Imefichuka kuwa Wafanyakazi wa Mossad walivamia mtandao wa kamera za trafiki za Tehran kwa miaka kadhaa

Imefichuka kuwa Wafanyakazi wa Mossad walivamia mtandao wa kamera za trafiki za Tehran kwa miaka kadhaa

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Imefichuka kuwa Wafanyakazi wa Mossad walivamia mtandao wa kamera za trafiki za Tehran kwa miaka, wakifuatilia harakati za Ayatollah Ali Khamenei,walinzi wake, na maafisa wengine wakuu wa Iran kabla ya mauaji yake, kulingana na ripoti.

Israel ilipata ufikiaji wa karibu kamera zote za jiji, ambazo Iran zinatumia sana kufuatilia wapinzani wa utawala na raia wake wenyewe.

kwa kina makazi ya walinzi, ratiba zao za kazi, na ni nani walinzi walilindwa.
Picha hizo zilitumwa hadi Tel Aviv na sehemu za kusini mwa Israel.
Moja ya pembe za kamera ilikuwa muhimu sana, ikiruhusu mawakala kufuatilia mahali walinzi walipoweka magari yao ya kibinafsi walipofika kwenye makazi ya Kiongozi Mkuu kwenye Pasteur Street katikati ya Tehran.

Uvamizi huu ulikuwa sehemu ya kampeni ya ujasusi iliyodumu kwa miaka, ambayo hatimaye ilisababisha kuuawa kwa Khamenei Jumamosi, baada ya ndege za kivita zilizotokea moja kwa moja kutoka kambi za kijeshi za Israeli kuzipiga mabomu hadi 30 ya usahihi kwenye makazi yake.

Miili ya walinzi wa Kiongozi Mkuu ilipatikana chini ya mabaki baada ya shambulio la mchana lililolenga kuondoa utawala. Khamenei alitawala kwa miaka 36.

Wakati Israel ilipopata eneo la Khamenei asubuhi ya Jumamosi, waliharibu minara karibu 12 ya simu za mkononi karibu na Pasteur Street,kufanya simu zake zichukue kuwa zenye shughuli nyingi na kuzuia walinzi wake kupokea onyo lolote.
 
1772544933045.png

Marehemu Ali Khamenei


News in-depth Middle East war
Inside the plan to kill Ali Khamenei

Soma zaidi kupitia link hii: Client Challenge

Mpango wa kumuua aliekuwa kiongozi mkuu wa Iran (Supreme Leader) Ayatollah Ali Khamenei ulifanywa kwa zaidi ya miezi mitatu majasusi wa Mossada na CIA wakipanga kila kitu.

Mara nyingi majasusi wanapokuwa katika mipango yao kuhusu "Target" waliemchagua humweka chini ya uangalizi na ufuatliaji (Surveillance) na hapohapo huwa na vyanzo mbalimbali vya kupata taarifa za papo kw ahapo (real-time feed) na hichi ndicho kilotokoea kwa Khamenei na kundi zima la makamanda wake na viongozi wengine wa ngazi za juu.

Siku ya jumamosi ilopita, Khamenei alikuwa ana mkutano wake na viongozi wote wa ngazi za juu wa jeshi, baraza la mapinduzi na baraza la usalama na viongozi wa serikali ambao ni tofauti kabisa na uongozi ulioko chini ya serikali ya Iran ambayo yaongozwa na raisi Masoud Pezeshkian.

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti hilo la FT, majasusi wa Mossad na CIA ambao wamekuwepo nchini Iran na kupafanya kama mitaa wa Narung'ombe na Nyamwezi pale Kariakoo waliweza kuuingilia (hacking) mfumo wa taa za barabani na mfumo wa minara ya simu ili kuwazuia walinzi wa Khamenei wasiweze kuwasiliana pale ambapo pangetokea tishio lolote.

Mmoja wa majasusi hao ambae hakupenda kutajwa jina lake alisema wahifahamu Tehran kama wanavyoifahamu Jerusalem na pale unapokuwa ukilifahamu eneo khasa lile ulilokulia na mitaa yake yote ni lazima utabaini mabadiliko yoyote yale hata yale madogo.

