mbwa mwitu, dubu ambaye hata Daudi alimuua machungani etc.
 
Ni sahihi nimeongeza maarifa
 
Kuna simba wanaitwa Mountinous Lion au Cougar au Puma ni Species ya simba kwenye maeneo hayo! hao wanapatikana sana kwenye majabari makubwa huko..kama ulishawahi kuona filamu ya Samson utaona haikua jangwani alipopambana na simba bali ilikua kwenye mamilima makubwa yenye majabari ya mawe... et.c
 
Labda ile simba ya jana iliyochapwa mbili huko uarabuni...😁
 
Shukrani
 
Simba aliyeuawa na daudi alitolewa mbuga ya Serengeti hadi mashariki ya kati kwa kutumia merikebu iliyokuwa ya mfanyabiashara mmoja wa pale mikindani.

Una swali lingine?
 
Simba wa Jangwani ndio Simba wakubwa kushinda wote, sasa hivi wanapotea ila wapo wachache bado.

Unaona Morocco timu ya Taifa? Wanaitwa Atlas lion, Jina jengine La Atlas lion ni Barbarian lion, Huyu simba anapatikana Jangwa la Sahara North Africa yote ile hadi Egpty, pia anapatikana Ulaya Kusini na Asia Magharibi.

Atlas lion ndio simba mkubwa kushinda wote kizazi chetu hiki. Anakuwa na manyoya mengi hadi kwenye Tumbo mixer gold na nyeusi


Pia Ukitoa huyo Atlas Lion kuna simba wengine wanaitwa Asian lion/Persian lion, walikuwepo pia huo ukanda hasa maeneo ya Palestina, sema hawa ni wadogo wadogo na hawana hayo manyoya (Mane) ya kutosha kama Barbarian.

Pia kuna ushahidi wa masalia/Mabaki ya hao simba hayo maeneo ukitrace maelfu ya miaka, hivyo ushahidi wa kisayansi pia unaonesha kulikua na simba miaka hio.
 
Mkuu,

Kwa mujibu wa maandiko kuonekana kwa Simba mazingira yasiyo taraji ulikuwa ni mpango wa Mwenyezi Mungu kuwafifisha Wafilisti dhidi ya Waisraeli.

Hivyo Simba alitumika kama mnyama wa kuogopeka, mwenye nguvu na mkali kuliko wanyama wote.

Samsoni kupatiwa mamlaka na nguvu za kumuua Simba ni njia ya kuwadhihirishia Wafilisti kuwa wao si kitu kwa Samsoni, kuwa kama ameweza kumrarua Simba iweje binadamu?

Pia, uwepo wa nyuki na asali ni mpango wa Mungu kuendelea kujidhihirisha kupitia Samsoni, nyuki ni wakali ndiyo lakini Samsoni aliweza hata kupakua ile asali pasipo kudhuriwa na nyuki.


Mtazamo wangu kulingana na maandiko
 
Mkuu watu mnajua mambo hadi raha asee.Napata vingi vingi kuliko hata nilivyokusudia asee.Shukrani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…