Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Kuna siasa nyingi sana linapokuja swala la mishahara na maslahi mengine ya watumishi wa umma. Kote huko halmashauri hadi serikali kuu mishahara ni ya TGS ambayo ni kiduchu ukilinganisha na uhalisia wa maisha ulivyo.

Serikali kulipa mishahara bila allowances nyingine kama nyumba, usafiri kwenda na kurudi kazini, simu, maji, umeme, posho ya chakula kazini ni unyonyaji ulio wazi kwa watumishi. Ni heri serikali iwe na watumishi wachache inaowajali kuliko kuwa na utitiri wa watumishi ambao wengi wanaonekana kama waliopigika sana na maisha.

Jana nilikutana na watumishi wa halmashauri ambao tulikuwa intake moja, yaani ukiona hata mwonekano wa sura na kimavazi unahisi kabisa kuna ugumu mkubwa kwenye vipato vyao. Serikali saidieni watumishi wa umma angalau wa maintain hadhi zao, ni aibu!​
 
Kaskia
20230329_162826.jpg
 
Salaam ndugu Wana JF...

Naambiwa "Mama" yetu raisi wetu huwa anasoma humu JF.

Kwa heshima na taadhima naomba asome na hii.

Twende kwenye hoja..

Leo hii Kuna jamaa yangu kutoka halmashauri ya jirani kapata uhamisho kutoka halmashuri yake kwenda chuo cha Mandela (Arusha) yaani kwa huo mshahara anaoendea mpaka nimeshangaa.

Huyu jamaa basic analipwa TGS D = 745k ukitoa makota inayoingia mfukoni ni 500k and something.

Ila sasa huko aendako atakuwa analipwa basic 1.8Mil.

Hili limenifanya nijiulize ""KWANINI HALMASHAURI WANALIPWA KIDOGO KULIKO WATU WOTE SERIKALINI?""

Sometimes naonaga kama kufanya Kazi serikalini ukiwa chini ya TAMISEMI kama ni "laana/Majanga" maana kwenye mshahara huku ni dah "Ashukuriwe Mungu"

Hivi jiulize...
Tax Officer TRA Kazi yake ni kukusanya kodi, ada na tozo na Afisa mapato Halmashauri kaz yake nae ni kukusanya kodi na ushuru.
Mbona sasa huyu Tax Officer (accounts) analipwa zaidi ya Afisa mapato wa Halmashauri (accounts)..???

Hawa wawili, wamesoma course moja, chuo kimoja, wakaajiriwa na serikali moja ila tu kwasababu ya huyu yupo taasisi na huyu yupo "Local government" basi huyu anashavu zaidi ya huyu..!!
Why this, ikiwa wote wapo chini ya serikali moja?

Mishahara ya halmashauri inachekesha hasaa.
Ukiachana na afya ambao kidogo wao "alhamdulilahi ila"
1. Ukisoma diploma mshahara ni TGS C = 500k take home 400k
2. Ukisoma Bachelor ya miaka 3
TGS D = 700K take home 500k
3. Ukisoma Bachelor ya miaka mi4 ni TGS E = 900K take home 700k

(Mishahara hii nime approximate kwa kukaribisha zeros at the end)

Na kengine huku Halmashauri hizi masters na short course hazina hata maana ki-mshahara zaidi ya kwamba ni "Added advantage" ila sio ki-financial aspect HAKUNA LOLOTEE.
Unakuta wewe una masters na mwenzio bachelor ila mshahara mnafanana.

Huwa nawaambia madogo ""Njoo halmashauri tafuta cheki namba halafu sepa huko kwenye mishahara minono"".
Kwani nani asiyependa kufanya Kazi kwenye mshahara mkubwa?

Haiwezekani uliosoma nao wote mpo serikalini ila wao wana mishahara na maposho zaidi yako kisa wewe upo local government...!!!

Kwa upande mwengine.
Ukiangalia bungeni wanatupa sanaa lawama kwa Halmashauri huku wanasahau kuwa watumishi wao bungeni wana mishahara mikubwa kuliko wa halmashauri.

Yaani halmashauri inasemwa sanaa juu ya wizi ila HAKUNA MTU YEYOTE ANAYEONGEA KUHUSU UDOGO WA MISHAHARA YA HALMASHAURI.

Sijawahi hata siku moja kusikia taasisi yoyotee nchini ikiongelea maslahi ya watumishi wa Halmashauri zaidi ya kuwalaumu.

KUHUSU POSHO.
Watu wanakwambia "Halmashauri wanajilipa posho sana"

Wanasahau kuwa, posho ni mapato ya ndani "own source" na kuna Halmashauri hayo mapato ya ndani HAKUNA.

Hivi halmashauri kama Ukerewe, Tanganyika, Momba, Mpimbwe, Ileje WANAJILIPA MAPOSHO kwa mapato gani?
Ikiwatu makusanyo yao hat Bil 2 kwa mwaka hakuna (maana vyanzo vya kukusanyia hakuna).
Sasa Hawa hizo posho wanapata wapi?

MAMA HALI NI MBAYA.
Watumishi wa Halmashauri Wana hali mbaya.
Achana na hizi Halmashauri za mjini, ila hizi Halmashauri za vijijni watu Wana hali mbaya na ""Asilimia 90 ya watumishi wanapigana na kuhangaika ili wahame"" maana hakuna anayekubali mshahara mdogo huku kwenye mkubwa panaonekana.

Imefika wakati hii mishahara ya Halmashauri iangaliwe.
Inakuaje mtu mwenye bachelor yake ya uhasibu kaajiriwa tokea 2015 mpaka leo mshahara ni 745,000/= yaani ukitoa kodi kinachobaki ndio aendeshee maisha.

Walimu nao wanateseka.
Hizo TGTS C, D, E, F ukizisoma utadhani ni pesa nyingi.
Sasa ngoja uandikiwe ni kiasi gani UTABAKI KUSHANGAA.

Unakuta mwalimu kasoma na mwenzake Bach. Ed
Huyu kawa mwalimu wa sekondary huyu kaajiriwa assistant tutor.
Sasa ukitaka kuona ""maajabu cheki mishahara yao""

Tutor ana mshahara kuliko mwalimu. Bila kusahau Tutor anaposho za vipindi na vitu vyengine ila yeye mwalimu kwanini asiwe na posho za vipindi?

Kuna Watu wapo taasisi huko WANALIPWA mishahara mara tatu ya halmashauri.

Madereva...
Katika fani nayoonea huruma ni walimu na madereva.

Kwani Kuna utofauti gani wa dereva wa BOT, Wizara na Halmashauri?

Hivi V8/gari si ileile na gia si zilezile na lami si ileile, KWANINI Dereva wa Halmashauri ana TGS B na wengine WANALIPWA mara mbili yake?
Au magari yao wao yanapaa na ya halmashauri yanatembea kwenye lami?

HII SI AFYA KABISA.

Nina mengi ya kuongea NAOMBA NIISHIE HAPO.

Mama Niko chini ya miguu yako NAOMBA HILI LITAZAMWE.

Mishahara ya Halmashauri ni nomaaa Raisi wangu.

Asante.

#YNWA
Pm MAJALIWA aliunda TUME ya kuharmonise mishahara mashirika ya umma na serikali na local authorities Hadi Leo ripoti haijawekwa hadharani. Kwa kweli Mimi ni mmoja wapo wa wananchi nisiyekuwa na Imani na PM achilia Ile kamba alotupiga eti RAIS NI MZIMA ANAENDELEA NA MAJUKUMU YAKE.....
Tangia hapo yule baba simwelewi Hadi kesho.
 
Back
Top Bottom