Hivyo hapa yaonyesha wazi kulikuwa na vyanzo kadhaa vya kusaidia mpango huo wa kijasusi vikiwemo mfumo wa taa za barabarani, minara ya simu na pia binadamu au majasusi ambao wapo ndani ya eneo husika.

Uamuzi wa kumshambulia Khamenei na wasaidizi wake wote ulifikiwa baada ya kubaini kuwa siku hiyo ya jumamozi alikuwa akikutana na viongozi hao kupanga mambo yote ambayo leo hii Iran yatekeleza ikiwemo kushambulia nchi jirani za kiarabu jambo lilopelekea kuwepo na vita kubwa katika eneo lote la ghuba.

Hivyo twaweza kuona kwamba kazi ya ujasusi pia huitaji watu ambao wa ujuzi mkubwa masuala ya teknolojia na pia uwezo mkubwa wa kuchambua taarifa (intelligence analysis) na hapohapo ukiunganisha mauaji ya Hassan Nasrallah, raisi wa Iran Ibrahim Raisi, na viongozi wengine wa kijeshi utaona kwamba majasusi wa kileo khasa wa nchi kama Israeli wapo katika ngazi ingine kabisa.

Kwa kupanua wigo wa elimu hii ya ujasusi na pia uelewa wa masuala haya ya kimataifa na jiografia ya kisiasa soma gazeti hii la FT na vyanzo vingine lukuki vilivyopo katika mfumo wa kiintelijensia au "Open Source Intelligence".

Je, nini maana ya Open Source Intelligence au OSINT?

Huu ni mfumo wa tovuti ambazo zatoa njia na vyanzo vya kupata habari na taarifa ambazo zipo bure kwa ajili ya kufanya utafiti, uchunguzi pamoja ya usalama wa mitandao au Cyber Security.

Kwa wale wanonisoma "between the lines" watanielewa.

Vyanzo: Client Challenge
 
Swali , waliwezaje kuvamia hizo camera za traffic?

WAnanchi wa Iran wamechoshwa na serikali ya misimamo mkali wa ki Islam.(Ndipo usaliti unapotokea).
Iran wangekuwa na msimamo wa wastani kama Dubai, wangekuwa wako mbali sana 😂
 
Imefichuka kuwa Wafanyakazi wa Mossad walivamia mtandao wa kamera za trafiki za Tehran kwa miaka, wakifuatilia harakati za Ayatollah Ali Khamenei,walinzi wake, na maafisa wengine wakuu wa Iran kabla ya mauaji yake, kulingana na ripoti.

Israel ilipata ufikiaji wa karibu kamera zote za jiji, ambazo Iran zinatumia sana kufuatilia wapinzani wa utawala na raia wake wenyewe.

kwa kina makazi ya walinzi, ratiba zao za kazi, na ni nani walinzi walilindwa.
Picha hizo zilitumwa hadi Tel Aviv na sehemu za kusini mwa Israel.
Moja ya pembe za kamera ilikuwa muhimu sana, ikiruhusu mawakala kufuatilia mahali walinzi walipoweka magari yao ya kibinafsi walipofika kwenye makazi ya Kiongozi Mkuu kwenye Pasteur Street katikati ya Tehran.

Uvamizi huu ulikuwa sehemu ya kampeni ya ujasusi iliyodumu kwa miaka, ambayo hatimaye ilisababisha kuuawa kwa Khamenei Jumamosi, baada ya ndege za kivita zilizotokea moja kwa moja kutoka kambi za kijeshi za Israeli kuzipiga mabomu hadi 30 ya usahihi kwenye makazi yake.

Miili ya walinzi wa Kiongozi Mkuu ilipatikana chini ya mabaki baada ya shambulio la mchana lililolenga kuondoa utawala. Khamenei alitawala kwa miaka 36.

Wakati Israel ilipopata eneo la Khamenei asubuhi ya Jumamosi, waliharibu minara karibu 12 ya simu za mkononi karibu na Pasteur Street,kufanya simu zake zichukue kuwa zenye shughuli nyingi na kuzuia walinzi wake kupokea onyo lolote.
Pitia hiki kitabu mkuu
 

Attachments

Back
Top Bottom