Imebaki masaa machache sana wajisahaulishe kuwa twapaswa kuanza awamu ya sita na sio kuendeleza awamu ya tano

Sio kisheria ni lugha tu iliyozoeleka
Kisheria awamu ina miaka 10. kila awamu moja ikiwa na mihula miwili,muhula mmoja ukiwa na miaka mitano.
awamu ya JPM haikuisha, mama samia ana inherit awamu ya JPM ambayo ya tano, kumalizia vipindi vyake. japo ni Rais wa sita.
kwenye awamu hatuangalii Rais.
 
Sio kweli kama ndio hivyo hii ingekuwa awamu ya 7
 
Hii ni awamu ya tano Rais wa sita. Awamu ya sita bado mpaka uchaguzi mkuu ujao. Awamu huingia madarakani kwa uchaguzi na endapo aliyepita atashinda basi ataendeleza awamu yake.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Kwahiyo unataka kusema uchaguzi huu angepita LISSU ingekuwa awamu ya 5?
 
Kwa mujibu wa katiba rais anapofariki au kushindwa kuendelea na majukumu yake kwa sababu ya maradhi au sababu nyingine iliyoainishwa na katiba basi makamu wa rais atachukua nafasi ya urais na ikiwa muda uliobaki ni zaidi ya miaka mitatu katika ile miaka mitano basi rais aliyechukua madaraka itahesabika hiyo ni awamu yake ya kwanza na ataruhusiwa kugombea tena mara moja tu yaani kwa sasa Mama Samia ataruhusiwa kugombea tena 2025 ikiwa atashinda basi hiyo ndiyo itakuwa awamu yake ya pili na ya mwisho lakini ingekuwa Magufuli amefariki na kubakisha chini ya miaka mitatu basi ndio ingekuwa Samia anamalizia awamu ya Magufuli baadaye angeruhusiwa kugombea awamu zake mbili, hivyo hapo utaona Mama Samia ni rais wa awamu ya sita na hivi sasa inahesabika ni awamu yake ya kwanza.
Good
 
Mwisho wa marumbano samia suluhu hasani hawezi kuwa magufuri, kiutendaji na hata kitabia japo wengi wanatamani awe kama magufuri hilo halitawezekana,

Atatekeleza miradi sawa, atatumbua majipu sawa, atafanya kila alicho fanya magu lakini hawezi kuwa kama magu.mkae mkijua hivyo.

Mwisho, musiba na makonda ambao mnajiita veronica na joyce mmepata ujumbe wa mzee wa msoga.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Awamu ya sita ni jina tu ila ilani inayotekelezwa ni ile aliyoinadi Magu 2020-2025.

Kitendo cha Samia kutoonekana akiwa na barakoa wala kutilia mkazo juu ya hilo ni ushahidi tosha kuwa ataendeleza mabaya na mazuri ya mtangulizi wake.

Sioni jipya na wala halipo.
Muda ukifika ataivaa tu, kwani mdudu Bado yupo hasa ikulu

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Wewe utakuwa ulikula ban ukafungua ID nyingine
Kweli kabisa - halafu nikaomba kusamehewa wakagoma! Basi tena nimeanza upya wakati nilishakuwa na posts Zaidi ya elfu 40.
 
Mwisho wa marumbano samia suluhu hasani hawezi kuwa magufuri, kiutendaji na hata kitabia japo wengi wanatamani awe kama magufuri hilo halitawezekana,

Atatekeleza miradi sawa, atatumbua majipu sawa, atafanya kila alicho fanya magu lakini hawezi kuwa kama magu.mkae mkijua hivyo.

Mwisho, musiba na makonda ambao mnajiita veronica na joyce mmepata ujumbe wa mzee wa msoga.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Tehe tehe!
 
Kuna dereva mmoja wa bus la abiria alikuwa hapendi kuandamana na kondakta anaejua kuendesha kwa kuhofia kuwa anaweza kumfunika na pengine kumbishia kitu asichokubaliana nacho. Hivyo alipopewa nafasi na tajiri yake ili kutafuta kondakta wa kumsaidia kazi yeye alimtafuta mtu ambaye kwanza hakuwa na ujuzi wowote wa kuendesha gari na pia alihakikisha kwamba huyo kondakta muda wote yeye atakuwa mtu wa kuitikia kila atakalosema yeye. Siku moja wakiwa katikati ya safari dereva huyo aliugua tumbo la kuhara na hivyo akashindwa kuendesha gari. Abiria walibaki njia panda.
 
Stori za vijiweni hizi kuvuta siku iishe fasta.
 
Back
Top Bottom