Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Kuna siasa nyingi sana linapokuja swala la mishahara na maslahi mengine ya watumishi wa umma. Kote huko halmashauri hadi serikali kuu mishahara ni ya TGS ambayo ni kiduchu ukilinganisha na uhalisia wa maisha ulivyo.

Serikali kulipa mishahara bila allowances nyingine kama nyumba, usafiri kwenda na kurudi kazini, simu, maji, umeme, posho ya chakula kazini ni unyonyaji ulio wazi kwa watumishi. Ni heri serikali iwe na watumishi wachache inaowajali kuliko kuwa na utitiri wa watumishi ambao wengi wanaonekana kama waliopigika sana na maisha.

Jana nilikutana na watumishi wa halmashauri ambao tulikuwa intake moja, yaani ukiona hata mwonekano wa sura na kimavazi unahisi kabisa kuna ugumu mkubwa kwenye vipato vyao. Serikali saidieni watumishi wa umma angalau wa maintain hadhi zao, ni aibu!​
 
Pm MAJALIWA aliunda TUME ya kuharmonise mishahara mashirika ya umma na serikali na local authorities Hadi Leo ripoti haijawekwa hadharani. Kwa kweli Mimi ni mmoja wapo wa wananchi nisiyekuwa na Imani na PM achilia Ile kamba alotupiga eti RAIS NI MZIMA ANAENDELEA NA MAJUKUMU YAKE.....
Tangia hapo yule baba simwelewi Hadi kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…